Bodaboda aliyedaiwa kutekwa -afunguka - "alitoa bunduki - hawafananii na polisi nikaogopa"

Bodaboda aliyedaiwa kutekwa -afunguka - "alitoa bunduki - hawafananii na polisi nikaogopa"

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
.

View: https://m.youtube.com/watch?v=4upFAaJHGvg
Niliona gari yenye vioo vyeusi aina ya Alphard ikinifuatilia ... Rajab Hassan almaarufu Marco Charlie nikiwa Tumbi Kibaha nikaona watu wanataka kuniteka .. nikatumia njia za medani kuwakwepa nikaenda chama cha mabodaboda ... sasa wakati nikiwa na viongozi wa bodaboda tukaiona gari katika shell kituo cha mafuta..

Wakaniuliza kwanini utatuletea nzi hapa shell ndipo mkaona katika video hao wasiojulikana tuliotaka kuwafahamu wakaanza kunishambulia na kunichukua kwa nguvu ndani ya gari hadi kituo cha Polisi, ...

Pale kituoni Polisi sikupelekwa counter kuandikshwa bali nilipitishwa uani na kuingizwa katika ofisi na kutupwa chini nyuma ya meza ili nisionekane wakati ndugu na marafiki waliopokuwa wanafutilia nipo kituo gani cha polisi

Soma Pia:

Niliendelea kupigwa kichapo kwa kutumia chepeo ambalo askari rastaman dreadlocks alinishambulia kisha akaja mwingine na ubao wakaendelea kunishambulia...

Nikanyimwa dhamana na nikatupwa selo ...
 
Hapo awali :
:FIRE:
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi ilisema hivi :

22 February 2025

Polisi yakiri kumshikilia aliyekamatwa kwa nguvu kibaha, Yaanika sababu za nguvu kutumika


View: https://m.youtube.com/watch?v=qGgveyf5qig

Jeshi la Polisi limesema video inayosambaa ikimuonesha dereva bodaboda akikamatwa kwa nguvu katika eneo la Maili Moja, Kibaha mkoani Pwani Tanzania ni askari walikuwa wanamkamata mhalifu ambaye alikaidi.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Februari 22, 2025 katika kurasa zao za mitandao ya kijamii zimesema kuwa kijana huyo anatuhumiwa kufanya uhalifu kwa kutumia pikipiki maarufu ‘vishandu’.

“Picha hii mjongeo iliyopo kushoto inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na watu mbalimbali kutoa maoni yao ni tukio la ukamataji lililofanywa na askari Polisi Februari 20, 2025 katika eneo la Maili Moja, Mkoa wa Pwani.

“Mtuhumiwa huyo Rajabu Hassan alikuwa anatafutwa kutokana na tuhuma mbalimbali za kujihusisha na matukio ya uporaji kwa kutumia pikipiki ikiwa imekunjwa namba za usajili (plate number) na wakati mwingine ikiwa haina namba ya usajili kwa jina maarufu Vishandu,” imeeleza taarifa hiyo.


Taarifa hiyo imeongeza kuwa: “Hata wakati anawakimbia polisi walipojaribu kumkamata na kuwakimbia katika eneo la Mwendapole pikipiki aliyokuwa anaendesha ilikuwa haina namba ya usajili.

Baadaye Polisi walipofanikiwa kukamata katika eneo la Maili Moja ilikuwa haina namba ya usajili. “Wakati wa ukamataji alianzisha vurugu ili kukaidi ukamataji pamoja na askari kujitambulisha kwake hata hivyo walifanikiwa kumkamata na kumfikisha Kituo cha Polisi Kibaha ili kuendelea na taratibu nyingine za kisheria kuhusiana na tuhuma zinazomkabili,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na msemaji wa Jeshi la Polisi imeeleza kuwa ndugu zake wanazo taarifa kuwa anashikiliwa katika kituo hicho.
 
Tukio la Kibaha mkoa wa Pwani Tanzania limesababisha maoni mgongano katika mitandao ya kijamii

1740241182153.jpeg
 
22 February 2025
Tumbi, Kibaha
Pwani
Tanzania


HUYU HAPA BODABODA ALIYEDAIWA KUTEKWA -AFUNGUKA - "ALITOA BUNDUKI - HAWAFANANII na POLISI NIKAOGOPA"...ASIMULIA MKASA MZIMA BAADA YA KUACHIWA...

View: https://m.youtube.com/watch?v=4upFAaJHGvg
Niliona gari yenye vioo vyeusi aina ya Alphard ikinifuatilia ... Rajab Hassan almaarufu Marco Charlie nikiwa Tumbi Kibaha nikaona watu wanataka kuniteka .. nikatumia njia za medani kuwakwepa nikaenda chama cha mabodaboda ... sasa wakati nikiwa na viongozi wa bodaboda tukaiona gari katika shell kituo cha mafuta..

Wakaniuliza kwanini utatuletea nzi hapa shell ndipo mkaona katika video hao wasiojulika tuliotaka kuwafahamu wakaanza kunishambulia na kunichukua kwa nguvu ndani ya gari hadi kituo cha Polisi nikatupwa selo ...

Kuna kila sababu sasa Wananchi wamilikishwe silaha kwa Ulinzi binafsi.
Suala la kila Mwananchi Mtu mzima mwenye akili timamu kumilikishwa silaha iwe ni Haki ya msingi kwa kila raia ili kujihakikishia Ulinzi binafsi.

Kwa sasa nimeelewa vizuri ni kwa Nini hasa raia wa Marekani hawataki kubadilisha Sheria za nchi yao zinazotoa Haki kwa kila raia kumiliki silaha.
 
Hawa bodaboda wakwapua vitu akina mama ndio wahanga wakubwa na pochi zao

husogeza pikipiki akiwa mwanamke amebeba pochi yake akiwa anatembea kwa miguu au akiongea na simun hunyakua kwa spidi ya mwewe na kukimbia na pikipiki

Wanawake wanawajua vizuri asante jeshi la polisi

Majambazi ya Chadema na watetezi wa hao Majambazi walioko Chadema hawajui hayo au hufanya kusudi sababu ni Majambazi wenzao waliojificha Chadema
 
Hawa bodaboda wakwapua vitu akina mama ndio wahanga wakubwa na pochi zao

husogeza pikipiki akiwa mwanamke amebeba pochi yake akiwa anatembea kwa miguu au akiongea na simun hunyakua kwa spidi ya mwewe na kukimbia na pikipiki

Wanawake wanawajua vizuri asante jeshi la polisi

Majambazi ya Chadema na watetezi wa hao Majambazi walioko Chadema hawajui hayo au hufanya kusudi sababu ni Majambazi wenzao waliojificha Chadema
Shida inakuja unatofautisha vipi polisi na wahalifu polisi hawana uniform, wana tatoo, kama anavyosema. Utajuaje kama ni askari?
 
Shida inakuja unatofautisha vipi polisi na wahalifu polisi hawana uniform, wana tatoo, kama anavyosema. Utajuaje kama ni askari?

Tatizo hili bado ni sugu, polisi na serikali hawataki kulitafutia ufumbuzi.
Nia ni kuwa na taifa la wananchi waoga, na hivyo raia wasiohoji ni rahisi kuwaswaga katika kila hali ikiwemo kuwanyanyasa, kuwapora, kufanya uchafuzi katika uchaguzi, n.k

TOKA MKATABA :

10 February 2023

Tume ya Haki Jinai
waanza kuhoji Wakuu wa Polisi na wakuu wa .... ikiwa pamoja na kuangalia utendaji wa taasisi zilizopo ktk mfumo wa haki jinai.... ..

View: https://m.youtube.com/watch?v=26myjssYvAo

Mwenyekiti jaji Chande anasema kuna upungufu au mmomonyoko wa imani za wananchi kuhusu taasisi zilizopo ktk mfumo wa haki jinai pia jaji Chande awaomba raia kutoa maoni yao kuhusu utendaji wa taasisi hizo .. kwa kutuma maoni yao ktk anuani za mawasiliano za tume hiyo zilizopo twitter, FB, email, WhatsApp na simu.

Pia Toka maktaba :
Taarifa iliyotolewa jana Januari 6, 2023 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus imewataja wajumbe hao;
Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha taasisi za Haki Jinai nchini inayoongozwa na Mwenyekiti Jaji Mohamed Othman Chande na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue. Wajumbe wengine ni pamoja na:

  • Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dk Eliezer Feleshi,
  • Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais (Utumishi) Dk Laurean Ndumbaro,
  • Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP mstaafu Said Mwema
  • na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP mstaafu Balozi Ernest Mangu.
  • Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Dk Edward Hosea,
  • Askari Polisi mstaafu, Saada Makungu,
  • Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco Omar Issa,
  • Ofisa mwandamizi Ofisi ya Rais Baraka Leonard
  • na Mkurugenzi wa Utafiti katika Chuo Kikuu cha Zanzibar na Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Yahya Khamisi Hamad
RIPOTI YA TUME YATUA KATIKA DAWATI LA MHESHIMIWA RAIS
1740242830133.png

Picha : Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed

Hotuba ya Mhe. Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai akiwasilisha taarifa rasmi ya Tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za Haki Jinai hapa Nchini tarehe 15 July 2023.

Tume imebaini uwepo na mamlaka nyingi za ukamataji kiasi inakuwa ngumu kujua watuhumiwa waliokamatwa wapo wapi, vituo gani, nani kawakamata, ndugu wafahamu walipo jamaa zao walionyakuliwa na watu wanaodai ni wasiojulikana ..... ripoti ya mwenyekiti wa tume Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman amesema akisoma ripoti hiyo kwa rais mbele ya viongozi wa serikali na wakuu wa vyombo vya usalama walioalikwa Ikulu kusikiliza ripoti hiyo...
1740242787049.png
 
Shida inakuja unatofautisha vipi polisi na wahalifu polisi hawana uniform, wana tatoo, kama anavyosema. Utajuaje kama ni askari?
Mfano huyo angesema natekwa halafu wananchi hawamjui wakawashambulia na kuua hao polisi unajua nini kingewapata hao wananchi baadaye huyo mtu wakiambiwa alikuwa jambazi wakimkimbiza

Wao watahesabika sehemu ya huyo jambazi na kupewa kesi ya mauaji ya kuua polisi

Njia nzuri kwenye hilo ni kupiga simu polisi upesi au kuripoti kituo cha polisi cha karibu upesi au kwa mjumbe au kiongozi wa mtaa eneo hilo haraka haraka sana kwa simu au bodaboda anakimbia haraka kuripoti

Usichukue sheria mkononi hata apige kelele anatekwa

Kama huna uhakika hao wanabeba ni polisi au la na huna uhakika kama huyo mlia natekwa ni raia mwema au la tumia hizo nimekupa kama raia mwema unayeona tukio

Usitoe maamuzi haraka kuwa wake ni polisi au la na kuwa yule ni raia mwema au la

Ukachukua hatua kipofu pofu yaweza kukugharimu ikithibitika hatua uliyochukua sio kama ulivyochukua sababu ya mihemko ya kichadema maamuzi ukaozea jela au kunyongwa kwa kununua kesi isiyo yako na kuchukua hatua mbaya
 
Tatizo hili bado ni sugu, polisi na serikali hawataki kulitafutia ufumbuzi.

State sponsored terror :
Huu ni Ugaidi wa serikali ni ugaidi ambao serikali hufanya dhidi ya raia wake. Nia na madhumuni nchi iwe ya ma-kondoo waoga wasioweza kunyanyuka kupinga kila aina ya dhuluma ya ki- dola.

State coercion:
Kwa serikali kuwaburuza raia kunaweza kufafanuliwa kama hatua za makusudi zinazofanywa kwa niaba ya serikali, zinazolenga kuwalegeza na kulazimisha raia kuwa tabia fulani ya woga, na kutia unyonge katika DNA yao, yaani vinasaba wamwachie Mungu atawasaidia.

TANZANIA HAINA TOFAUTI NA NCHI ZA LATINO AMERIKA KATIKA KUENDESHA NCHI KIPOLISI
1740244977386.jpeg


1740243813802.png


MALENGO MAPANA YA KUZUA HOFU, NI CCM KUBAKI MADARAKA KWA KUENEZA HOFU KILA KONA:

Operesheni hizi za kuburuza, kujeruhi miili na bongo za raia zime kuwa copy na ku paste kutoka tawala za kidiktekta za latina Amerika, ili raia mtanzania baada ya kugongwa na vyombo vya dola akiguswa na unyasi aingie baridi akidhani ni nyoka dola ...

Operation Condor and speaks to survivors of the terror for "Americas Now."

View: https://m.youtube.com/watch?v=-_YEKdzjSDA
 
Back
Top Bottom