Bodaboda amuua mtoto wake kwa kumkata shingo

Bodaboda amuua mtoto wake kwa kumkata shingo

Mawazo plus hali ngumu,plus ukikosa uvumilivu na watu wa kukushauri na kukutia moyo kuhusiana na matatizo yanayokusibu basi jambo kama hilo lililotokea huwa halizuiliki
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema linamshikilia mtu mmoja aitwaye Amedius Mfoi (25) dereva bodaboda mkazi wa Muriet Jijini Arusha kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake aitwaye Amani Amedius Mfoi (03) Mkazi wa Morombo jijini Arusha.

Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishna msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Januari 23, 2024 muda wa saa 12:00 jioni mtaa wa Murieti Tarafa ya Elerai katika manisipaa ya jiji la Arusha.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo alimkata shingo mtoto huyo na kitu chenye ncha kali na kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Aidha ameeleza kuwa baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi mara moja Jeshi hilo lilianza uchunguzi na kumtafuta mthumiwa huyo kwa kushirikiana na wananchi ambapo walifanikiwa kumkamata muda mchache baadae.

ACP Masejo amesema baada ya uchunguzi Jalada litapelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.

Credit-CloudsTv
Vina kwa sababu ya Nyege wanakurupuka kuoa wakati hawako tayari bado.
 
Mwana kajiridhisha kumbe nina kazi ya kule mke anaebeba na kuzaa watoto wa wanaume wenzangu kisha ananiletea nihudumie.
Ukiangalia mtu unavyo hustle kwa jasho na damu harafu mpuuzi mmoja anakufanya wewe ni mbweha.

Dogo unakuta Hamwezi Mwanamke, sasa hasira zinaishia kwa watoto.
 
Duuuuh! inasikitisha sana,jamaa(bodaboda) kawaza sana ukute kwenye kazi ya upigaji bodaboda akitafuta riziki ya mke na wanae,kanusurika kifo maranyingi,halafu baadae anakuja anagundua kua watoto siyo wake,atakua aliumia sana,kakosa mshauri,kaua.
 
Ukiangalia mtu unavyo hustle kwa jasho na damu harafu mpuuzi mmoja anakufanya wewe ni mbweha.

Dogo unakuta Hamwezi Mwanamke, sasa hasira zinaishia kwa watoto.
Hasra mbaya sana, inatia uchungu alifanya maamuz machafu sana.
 
Mjinga mmoja
Acha kukurupuka kijana, hii habari kiini chake ni kukamatwa kwa mtuhumiwa.

Habari huwa na muendelezo, na huu ndio muendelezo wa kilichpostiwa huko nyuma. Acha kujifanya mjuzi kwenye habari zinazogusa maisha ya watu.

UWE UNASOMA NA KUELEWA.
 
Back
Top Bottom