Naiomba Bodi ya Ithibati Nchini Tanzania (JAB) kufanya uchunguzi katika Taasisi za Waandishi wa Habari Nchini na sio tu kwenye Vyombo vya Habari (Media Houses) kwani Kuna waandishi wengi kwenye Clubs hawana sifa za uandishi wa Habari ambapo wanafanya shughuli hizo kinyume na Sheria ya habari ya Mwaka 2016.
Katika Sheria hiyo Kifungu cha 19: Kinakataza mtu yeyote kujihusisha na kazi au shughuli za kihabari (kama vile uhariri, kuripoti habari, utangazaji, na uandaaji wa vipindi) bila kuwa na ithibati halali kutoka kwa Bodi. Kufanya hivyo ni kuvunja masharti ya sheria hii.
Pia, Kifungu cha 50(2)(b): Kinamaanisha kuwa kufanya kazi za Uandishi wa Habari bila kuwa na ithibati ni kosa la kisheria linaloadhibiwa kwa mujibu wa sheria
Hivyo basi, wito wangu kwa Bodi ya Ithibati ichukulie hatua clubs ambazo zinawaandishi makanjanja wasiokuwa na sifa hizo ,ili kuipa heshima ya Taaluma ya habari Nchini , kwani watu wengi wamejipenyeza kwa kutumia kimvuli cha Clubs kufanya Shughuli hizo kinyume cha Sheria.
Lakini pia wanashiriki shughuli za kiserikali na shughuli za kihabari bila kuwa na Press card kutoka Bodi ya Ithibati Tanzania, hivyo Mimi kama mwanahabari mzalendo katika Taifa Langu nimeona nitoe rai yangu kwa Bodi ya Ithibati ili isipite tu kwenye media house bali ipite kwenye press Clubs kote nchini ili kuwaondoa waandishi wasiokuwa na sifa, na itabaini wengi zaidi hawana sifa hizo ,lengo ni kuweka heshima na kutoonesha upendeleo wa utekelezaji wa Sheria ya huduma ya vyombo vya habari Nchini.
kitendo hicho kinaumiza Taaluma ya habari kwani wengi hawana sifa lakini Bado wanaendelea kufanya Shughuli hizo ili hali wengine wamehangaika kurudi shule ili wakidhi vigezo vya Sheria hiyo , huku wengine wakifanya bila kuwa na sifa zilizoanishwa kwenye Sheria ya huduma za vyombo vya habari Nchini ya mwaka 2016.
Kama Bodi imeamua kuwaondoa waandishi wasiokuwa na sifa basi usifanye upendeleo maana tumeona wameondoa waandishi wasiokuwa na sifa kwenye vyombo vya habari hapa Nchini , hivyo wafanye msako mkali kwenye hizi Taasisi za waandishi wa habari mikoani ili kuwaondoa waandishi wasiokuwa na sifa.