Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi yazionya Hospitali Binafsi kutokupokea Wagonjwa Wa dharura na Kuwa Discharge Wagonjwa mahtuti

Huduma bora mtapata kule kwenye hospitali zitakazofata maelekezo ya NHIF, Kwani wapi NHIF wamesema msipate huduma bora..? Btw, private institutions hazilazimishwi (not obliged) kuomba wafanye kazi na NHIF ila athari za hio kitu zitawatafuna wao, serikali na nyie wagonjwa.
 
Hiyo uliyoscreenshot kuonyesha dawa na price zake
Ndo hiyo hiyo Mkuu ipo kuanzia Ngazi ya Chini sana na mpaka ngazi ya Juu..
Ninazo nyingi but nitakutumia nikikaa poa zipo kuanzia Dispensary level mpaka National Hopital Level
 
hahaha, usifanye mzaa na aliyeshika makali bhn, anakukata muda wowote. APHFTA yamemshinda.
Wanarudi mezq ya majadiliano.. hao wataalamu wa afya kuna sehemu watajua. Namna ya kufanya comeback siku ukienda kutibiwa ndio utajua hujui...
hahaha, usifanye mzaa na aliyeshika makali bhn, anakukata muda wowote. APHFTA yamemshinda.
 
Ila Awamu hii ni zaidi aisee
Dr bado me najiuliza hivi ni kweli mtu avunjike mguu halafu gharama ya kumukea hogo iwe 12,000/= hivi hawa watu ni wazima kweli ? Hivi elfu 12 ndio gharama ya kumhudumia mtu aliyevunjika mguu? Hivi Ummy Mwalimu mbona anafanya mzaha sana

Dr Mambo Jambo kama inawezekana kuweka hapa vipengele vya gharama na huduma kwenye hicho kitika tukijadili tusaidie mfano hii ya hogo nimeitoa kwa Malisa imebidi nicheke nikajiuliza hivi Ummy alishawai kufanya hata biashara ya mihogo?

Ndio maana namkubali sana @Dr ngwajima maana yeye kwenye mambo kama haya huwa anakuja direct hapa tunapambana nae kwa hoja na anajibu maswali yetu maana kwanza si muoga! Naamini Ummy angekuwa na ubavu wa kuja uku angeelewa…lakini ni muoga maana hana la kutuambia hata @wizara ya afya nao wapo humu wanaogopa kujibu lolote kwa sababu ya uongo uongo!
 

Attachments

  • IMG_2049.jpeg
    594.6 KB · Views: 2
Ni nyingi sana ila nilipata Muda baada ya mazishi ya Mh Rais mstaafu tutachambua
 
Basi huenda kwa Mirembe kwa sababu ni Hospitali ya Taifa ya Mental Health huenda wanapokea Ruzuku ya Punguzo la Dawa..
ILa kwa sokoni haiko hivyo..

Tukumbuke Private haipati Ruzuku kutoka serkalini inajiendesha yenyewe
Sawa Mkuu,,, kwa kweli garama imeshuka sana maana mirembe wao kwa sasa olanzapine gm 10 ,wanauza tsh 300 kwa tembe moja akati kuna phamarcy zipo zipo mkabala na general hospital ya Dodoma ,wanauza tsh 1500 tena kwa kidonge cha gm 5 ,, hapo pamoto sana kwa family zisizo na uchumi mkubwa.
 
Tatizo waTanzania mnaletaga emotions sehemu ya kutumia akili. I am not supporting hiki kitita kipya either lakini 12k kwa POP is okay, hio ni gharama tu ya huduma. Bado NHIF wanalipa consultation fee hapo na kama kuna any diagnostic imaging itafanyika watalipa pia. Wengi mnalalamika ili muonekane na nyie mnafatilia current issues ila madai hayana mashiko. Wachache sana ndo wanaelewa nini kinalalamikiwa na wanagusa exactly where it needs to be discussed. Acheni emotions ndugu mwananchi, mnafanya hata wenye hoja muhimu waonekane wote hawana akili.
 
Kwa hiyo hospitali binafsi kulalamika ni kama wehu na hawana hoja? Ni kweli kabisa ni halali kabisa mtu kufungwa hogo kwa 12,000/= ? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Wananchi kulia Tanzania ni jambo la kawaida. . .
 
Kwa hiyo hospitali binafsi kulalamika ni kama wehu na hawana hoja? Ni kweli kabisa ni halali kabisa mtu kufungwa hogo kwa 12,000/= ? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Unataka afungwe kwa shilling ngapi..?
 
Huu uongo utautubu Lini??
Uongo wa nn wanakupa dawa nyingi ili wapige hela kuna hospital moja ilikuwa ukienda hata kama una tatizo dogo lakini lazima wakupe kitanda ulale ili wapige hela na kuweka drip za uongo.
 
Uongo wa nn wanakupa dawa nyingi ili wapige hela kuna hospital moja ilikuwa ukienda hata kama una tatizo dogo lakini lazima wakupe kitanda ulale ili wapige hela na kuweka drip za uongo.
Sasa ukipewa dawa nyingi wao hawali hasara ya kutoa Dawa hizo nyingi???
 
Serikali irekebishe miundo mbinu na huduma zake iwahudumie watu wake fully. Mbona hii iko wazi kibiashara!?
 
Watanzania tuko more than 60 milion hebu tuambie kuna jumla ya hospitali, vituo vya afya na zahanati ngapi nchi nzima? Je hospitali za serikali ni asilimia ngapi na za binafsi ni asilimia ngapi? Je wewe kama hapo unapoishi ni jirani na hospitali ya serikali una hakika kila Mtanzania yuko jirani na hospitali ya serikali? Kingine wenye hizo hospitali binafsi wameajiri watanzania wenzako wangapi? Hoja yangu ni kwamba tujadili kiini cha tatizo na siyo kuanza kujadili ubaguzi, leo unahamasisha watu waachane na hospitali binafsi kesho utahamia kwenye shule binafsi Vs za serikali. Miaka ya nyuma hizi bima za afya zilikuwa nyingi tuu Jubilee, AAR, Strategy etc mpaka NSSF walikuwa na bima ya afya, jambo hili lilikuwa zuri kwa sababu kulikuwa na uwigo mpana wa hizi huduma na wafanyakazi na watu wengine walikuwa huru kuchagua mfuko waupendao. Jambo hili lilifanyika NHIF kutozidiwa na wateja na hivyo mfuko kuwa na uwezo wa kuhimili. Sasa hivi mfuko umezidiwa na ukichanganya na changamoto za uendeshaji (mfano kukopeshana fedha za wanachama) ndiyo kabisaaa...
 
CCM wanaweza kuzifungia, uliona waziri Ummy alisema wakiwaondoa wagonjwa wanafungiwa kutoa huduma. CCM wao wanajiona wako juu ya sheria. NHIF ni mali yao na wanajichotea mapesa tu huko, ahalafu watoa huduma wanasotea malipo yao.

Hizi ni siasa, za ccm wao kama wanataka na wanaweza, wafute mikataba na watoa huduma wa private hospital. Hawa private hospital wanaweza kujiendesha bila hao NHIF, kwasababu walifanya hivyo muda mrefu kabla hawa NHIF hawajaja.

Serikali inataka itoe bei elekezi kwenye huduma, wakati vitendea kazi, mazinira ya utendaji na malipo ya waajiriwa private ni tofauti na kule Serikalini.

Bei Elekezi wapeleke hospitali zao ccm, hizi private waziache.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…