Tetesi: Bodi Simba yaridhia kuachana na Robertinho

Tetesi: Bodi Simba yaridhia kuachana na Robertinho

Mnasubiri nini kumuondoa kocha? Miezi 9 yupo na timu bado hajapata muunganiko tu?
Hamuoni timu inashinda kwa uwezo binafsi wa wachezaji tu?

Au mpaka aitie hasara klabu ndio mumuondoe?

Kuweni na huruma na mioyo ya washabiki wenu!

Bado kurushiwa makopo tu!
Katupatia ngao ya jamii dhidi ya Yanga, ligi kuu tunaendelea kushinda na hatujafungwa , mashindano ya Caf tayari katuvusha kuingia makundi haijalishi ni kwa mbinde au nini.
Je ' afukuzwe kwa ubaya upi???
 
Hatuchezi kama yanga
 
Wabongo bana, mtu unashinda kuanzia ngao ya hisani, mechi zote NBC na unafuzu makundi lakini bado Wanataka kukutupia virago, mnataka afanyaje? Mbona Mourinho kwenye mafanikio hakua na pira biriyani?
Hakuna kocha hapo.
 
View attachment 2769201

Habari zilizotufikia ni kuwa bodi ya klabu ya Simba imeridhia kuacha na kocha wake Mbrazil Roberto Oliveira 'Robertinho' kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa timu tangu msimu huu kuanza licha ya kupewa asilimia kubwa ya wachezaji aliowahitaji.

Simba itatangaza uamuzi huo baada ya mechi dhidi ya Tanzania Prisons katika mwendelezo wa ligi kuu NBC Tanzania [emoji1241]

Juma Mgunda ataichukua timu kwa muda huku klabu ikiendelea kutafuta kocha wa kuja kuifundisha klabu hiyo na kumpa malengo yao.
Huyu si kocha kbs amekuwa mlopokaji tu anapoongea hata mate hamezi English wenyewe mbaya
 
Wabongo bana, mtu unashinda kuanzia ngao ya hisani, mechi zote NBC na unafuzu makundi lakini bado Wanataka kukutupia virago, mnataka afanyaje? Mbona Mourinho kwenye mafanikio hakua na pira biriyani?
Nabi alifukuzwa El Merrreikh kwa Kutoa sare na simba mechi Moja tu akiwa kocha mkuu hata Yanga walimfukuza kocha aliyempokea Kaze akiwa ameshinda mechi tatu kwa asilimia 100 Ila wenye timu hawakuridhika kbs na performance ya timu pamoja na kushinda

Mie siafiki kumfikisha hadi huko kwa prison kwani simba itakuwa imefungwa kbs siku hiyo
 
Wabongo bana, mtu unashinda kuanzia ngao ya hisani, mechi zote NBC na unafuzu makundi lakini bado Wanataka kukutupia virago, mnataka afanyaje? Mbona Mourinho kwenye mafanikio hakua na pira biriyani?

Tatizo ni kuji compare na Yanga, kipimo chao ni yanga, hawajui Yanga ni Baba lao.
 
Ila Kama taarifa hizi ni za kweli hatutaki kumsikia huyu kocha anatupa vijisababu kuwa alikuwa anapangiwa wachezaji na viongozi.
Ila nafikiri sio sahihi kuachana naye Sasa maana tuna mchezo ngumu wa Africa super league.
Akibakia hadi siku hiyo itakuwa ni kutwanga maji tu atatuliza Asepe hadi leo
 
Katupatia ngao ya jamii dhidi ya Yanga, ligi kuu tunaendelea kushinda na hatujafungwa , mashindano ya Caf tayari katuvusha kuingia makundi haijalishi ni kwa mbinde au nini.
Je ' afukuzwe kwa ubaya upi???
Hapo kwenye 'mbinde' panafaa kumuondoa. Kwasababu hata wewe umekili ni mbinde!

Gao ya jamii, ligi Kuu sio hoja kwasasa, Kwasababu malengo yetu ni nusu fainali za klabu bingwa. Kwa hiyo 'mbinde' unadhani tutatoboa kweli?
 
Kama wameshaanza kuangaika hivi hiyo timu haiwezi kufika mahali.Viongozi wa simba wana mihemko sana,wanakosa utulivu wa muda mrefu kwenye kuiandaa timu ifike nafanikio makubwa.wanawaza mafanikio ya haraka haraka wakati bado ni timu mbovu.Mimi bado naamini simba ilikosea sana kuachana na Patrick Aussems(uchebe),kwasababu yule mzee ndiye angalau alianza kuipa timu makali na falsafa inayoeleweka.Wangekua wavumilivu kwa makocha wangepata wanachokitaka ila ilo somo inaonekana ni gumu kwao.
 
Aondoke, hana mbinu zozote. Kila mchezaji anacheza anavyojua. Tunamshukuru kwa kumpiga utopolo na kila la kheri huko aendako
Hicho ndio kikosi alichokua nacho unadhani nirahis kubadilisha wachezaji haraka hivyo..Kutengeneza timu kunahitaji muda wakutosha.nyie mnataka mwalimu aje siku hiyo hiyo timu ifike fainali.kwa mawazo hayo ata Pep gadiola hawezi.Mnataka timu icheze vizuri alafu hamjifunzi kwa yanga waliotengeneza falsafa ya timu kwa muda ambayo mwalimu yoyote anayekuja anaendelea nayo.Simba wamebadilisha badilisha walimu ndani ya muda mfupi hadi wamepoteza ile ladha ya pira biriani.
 
Mnasubiri nini kumuondoa kocha? Miezi 9 yupo na timu bado hajapata muunganiko tu?
Hamuoni timu inashinda kwa uwezo binafsi wa wachezaji tu?

Au mpaka aitie hasara klabu ndio mumuondoe?

Kuweni na huruma na mioyo ya washabiki wenu!

Bado kurushiwa makopo tu!
Profesa alikaa na yanga muda gani hadi timu ikaanza kufanya vizuri?.Matunda wanayoyapata leo yanga nikwasababu walimvumilia Nabi.Tofauti na hapo huo mpira mzuri unaochezwa na yanga sasa usingekuwepo.Tuwe wakweli.Uvumilivu unalipa kuliko papara.
 
sio muumini wa kubadilibadili makocha ila kwa kocha huyu ni wa kubadili, chini yake ameuwa uwezo wa wachezaji kama saidoo,si yule wa mgunda kabisa, chama kawa tepetepe mnoo, moses phiri ndo hataki kumsikia kabisa, baleke si yule tumjuaye na sasa kahamia kwa kanoute Putin kuhakikisha anapotea
Mchezaji anapewa nafasi ya kucheza alafu anacheza chini ya kiwango hapo kocha anakua na tatizo gani?.Hao wote uliowataja wanachezeshwa ni jukumu lao kuipigania timu kwakuonyasha juhudi binafsi ili timu ifanye vizuri.Kazi ya mwalimu ni kuelekeza tu ila mengine ni juhudi za mchezaji mwenyewe.
 
Back
Top Bottom