Bodi ya Ligi yapigilia msumali suala la derby, yasema ipo na lazima ipigwe Juni 15, 2025

Bodi ya Ligi yapigilia msumali suala la derby, yasema ipo na lazima ipigwe Juni 15, 2025

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
450
Reaction score
3,368
Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya ligi kuu nchini Tanzania Almas Kasongo amesema kuwa kikao cha leo kilikuwa ni kikao cha kupokea matakwa ya Yanga Sc ambao wamekuja na matakwa manne ikiwa ni kujiuzuru kwa Mwenyeketi wa bodi ya ligi, kujihuzuru kwa Afisa Mtendaji mkuu wa TPBL, Katibu mkuu wa TFF na kuona bodi ya ligi kuu inakuwa chombo huru.

Hivyo basi matakwa hayo yamepokewa na yatawasilishwa kwa shirikisho la soka nchini "TFF" ila kwa mamlaka ya bodi ya ligi mpaka sasa ni Mchezo upo pale pale juni 15.


==========================

TAARIFA KWA UMMA #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko.jpg

Wakati huohuo Klabu ya Yanga nayo imetoa taarifa kuwa msimamo wao upo palepale kuwa hawataingiza timu uwanjani.

TAMKO LA YANGA
Uongozi wa Young Africans Sports Club, unapenda kuutarifu umma kuwa, tarehe 7 Juni, 2025 tulipokea barua kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa ajili ya kuhudhuria kikao maalum cha kujadili masuala yahusuyo mchezo namba 184 wa Ligi Kuu ya NBC, YANGA dhidi ya Simba.

Uongozi wa Klabu yetu ulitii wito huo na kushiriki kwenye kikao kilichofanyika leo, Jumatatu Juni 9, 2025 kwenye ofisi za Bodi ya Ligi Tanzania zilizopo jengo la NSSF Mafao House, Dar Es Salaam, kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Baada ya majadiliano ya saa kadhaa, Viongozi wa Klabu waliwasilisha msimamo wa Klabu yetu kuwa hatutashiriki mchezo namba 184 uliopangwa kufanyika tarehe 15 Juni 2025 mpaka pale matakwa yetu tuliyoyawasilisha kwa maandishi kwao yatakapotimizwa.

Tunawatakia kila la heri Bodi ya Ligi na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini katika kushughulikia matakwa yetu yenye mustakabali mkubwa kwenye maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania.

Imetolewa na
Kamati ya Utendaji
Young Africans Sports Club
 
Almasi Kasongo ame maanisha aliyewapa amri ya kupanga tarehe ambaye ni boss wao Tff amewatuma tena waje wakae na Yanga na kuwasikiliza official kwakua Yanga haikuandika barua juu ya madai yao.

Maana yake Bodi ya ligi hawana meno ya kusema lolote kwasasa ila malalamiko wameyapokea kupitia kikao na wamerudisha kwa boss wao aliye waambia wapange tarehe.

Maana yake boss wao ndie atakaye toa tamko kwasasa ratiba ipo vilevile.
Kwa wale wenye D 2 wanajua hakuna mechi na siku sinnyingi bodi Watakuja na tamko kutoka kwa boss wao aliye watuma.
Kwa Leo ilikua ni kupokea maoni ya Yanga kwakua Yanga haikuwahi kuwaandikia official.
 
Hawa jamaa wajinga sana, kama wao derby ipo waliwaita Yanga kufanya nini?

Na maelezo yake ni kwamba wameyapokea matakwa ya Yanga sasa inakuaje tena unatangaza derby ipo wakati una task umepewa?
derby ipo pale pale mpaka itakapo tangazwa vingine

yuko sahihi,

kama tamko la mkubwa litakuwa ibadirishwe ndio itakuwa derby haipo
 
Hawa jamaa wajinga sana, kama wao derby ipo waliwaita Yanga kufanya nini?

Na maelezo yake ni kwamba wameyapokea matakwa ya Yanga sasa inakuaje tena unatangaza derby ipo wakati una task umepewa?
Maana yake hawana meno, Amri zote zinategemea boss wao Tff, kwaiyo ni kama Remote tu.
Sasa wanarudi kumsikiliza Wallec Karia alafu watarudi tena.
Lakini wanajua tarehe 15 mechi hakuna.
 
Yanga asipoleta timu ajiandae kucheza na Yombo fc daraja la 6 huko na anatema pointi 3 na kubwa kuliko yote mnyama anatangazwa bingwa.

Yaani safari hii Yanga wanaumia kila sehemu maana bodi haiwezi kuamrishwa cha kufanya na Yanga.
 
Yanga asipoleta timu ajiandae kucheza na Yombo fc daraja la 6 huko na anatema pointi 3 na kubwa kuliko yote mnyama anatangazwa bingwa.

Yaani safari hii Yanga wanaumia kila sehemu maana bodi haiwezi kuamrishwa cha kufanya na Yanga.
Ndo hasara ya kutumia busara katika maaumuzi wakati sheria na kanuni zipo. Bodi itaamurishwa tu na yanga. Bodi wametelekeza nguvu zao kwa simba na yanga.
Simba anasema sipeleki timu uwanjani bodi wanaitikia tu kama dume lillilofumaniwa na mke wa mtu, wakati kanuni zipo. Halafu wanataka yanga watii maagizo yao.
Bodi Hawawezi kuendesha ligi kama vikao vya familia.
 
Back
Top Bottom