Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (HESLB) kumtumia control namba mtu asiye na ajira ni kumuongezea stress, badilikeni!

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi Elimu ya Juu (HESLB) kumtumia control namba mtu asiye na ajira ni kumuongezea stress, badilikeni!

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, shalom!!!

Ninapata malalamiko mengi Kwa vijana wangu wengi Walio mtaani wanaopambana kujitafuta Ili wapate chochote kitu Cha kujikimu mahitaji Yao na ya wanaowategemea.

HESLB, bodi ya mikopo, unapomkopesha mwanafunzi wa chuo, lazima unakuwa na taarifa zake, namba ya simu IPO, namba ya nida , nk nk.

Na Kwa kawaida, mtu huyo akipata KAZI serikalini au sekta binafsi, taarifa zake zikipelekwa NSSF, PSPF,nk lazima mtajua kuwa mtu huyo tayari ameingia mfumo wa kupata pesa, hapo ni sawa kumpigia simu au kuwasiliana na waajiri wake Ili kupata namna Bora ya Kupata mkopo mliomkopesha. Akikuza biashara na kupata VAT Registration Number ( VRN) mfumo wenu utajua sababu NIDA yake ilitumika, mnawasiliana nae alipwe Polepole.

Sasa, kumtumia controll namba kwamba mnamdai M. 16, yaani 16,000,000/= kijana aliyemaliza chuo, hajapata KAZI, Hana hata mia, aliyebomolewa Banda lake la biashara na mgambo wa Jiji,wengine wanarandaranda wakifanya vibarua mtaani, ghafula inaingia message yenye ujumbe ulioambatana na bill ya control namba yenye kuonyesha deni analodaiwa na bodi ya mikopo HESLB, hamuoni kuwa Hali hiyo ni kumuongezea stress?

USHAURI.
1. Bodi ya mikopo, HESLB, kupata pesa yenu kirahisi, wasiliana na Waziri Mwigulu Nchemba na waziri wa Ajira Ili mshauriane, ipatikane namna Bora ya kuwaajiri Hawa vijana Kwa namna mbalimbali Ili pesa ya umma iweze kurudi Kwa wakati.

2. Hakikisheni mifumo inasomana, kama kijana hajaajiriwa mnatakiwa kujua Ili kuepuka usumbufu na stress mnazowasababishia Hawa vijana.

3. TRA, Wizara ya Fedha, viwanda na biashara, Ajira, shirikianeni Ili kusaidia vijana Hawa wafungue kampuni, walelewe na kupata msamaha wa Kodi Ili wakuze biashara zao, waongeze tax base na walipe mikopo wanayodaiwa na bodi ya mikopo HESLB na waweze pia kulipa Kodi Ili kukuza Uchumi wa Nchi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏. Cc: mwigulu nchemba

PIA SOMA
- Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) yaja na 'Kampeni ya Fichua' kuwasaka wadaiwa sugu
 
Wazo bora la siku , hongera mtoa mada
Dogo amepigiwa simu na afisa wa Bodi ya mikopo akimkaripia kwamba kwanini hajalipa mkopo na ametumiwa control namba, mwezi uliopita,

Dogo ananiambia hapa Leo sijapata pesa, nauli yenyewe kurudi home mtihani, halafu tena unapigiwa simu ukikumbushwa deni kana kwamba umepata ajira una pesa, hutaki kulipa!!

Imebidi nimtie tu moyo.

Hii Si sawa!!
 
Dogo amepigiwa simu na afisa wa Bodi ya mikopo akimkaripia kwamba kwanini hajalipa mkopo na ametumiwa control namba, mwezi uliopita...
Sio sawa kabisa hata kama ni mdeni wao , mtu unakuta ananstress za maisha , ajira hakuna , wazazi na ndugu waliomsaidiabkumsomesha wanamtegemea yeye then bado bodi nao wakusumbue.
Tsh 16M, si mtu anaweza kufa kwa mawazo
 
Salaam, shalom!!!

Ninapata malalamiko mengi Kwa vijana wangu wengi Walio mtaani wanaopambana kujitafuta Ili wapate chochote kitu Cha kujikimu mahitaji Yao na ya wanaowategemea.

HESLB, bodi ya mikopo, unapomkopesha mwanafunzi wa chuo, lazima unakuwa na taarifa zake, namba ya simu IPO, namba ya nida , nk nk.

Na Kwa kawaida, mtu huyo akipata KAZI serikalini au sekta binafsi, taarifa zake zikipelekwa NSSF, PSPF,nk lazima mtajua kuwa mtu huyo tayari ameingia mfumo wa kupata pesa, hapo ni sawa kumpigia simu au kuwasiliana na waajiri wake Ili kupata namna Bora ya Kupata mkopo mliomkopesha.

Sasa, kumtumia controll namba kwamba mnamdai M. 16, yaani 16,000,000/= kijana aliyemaliza chuo, hajapata KAZI, Hana hata mia, aliyebomolewa Banda lake la biashara na mgambo wa Jiji,wengine wanarandaranda wakifanya vibarua mtaani, ghafula inaingia message yenye ujumbe ulioambatana na bill ya control namba yenye kuonyesha deni analodaiwa na bodi ya mikopo HESLB, hamuoni kuwa Hali hiyo ni kumuongezea stress?

USHAURI.

1. Bodi ya mikopo, HESLB, kupata pesa yenu kirahisi, wasiliana na Waziri Mwigulu Nchemba na waziri wa Ajira Ili mshauriane, ipatikane namna Bora ya kuwaajiri Hawa vijana Kwa namna mbalimbali Ili pesa ya umma iweze kurudi Kwa wakati.

2. Hakikisheni mifumo inasomana, kama kijana hajaajiriwa mnatakiwa kujua Ili kuepuka usumbufu na stress mnazowasababishia Hawa vijana.

3. TRA, Wizara ya Fedha, viwanda na biashara, Ajira, shirikianeni Ili kusaidia vijana Hawa wafungue kampuni, walelewe na kupata msamaha wa Kodi Ili wakuze biashara zao, waongeze tax base na walipe mikopo wanayodaiwa na bodi ya mikopo HESLB na waweze pia kulipa Kodi Ili kukuza Uchumi wa Nchi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni 🙏. Cc: mwigulu nchemba
HESLB tumeni control namba , vijana wengi wanakaa baa kila siku kunywa huku wakitukana serikali hawana ajira hizo za kunywa wanakopa?
 
HESLB tumeni control namba , vijana wengi wanakaa baa kila siku kunywa huku wakitukana serikali hawana ajira hizo za kunywa wanakopa?
Ukiwapa KAZI lini Ili upate uhalali wa kuwadai?

Hapo ukute una miaka zaidi ya 60 lakini Bado ni mtumishi wa Serikali.

Ruto ameshavunja Baraza la mawaziri Kwa shinikizo la Hawa Hawa mnaowadharau.
 
Ukiwapa KAZI lini Ili upate uhalali wa kuwadai?

Hapo ukute una miaka zaidi ya 60 lakini Bado ni mtumishi wa Serikali.

Ruto ameshavunja Baraza la mawaziri Kwa shinikizo la Hawa Hawa mnaowadharau.
1. Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kuna pahala inasema itawatafutia ajira mkimaliza Chuo?

2. Gen -Z wa Tanganyika mnazidiwa hata na watoto wa Somali ku-reason, watu waliozaliwa kwenye utapiamlo!

3. Kwamba ukikopa BENKI , hiyo benki ina wajibu wa kukutafutia biashara ili uweze kulipa deni lao?

4. Acheni upuuzi kwenye hii nchi!
 
Takwimu zinasema,

Kila mwaka vyuoni wanahitimu wanafunzi zaidi ya 1,000,000. Yaani 1 M.

Sasa Kwakuwa tatizo hili ni la kimfumo, tupate suluhu ya kimfumo kuliko kumsaidia mtu mmoja pekee!!
Sio kwamba nimekuuliza labda nitamsaidia, mimi nimemaliza miaka mingi sijawahi lipa ila sijapokea sms labda huenda toka miaka hiyo nishabadili namba mara nyingi tu.
 
Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kuna pahala inasema itawatafutia ajira?

Gen -Z wa Tanganyika mnazidiwa hata na watoto wa Somali ku-reason, watuy waliozaliwa kwenye utapiamlo!

Kwamba ukikopa BENKI , hiyo benki ina wajibu wa kukutafutia biashara ili uweze kulipa deni lao?

Acheni upuuzi kwenye hii nchi!
Sawa,

Nitawambia waache upuuzi🙏
 
1. Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu kuna pahala inasema itawatafutia ajira mkimaliza Chuo?

2. Gen -Z wa Tanganyika mnazidiwa hata na watoto wa Somali ku-reason, watuy waliozaliwa kwenye utapiamlo!

3. Kwamba ukikopa BENKI , hiyo benki ina wajibu wa kukutafutia biashara ili uweze kulipa deni lao?

4. Acheni upuuzi kwenye hii nchi!
Umenena vyema kabisa.
 
Sawa,

Nitawambia waache upuuzi🙏
Tunakuwa wapuuzi sana, kila kitu tunalaumu serikali.
Unatoka kwenu Namanyere unakuja Kariakoo unapanga biashara katikati ya barabara ukiondolewa unaihoji serikali uende wapi, hivi na hawa matajiri nao wakapaki magari mlangoni kwako wanafanya service utaendaje kuharisha wali wako wa maharagwe yaliyochacha?
 
Sio kwamba nimekuuliza labda nitamsaidia, mimi nimemaliza miaka mingi sijawahi lipa ila sijapokea sms labda huenda toka miaka hiyo nishabadili namba mara nyingi tu.
Kwamba unashauri abadili namba Ili asisumbuliwe?

Muhimu hapa tushauri Serikali yetu, ije na mkakati Bora utakaowezesha vijana waingie kujiajiri, vikwazo viondolewe, Kodi ziwe Rafiki Ili wapate pesa, wajiajiri na kutengeneza ajira Ili walipe mikopo na Kodi Kwa furaha.

Karibu Kwa ushauri 🙏
 
Tunakuwa wapuuzi sana, kila kitu tunalaumu serikali.
Unatoka kwenu Namanyere unakuja Kariakoo unapanga biashara katikati ya barabara ukiondolewa unaihoji serikali uende wapi, hicvvi na hawa matajiri nao wakapaki magari mlangoni kwako wanafanya service utaendaje kuharisha wali wako wa maharagwe yaliyochacha?
Samahani boss!!
 
Back
Top Bottom