Boda boda kila siku watu wamapata ajali Dar

Boda boda kila siku watu wamapata ajali Dar

Juzi nilipanda Moja naenda kariakoo aisee hadi nafika nilisema Asante Mungu
Njiani anapokea sim anaweka kwenye kofia anaanza kelele
Kamuona dada kwenye boda nyingine anasogelea ampige Kofi la mgongo wanaanza story
Uzoefu wa barabara zero kabisa
Anyway pole mno kwa wafiwa kwa kweli ni vifo vibaya maana ni ghafla sana
 
Mozambique hakuna bodaboda.kule walipiga marufuku na wakapunguza kodi ya magari pamoja na bajaji.watu wa msumbiji wengi wanamiliki magari tofauti na sisi kodi ya gari ni sawa na bei uliyonunulia huko ulaya
Uko sahihi Msumbiji wananchi wengi wana magari yao binafsi, na km sivyo usafiri wa umma ni ma bus au coaster.

Kuanzia Lichinga hadi mpea, malulu hadi Maleta, kote huko. Hukuti boda hovyo.
 
Hivi kwani kabla ya bodaboda tuliishije? Au kuna ongezeko la watu kiasi inalazimika kutumia bodaboda?
Mkuu kipindi icho tulikua tunatumia baiskeli, kama hamna baiskeli basi kutembea kilomita 5 mpaka 10 haikua issue.

Sasa hivi mahitaji ya nyumbani yanafanywa na boda (wangu) safari fupi tu bodaboda huyu hapa, watu wameona fursa kubwa kwenye kurahisisha maisha ya watu ukichanganya pia ajira imekua ngumu.
 
Leo naona mnatupondea maafisa usafirishaji mnasahau sisi ndo tunaowajazia mikutano yenu ya chama chenu pendwa cha CCM alafu Leo mnatusuuza daaaah inasikitisha🖐️
 
Alafu utatuajiri kwenye biashara zako mkuu?? Au ndo tukianza kuwapiga kabari za mbao mnaanza kuleta nyuzi kuwa vijana hawafanyi kazi
Kabla ya bodaboda watu waliishije? Hizo takataka zinaongeza vilema na vifo tu.
 
Kwasababu vifo ni vya mafukara na watoto wa masikini msitarajie Sheria zozote kubadirishwa!


Hadi pale watoto wa vibopa wakifa Kwa Bodaboda
 
Juzi nilipanda Moja naenda kariakoo aisee hadi nafika nilisema Asante Mungu
Njiani anapokea sim anaweka kwenye kofia anaanza kelele
Kamuona dada kwenye boda nyingine anasogelea ampige Kofi la mgongo wanaanza story
Uzoefu wa barabara zero kabisa
Anyway pole mno kwa wafiwa kwa kweli ni vifo vibaya maana ni ghafla sana
Ukimwambia aendeshe Pole Pole na awe mstaaharabu hakuelewi kwani?
 
Kabla ya bodaboda watu waliishije? Hizo takataka zinaongeza vilema na vifo tu.
Mkuu tatizo ni nchi yetu kuwa na upungufu wa ajira kwa vijana na hata miaka ya nyuma kabla ya boda boda kumbuka vijana waliamua kujiajiri kwenye Daladala za baiskeli. Kwa hiyo tusilaumu boda boda na mkiwalaumu au kutaka kusitisha hiyo ajira Yao je mmewawekea mazingira yapi baada ya kuacha kazi ya boda boda? Au tuhamie kwenye ujambazi muanze kulala saa 12 kama kipindi kile cha panya road.

Alafu msisahau sisi boda boda tuna vikosi vyetu vya majina ya 32 na 45 sasa jichanganyeni tuache boda boda tuunganishe vikosi kama hamjaanza kulala saa 12
 
Kiukweli barabarani ni boda tu wanaongoza kwa uvunjifu wa sheria na matumizi salama ya barabara,wengi wa madereva wa vyombo vya moto wapo rough na hawajali wa upande wa pili.
Mimi huwa nawaza vitu viwili,vyombo vya moto/kawaida vijitegemee/ziwe na njia tofauti,pia kila barabara ya lami inayojengwa basi walau iwe double road kama tatizo ni bajeti ni Bora ibaki barabara ya vumbi kuliko kupoteza watu kwa ajali mbaya ama kuwapa ulemavu.
Ingependeza pia speed ya vyombo idhibitiwe kama walivyofanya kwenye buses kipindi fulani.
 
Nawashangaaga abiria wamelipa nauli hafu wanaendeshwa ovyo ovyo na bodaboda. Sometimes hadi dereva boda anaenda opposite lane hafu liabiria limekenua tu
 
Back
Top Bottom