Sean Paul
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 1,330
- 3,289
Habari za weekend wanabodi.
Moja kwa moja kwenye mada. Ni asubuhi nawahi kazini, nikiwa mmoja wa viongozi idara ya mauzo, pickup niliyopewa na ofisi inasumbua iko juu ya mawe.
Natoka nje jirani na ninapoishi kuna vijana wa bodaboda. Wanaponiona wananichangamkia na napanda mojawapo. Safari ikaanza kuelekea kazini kwangu. Wakati tunakaribia kufika, namuuliza kijana kama ana change ya elfu 10 naye anasema hana. Anatakiwa achukue elfu sita.
Nikamwambia chepuka hapo sheli tuombe change. Tulipofika pale mimi ndio nikaomba change, maana wale wadada wa pale nimezoeana nao sana kwa maana ndipo hujaza mafuta kama card za ofisi zikiwa na changamoto. Katika maongezi mawili matatu, nikafanya utani na mmojawapo wa maneno kidogo, punde tukaondoka.
Kesho yake jioni, wife to be karudi job (kuna times anakaaga kwangu hata week 2) analalamika kuna kidada cha sheli nina mahusiano nacho.
Ikabidi nitulie kwanza niscrutinize...........kumbe yule bodaboda ndiye humbeba kila asubuhi my wangu akilala kwangu kumuwahisha stand (ubaya ye anawahi sana kuamka na njia zetu ni tofauti). Kumbe dogo kamsimulia tukio langu na wale madem wa sheli........too bad akaongeza siku zote yeye (bodaboda) hujua mi mpole nisiye na stori na mtu nikipita na kuwapa hi kijiweni kwao, kumbe mchangamfu sana. Nikasolve msala ukaisha.
Ndipo bodaboda mmoja akaniambia kama una siri zako, usipande bodaboda mmoja kila siku. Kwa mfano una ratiba ya kuchepuka, umetoka home chukua boda akufikishe nusu safari, mlipe aondoke. Akishaondoka chukua nyingine ikufikishe unapoenda. Pale kijiweni wanawajadili sana huwa unapendelea kwenda wapi au sehemu walizowahi kukupeleka. Kwa week ile moja niliyopanda bodaboda mfululizo akaniambia walishatonyana wakiniona tu wanajua buku 6 hiyoo inakuja.
Bodaboda akikwambia demu fulani achana naye, msikilize. Be warned, usije sema sikukwambia.
Sean.