Tafakari yetu
JF-Expert Member
- Apr 19, 2021
- 1,505
- 4,427
Wengine wanafikiri bado tupo kwenye zile zama za ulimbo na ulimbombo, zile zama za kuambiwa Jambo na kukubali bila kujiridhisha. Wanaofanya hivyo wanatambua watanzania ni wavivu sana wa kutafuta ukweli hivyo lolote analosema linabebwa kama lilivyo.
Kitendo Cha Lissu kusema China hakuna bodaboda licha ya kutengeneza mamilioni ya pikipiki akiwa katika kukazia hoja hafifu ya Lema kwamba bodaboda, kimenitafakarisha sana. Nimetafakari kwa sababu bidhaa nyingi zinazoletwa Afrika kutokea nchi nyingine China ikiwemo mara nyingi huwa ni 'second hand' hivyo Kama kuna utengenezaji wa mamilioni ya pikipiki China na zinaletwa zikiwa Used, nani atakuwa kazitumia? Bila shaka ni wenyewe:Je,kwa matumizi yapi?
Ndipo nikaingia chimbo kuchimba ukweli wa kauli ya Lissu kwamba China hakuna bodaboda na "reasoning" yangu na sasa nipo huru kwa kuujua ukweli. Biblia inasema' mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru kwelikweli'. Ukweli nilioujua ni kwamba Lissu ameamua kutudanganya kwa sababu anajua tabia ya uvivu wa kutafuta ukweli tuliyonayo na pia nimejua bodaboda (Motorcycle taxi) ni ajira kwenye nchi ya China na nchi nyingine.
Wikipedia
Ni mimi Karlo Mwilapwa
0715 804 254