Bodaboda zimekuwa nyingi, vifo vinavyotokana na ajali vimekuwa ni vingi mno

Bodaboda zimekuwa nyingi, vifo vinavyotokana na ajali vimekuwa ni vingi mno

Hii biashara imekuwa na vijana wengi kila baada ya nyumba tano utakutana kijiweni Cha boda kazi hii imekuwa ni ya mateso sana vijana wanafanya kazi masaa mengi kupata riziki pia ni hatari sana kwa afya zao vifo vinavyotokana na ajali za boda boda vimekuwa ni vingi mno.

Nashauri Serikali kuongeza Kodi kwenye hizi boda boda moja imfikie mnunuzi kwa millioni 5, hii itasaidia kupunguza ajali zinazojitokeza.
Duh.! Kuongeza kodi?
 
niko najichanga nifungue spare za pikipiki, Hii ni fursa nzuri sana
Sure mkuu halafu kwa pembeni ya ofisi unaweka kigereji fulani cha kizushi. Ningekua na ujuzi wa spare za pikipiki ningelitathmini hili suala kwa ukaribu zaidi
 
vip kuhusu tuvibanda twa m-pesa,na Airtel money....
 
Point yangu ya msingi kwanini kundi kubwa la watu wanakuwa kwenye shughuli moja ambayo inakuwa inaleta maafa mengi Mimi kwa mawazo yangu naona nguvu kazi inakuwa inapungua kuona kundi kubwa la watu kufanya shughuli moja yenye kipato duni
Ndio utoe option nyingine za hao vijana kwenda ila sio kuongeza kodi. Ongezeko la kodi linabebwa na mtumiaji wa mwisho. Ukimuongezea kodi mfanyabiashara atakachofanya yeye ni kuongeza bei ya bidhaa/huduma.
 
Unaomba serikali iongeze Kodi wakati juuzi kila mkoa zimeongezwa boda boda 700 kila mkoa kutoka mfuko wa SSH2025 so pambania family yako achana na biashara za watu
Mimi naombea sana sana kasi ya kununua bodaboda iendelee na izidi. Pia wabunge na viongozi wote akiwemo rais wazidi kugawa za bure. Hii ni kwa sababu baada ya muda tutakuwa na jeshi kubwa na lenye nguvu sana la kuwaondoa hawa mafisadi.
 
Kabisa mbona hajaona maframe

Ova
Sasa mkuu unataka mtu aelezee kero zote kwenye uzi mmoja si atalazimika kuandika kitabu kizima. Yeye kaiona kero ya bodaboda kaisemea wewe unaona kero ya utitili wa fremu pia unaweza kuifungulia uzi ukatililika.
 
Tatizo tushachukulia bodaboda kama back up ya ukosefu wa ajira au kushindwa kujiajiri kwenye biashara za maana ila kiuhalisia boda boda sio ajira kama alivosema Lema, vijana wanaondoka sana na kupata vilema na hizi pikipiki
 
Tupe mfano wa biaahara za maana ambazo badala ya kuchujua pikipiki ya mkataba kijana anaweza kuifanya bila ya kuwa na mtaji wa pesa
 
Sure mkuu halafu kwa pembeni ya ofisi unaweka kigereji fulani cha kizushi. Ningekua na ujuzi wa spare za pikipiki ningelitathmini hili suala kwa ukaribu zaidi
spare za pikipiki nazifahamu vzuri sana. Mkuu ukifungua spare lazima sehemu iwe na nafasi sbabu lazima kuwepo na huduma za ufundi.lakini spare zinahitaji muda kuzifahamu.
ILA unaweza hata kuanza na urembo kama sticker, reflector na vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji sana muda mrefu kuvifahamu
Wewe una uzoefu wa biashara gani?
 
Tupe mfano wa biaahara za maana ambazo badala ya kuchujua pikipiki ya mkataba kijana anaweza kuifanya bila ya kuwa na mtaji wa pesa
Hakuna biashara ya kuanza bila kuwa na mtaji wa pesa, hata kuchukua mkataba wa hiyo boda huo mkataba ni kama pesa tu.

Nenda kariakoo maduka ya jumla kachukue mzigo utembeze mule nayo pia ni bila kuwa na mtaji wa pesa kama ulivosema.
 
CCM tumeingiza boda 18,200, bado kuna mzigo unakuja wa kugawa kama mitungo ya gesi inavyogawiwa.
Kama nchi tumepotea. Badala ya kuwapa vijana pembejeo au wekeza kwenye academy unawapa bodaboda kweli. Kuna sehemu hatupo sawa
 
Zambia hakuna bodaboda wala bajaji za abiria kama Tanzania! Na maisha yanaendelea vizuri tu.
Yani ccm wameshindwa kuwavuta vijana kwenye kilimo!??

Hawana maarifa hawa jamaa.

Kila siku kwenye uchaguzi wanasema wanatuletea maji watajenga hospitali kwani nani anatawala?
 
Sasa mkuu unataka mtu aelezee kero zote kwenye uzi mmoja si atalazimika kuandika kitabu kizima. Yeye kaiona kero ya bodaboda kaisemea wewe unaona kero ya utitili wa fremu pia unaweza kuifungulia uzi ukatililika.
😄 sawa sawa mkuu
Uzi wa maframe unakuja

Ova
 
Yani ccm wameshindwa kuwavuta vijana kwenye kilimo!??

Hawana maarifa hawa jamaa.

Kila siku kwenye uchaguzi wanasema wanatuletea maji watajenga hospitali kwani nani anatawala?
Kuendesha boda au kufanya biashara ya boda ni sawa na kufanya biashara ya magendo
😄 maana muda wote mnakimbizana na polisi wale tigo
Voda faster
Ukija sasa kwenye usalama wa uhai ndiyo hivyo tena kifo nje nje

Upo sahihi kabisa lkn maajabu unakuta raisi ananunua bodoboda?

Ananunulia vijana bodaboda.....

Kweli Bongo bahati mbaya
 
Back
Top Bottom