Bodaboda aliyedaiwa kutekwa -afunguka - "alitoa bunduki - hawafananii na polisi nikaogopa"

Mimi niliporwa simu morogoro tarehe 29-12-2021 maeneo ya magereza nikiwa kwenye bajaji nilikaa nyuma upande wa kushoto hadi leo simu haijapatikana,

Waporaji waliendelea kuwapora wengine tena nikiwashuhudia kwa macho yangu nasubiri nikiwa na pesa niwashugulikie nitatoa taarifa polisi kwamba leo Niko doria maeneo ya magereza nitarekodi matukio na drone kwaajili ya ushahidi
 
Je boda boda anamiliki bunduki ama mimi uwezo wangu wa kutafsiri maneno, (maelezo ya mwandishi) ni mdogo
 
Wewe kama siyo kibaka mmojawapo anayefanya Uhuni huo basi utakuwa ni mama mmojawapo aliyetendewa Uhuni huo,pole sana
 
Bila shaka wewe utakuwa ndio yule rasta
 
1. Msemaji wa jeshi alipewa taarifa za uongo!!!!
2. Mtuhumiwa aliyedaiwa kutekwa na polisi wamemtaja kama 'Rajab Hassan' kwamba ni mwizi mzoefu kwa kutumia pikipiki!!!
3. Mtuhumiwa baada ya kuachiliwa akihojiwa na vyombo vya habari mtandao amejitambulisha kwamba yeye anaitwa 'Marco Charlie' kwamba pikipiki aliyokuwa anaendesha ilikuwa haina namba za usajili kwa sababu ndio alikuwa ameinunua na ilikuwa haina usajili. Taratibu za usajili alikuwa amefanya akisubiria majibu ili mchakato wa kupewa namba ufanyike
4. Mtuhumiwa alidai yeye sio mwizi na hajawahi kuiba kwa yeyote
5. Wakati alipokuwa kwenye shughuli zake aliona gari kwa nyuma ikimfuatilia, kila akiongeza spidi na lenyewe linaongeza spidi, akipunguza spidi ili lipite na lenyewe linapunguza spidi pia likiwa nyuma yake. Akahisi wale hawakuwa watu wema ndipo alipochepuka njia isiyotumika na gari akaenda kwenye kituo cha waendesha bodaboda akaelezea mashaka yake. Walipoanza kufuatilia kujua hilo gari ni la nani na kwanini waliokuwemo walikuwa wanamfuatilia, ndipo wakaliona linaingia kituo cha mafuta likasimama. Waliambatana kuelekea hapo kwenda kuwauliza kwanini walikuwa wanamfuatilia na yeye akiwahoji mbona walikuwa wanaleta nzi kwa raia?
6. Kauli hiyo bila shaka iliwaghafilisha ndipo wakamkabili kumkamata kwa nguvu

Tanbihi: Ukamataji usio na staha na weledi bila kujali walikuwa wanavunja haki za binadamu, PGO na sheria za nchi.

This kind of animosity arrest should come to an end
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…