DOKEZO Bodaboda wengi hawajui matumizi ya taa za ‘dabo hazadi’, waelimishwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sio visungura wanakula bangi sana inayofanya wajiamini sana kwa mambo ya hovyo.

Akila kisungura hata mbele hawezi ona.
Yani boda anakupita kama upepo alafu mita mia nyingi unamkuta kapaki ,unajiuliza alikua anakimbizana na nini? Jibu hupati, ile sio akili ya kawaida ,upo sahii
 
Moja ya sheria za usalama barabarani zinasema membea kama unaona usalama upo mbele maana wewe unaendesha pia alie nyuma yako , ila haya ni twende tu .
 
Hawajui sheria za barabarani karibia zote
 
Wangekuwa wamepitia vyuo vya udereva kusoma na kufaulu mitihani kungekuwq hakuna haja ya kuwaelimisha kitu kama hivyo
Wengi hawajui vingi
Uchumi
Afya
Mazingira nk.. Ambavyo vyote hivyo wanapaswa kufundishwa na kuvifanyia mitihani kabla ya kuingia barabarani
 
Ukienda China wadada wengi wanafanya boda za vibajaji vya kucharge kwa umeme , wako smart anzia mwonekanao wao , uvaaji kwa wanaijali kazi yao , njoo hawa wa kibongo si wote ila wengi ,hawajui kama ni kazi ,koti la kuzuia upepo unakuta lipo mwezi mzima halijui maji au sabuni ,uchafu uchafu tu
 
Mkuu boda wengi ni mazoe tu , siku tatu kafundishwa huko vichakani ati yupo barabarani ,so wengi wanaendelea kuutafuta uzoefu barabarani na kwa kubatisha tu . That's wamevunjika viono wengi sana kama sio kupata vilema vya kudumu au kupoteza maisha kabisa , ni wachache sana bodaboda utawauliza angalau alama 10 za barabarani kupitia michoro wakatoboa hata nusu .

Waende shule waundiwe sheria mpya ,kama madereva wa magari wanatakiwa kufanya hivyo why wao ,tunaheshimu kwamba ni sehemu ya ajira ila sitamani ajira nyenye madhara makubwa kiasi ichi
 
Utambunzi wa boda boda kupitia lesen ambapo bila shaka inaendana na kumbukumbu muhimu za mhusika baada ya mafunzo zifanyike , huko pia kuna vibaka wakijificha kwenye kivuli cha bodaboda ifanyiwe kazi , mwaka mmoja nimemnusuru afisa Mkubwa ,kosa kafanya boda ila kazingirwa wakitaka choma gari yake , sijui kama yupo maana nikitoka mishe zangu nilimtambua ila hatufamiani ,alikuepo kiaele mmoja nilimvuta pembeni nikamtia 50 na kumwambia awatulize wenzake ila uyo afisa hakujua nini kilifanyika kabla , na wala sikutaka jitambulisha .
 
Waende shule waundiwe sheria mpya ,kama madereva wa magari wanatakiwa kufanya hivyo why wao ,tunaheshimu kwamba ni sehemu ya ajira ila sitamani ajira nyenye madhara makubwa kiasi ichi💪🏿✔🙏🏿
 
Mtoa mada sidhani kama hata anaelewa ukisema double Hazard na single hazard inakuwaje n Na taa ya kukunja kona inaitwaje ?
 
Yani boda anakupita kama upepo alafu mita mia nyingi unamkuta kapaki ,unajiuliza alikua anakimbizana na nini? Jibu hupati, ile sio akili ya kawaida ,upo sahii
Wengi ganja na mkumbo tu, visungura wanakula mateja
 
Nazingatia sana vivuko na kuwaangalia wanafunzi wavuke kwa usalama asubuhi hiyo ikifika mchana au jioni ni mwendo wa kuwakwepa boda boda mwanzo mwisho maana unakuta mwingine anakupita kushoto harafu kwa kasi sana huku akikuangalia wengine mikoa ya Kaskazini wana mikao yao kuona kama bara bara wameitalawa..
Ukisahau uwepo wa boda boda utawalamba sana maana ni kama vyombo vinaendeshwa na remote vile..
 
Uko sahihi💯
 
Kofia ngumu kwa boda boda ni msamiati mgumu sana.
 
Bodaboda yeye indicator ni urembo. kuvuta speed hadi 80km/h hali unaenda kusimama mita 100 tu baada ya rough overtaking ni ufahari na ndio kujua kuendesha pikipiki.
Wana mbwembwe sana hawa vijana wangu 😂😂😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…