KERO Bodaboda wa Tanzania wameshindikana kwa tabia zao barabarani au wameendekezwa?

KERO Bodaboda wa Tanzania wameshindikana kwa tabia zao barabarani au wameendekezwa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Sasa hivi jamaa wanaleta vitimbi vyao hadharani na hamna kitu unaweza kuwafanya.

Ni kama wana utawala wao wapo dunia yao isiyo na sheria. Wao ndio mabingwa wa kubebana mishikaki na kuchomekea wengine kwa mbele kwa kisingizio cha wana haraka.
Wameendekezwa, ni as if sheria za barabarani zina apply kwa magari tu, ila wao ahhhhh

Na haya yote wameyataka serikal
 
Nafikiri mimi ndio ntakuwa wakwaza kutoa wazo hili,
Manispaa husika ziwatumie mgambo maalum wa kusimamia boda boda,mgambo hao wawe na body camera ya kumbu kumbu yaani wakati anamkamata mtu awe ameiwasha na kurekodi kila kitu.
Malipo ya Ushuru na adhabu yaingizwe kwenye mapato ya manispaa husika.
 
Sasa hivi jamaa wanaleta vitimbi vyao hadharani na hamna kitu unaweza kuwafanya.

Ni kama wana utawala wao wapo dunia yao isiyo na sheria. Wao ndio mabingwa wa kubebana mishikaki na kuchomekea wengine kwa mbele kwa kisingizio cha wana haraka.
Abiria, tena watu wazima (na pengine ni wanandoa) wanapoamua kukubali ujinga wa ku-risk maisha yao na ya watoto wao kwa kufanya ujinga kama huu nani anawakiwa kulaumiwa?
 
Usiwaseme vibaya wapiga kura na waongoza mosafara ya kampeni...
 
Yuko mmoja aliingiwa na wadudu machoni halafu yupo speed, mbele ni semi ziko foleni, usiulize kilichotokea.
 
Kuna mdau kaleta uzi anasema huko gongolamboto boda kakanyagwa na lori na kakata moto...traffic mpaka kuja hapo kachukua dk 40 muda wote huo hakupewa huduma ya kwanza
Watu walikuwa wanamshangaa

Ova
 
Nafikiri mimi ndio ntakuwa wakwaza kutoa wazo hili,
Manispaa husika ziwatumie mgambo maalum wa kusimamia boda boda,mgambo hao wawe na body camera ya kumbu kumbu yaani wakati anamkamata mtu awe ameiwasha na kurekodi kila kitu.
Malipo ya Ushuru na adhabu yaingizwe kwenye mapato ya manispaa husika.
Hata wakifanya buku mbili kwa kosa watapata mamilioni kwa siku
 
Bodaboda wameshindikana wapo rafu sana wanapita kushoto mwa magari hawajari usalama wao wanasababisha ajari nyingi sana barabarani kwa kifupi hawa jamaa ni kero kubwa sana,unavyoendesha gari adui namba Moja barabarani ni bodaboda.
 
Bodaboda wengi hawaiheshimu kazi yao, lakini pia wanachukulia mambo ya barabarani kirahisi rahisi sana. Na wanajikuta wana haraka kuliko vyombo vyote vya usafiri hata kama anaenda kupaki tu

Unakuta boda yupo speed 70 high way au mtaani na wkt huohuo hana helmet, hajavaa viatu zaidi ya tusendo ambato katuegeshea tu kwenye miguu, hana jacket zito la kumkinga na upepo mkali, wengine wanakalia kiti kiupande ili mradi tu ajione ni mjanja... Na hawa wa hivi kuchomekea ndiyo zao

Poleni sana bodaboda wote msiojielewa, kifo na ulemavu vinawapenda sana kuliko tunavyowapenda
Na sie tunawapenda wake na mabinti zenu kuliko muwapendavyo nyie
 
Back
Top Bottom