Swali ni kuwa Kuna shida gani hapo kuna nini kwanini Inatumika Nguvu nyingi sana?
Kwanini tusijadili hicho.kitita kuliko kutumia Nguvu?
Ukisikiliza maelezo ya waziri wa afya mh. Ummy Mwalimu ya jana kwa wenye ufahamu utaelewa nani ameleta sintofahamu:
1: Kama waziri aliunda tume, ikaleta majibu kwenye kikao.
2: APHFTA walisikiliza hoja za tume na kuomba kwenda kupitia maelezo husika ili waje na mrejesho pia. Huwezi kujibu chochote wakari unapata taarifa kwa mara ya kwanza.
3: Baada ya hapo nini kilifuata??
NHIF na Serikali kwenda kuingiza kitita kipya kwenye utekelezaji. Kwa nini wakati mawasiliano yanaendelea, na kikao kinachofuata ndo kilikuwa cha kusikiiliza APHFTA??
4: Kwenye sintofahamu angalia mtu anaevulumisha maneno mengi mengi bila sababu kufunika nia ovu. Nani alikimbia meza ya mazungumzo?
5: Vyovyote iwavyo kama haya mambo yasiposhughulikiwa kwa utashi mwema, sisi mashabiki ndo tutaumia na familia zetu, rafiki au ndugu. Tutapata huduma isiyokidhi vigezo.
Sijui kama NHIF pia walishafanya utafiti kuja kwa nini wanufaika wa mfuko wanakuwa na multiple visitations? Watu wanajitahidi kufanya the minimal they can. Tatizo la kuonwa mara moja mtu anazunguka vituo kibao kila mmoja akiogopa kufanya vipimo kwa pamoja. Mbonanhao wa bima nyingine hawazunguki?
Watapiga picha, wataunganisha NIDA na kuweka signature pads LAKINI ni muhimu wabadili attitudes na approach yao kwa watoa huduma za afya.
6: Aliyesababisha gharama za uendeshaji kuwa juu hataki kulipia gharama husika. Kodi rukuki zimepelekwa kwenye vituo hivihivi vya afya bila kujali kuwa atakaekuja kulipa ni mtumiaji wa mwisho.
A: GHARAMA HALISI/HITAJIKA ZA UENDESHAJI
1: UMEME
2: MAJI
3: PANGO
4: TAKA
5: MISHAHARA
6: MASHINE ZA VIPIMO
7: DAWA
8: OTHER CONSUMABLE/REAGENTS/KITS
9: VIFAA TIBA
10: SUPPORTIVE SERVICES ULINZI
11: USAFI NA VITENDEA KAZI
Nk.
GHARAMA ZITOKANAZO NA SERIKALI
1: TRA
2: FIRE/ZIMAMOTO
3: OSHA/USALAMA MAHARA PA KAZI
4: HALMASHAURI/MANISPAA
5: LESENI YA DAKTARI
6: NEMC/MAZINGIRA
7: USAJILI WIZARA
8: TAEC/MIONZI
9: LESENI YA MAABARA
10: LESENI YA PHARMACY
Nk.
Kama serikali imelipwa kodi na ina nia njema, kwa nini tasisi zake zinakuja kwa mlango wa nyuma kudai malipo tena na si kutoa huduma na kuhakiki vigezo?
Swali ni kuwa Kuna shida gani hapo kuna nini kwanini Inatumika Nguvu nyingi sana?
Kwanini tusijadili hicho.kitita kuliko kutumia Nguvu?