DOKEZO Bodaboda wengi hawajui matumizi ya taa za ‘dabo hazadi’, waelimishwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naomba bodaboda wapewe elimu ya matumizi ya Double hazard lights, asilimia kubwa wanazitumia kama fasheni lakini ndiyo chanzo kikubwa cha ajali.

Mfano amewasha hazard halafu yupo mbele na aliyepo nyuma yake hawezi kujua uelekeo wake, ghafla anakunja kushoto wakati huo hajazima hazard, kwa mazingira hay oni rahisi kutatokea ajali.
 
Hasahasa hawa wenye pikipiki toleo mpya aina ya sinorey kila dereva kawasha
 
Mateja, wavuta bangi ndio walioja huko unategemea nini?
Hawa jamaa tusiwabeze ni hali za maisha zinapelekea mpaka wanafikia huko,

Juzi ile siku ya maulid kuna boda amegongana na guta pale njia panda ya tegeta A, hii barabara ya madale, akafariki pale pale, lakini mashuhuda wanasema chanzo cha ajali ni dereva wa guta,
 
Naomba bodaboda wapewe elimu ya matumizi ya Double hazard lights, asilimia kubwa wanazitumia kama fasheni lakini ndiyo chanzo kikubwa cha ajali.

Mfano amewasha hazard halafu yupo mbele na aliyepo nyuma yake hawezi kujua uelekeo wake, ghafla anakunja kushoto wakati huo hajazima hazard, kwa mazingira hay oni rahisi kutatokea ajali.
Kwa kifupi Bodaboda ni janga kubwa ingawa tunazitumia. Yapo makosa ambayo kwa kina wanapaswa kuelekezwa ili kupunguza ajali;

1. Kutumia Double Hazard bila sababu Huwachanganya walioko nyuma kuhusu kama unataka kushoto au kulia.

2. Kugeuka bila Indicator Unabadilisha mwelekeo ghafla bila kuwaonya wengine.

3. Kupita magari kwa hatari
Kupenya kwenye nafasi ndogo kunaweza kusababisha kugongana.

4. Kukaa kwenye Blind Spot
Dereva wa gari anaweza asikuone kabisa unapopita pembeni.

5. Kukata kona ghafla
Unabadilisha njia bila kutoa nafasi kwa wengine.

6. Mwendo mkubwa kwenye foleni Gari likibadilisha mwelekeo ghafla, muda wa kujiepusha huwa mdogo.

7. Kutumia simu ukiendesha Hupunguza umakini na reaction time.

8. Kumzoesha abiria kukaa vibaya Huvuruga balance na kuongeza hatari ya kuanguka.

9. Kufuata gari kwa karibu sana Ukifunga breki ghafla, unaweza kuligonga.

10. Kuendesha pikipiki yenye hitilafu Breki, matairi au taa mbovu zinaweza kuwa chanzo cha ajali.

11. Kuendesha abiria bila kofia ya ngumu.

Haya ni baadhi ya makosa ambayo wakielekezwa ajali zinaweza pungua.
 
Hao ni ma afsa na tulishakubaliana hakuna afsa mjinga apa tz wote wana elimu
 
Naomba bodaboda wapewe elimu ya matumizi ya Double hazard lights, asilimia kubwa wanazitumia kama fasheni lakini ndiyo chanzo kikubwa cha ajali.

Mfano amewasha hazard halafu yupo mbele na aliyepo nyuma yake hawezi kujua uelekeo wake, ghafla anakunja kushoto wakati huo hajazima hazard, kwa mazingira hay oni rahisi kutatokea ajali.
Sahii sana, nakubaliana na wewe , hawa ndo maana yanavunjika viuno .

Sheria ya kusoma kama ilivyo kwa madereva ya magari iwe kwa bodaboda nchi nzima , wapate leseni baada ya kuhitimu.

Bodaboda imezalisha vichaa wengi ila wapo ambao wapo smart na wanajua wako barabarani.

Jiulize why dereva bajaji wengi hawapati ajali ,jibu wengi dereva bajaji walikua madereva teksi zamani.

Pili madereva wengi ambao hawakua dereva Taksi hupiga diwaka kwenye bajaji mpaka wanakua smart kabla ya kuanza udereva .

Njoo kwa boda siku mbili ya mafunzo naye barabarani anajiona ni dereva mkuu.

Hayana utulivu ,hayajali kwao afike kijiweni hata kama anaenda kupaki .

Serikali ifanye mkakati mpya yakasome then ndo yaendelee na mibodaboda yao.

Pamoja na mapungu tajwa hapo juu ni makorofi bila kujali boda amegongwa kwa makosa yake ila utajaziwa inzi balaaa , yana umoja hata kwenye makosa .
 
Usisahau kuvaa Pedi ukiwa kwenye mkusanyiko
 
ni hatari sana unakutana na dabo hazad halafu za rangi tofauti na taa ya mbele iko full kumulika utazani ni mchana..
 
Naomba bodaboda wapewe elimu ya matumizi ya Double hazard lights, asilimia kubwa wanazitumia kama fasheni lakini ndiyo chanzo kikubwa cha ajali.

Mfano amewasha hazard halafu yupo mbele na aliyepo nyuma yake hawezi kujua uelekeo wake, ghafla anakunja kushoto wakati huo hajazima hazard, kwa mazingira hay oni rahisi kutatokea ajali.
Hao ni vilaza PASEE ,siyo hizo hawajui sheria nyingi sana za barabarani.

Utakuta lipo kwenye barabara ambayo ina njia mbili za kwenda linakaa KULIA badala ya kushoto.

Wapewe elimu hao BODABODA ni Maamuma wa sheria za barabarani.
 
Akili za bodaboda, waendesha maLandcruiser ya serika, na wale wa mabasi akili zao ni moja. Bangi wanayotumia ni moja na mganga/mchawi wao ni mmoja.
Ni watu wenye haraka kuliko watumiaji wengine wa barabara.

Bodaboda yeye indicator ni urembo. kuvuta speed hadi 80km/h hali unaenda kusimama mita 100 tu baada ya rough overtaking ni ufahari na ndio kujua kuendesha pikipiki.
 
Back
Top Bottom