Acheni Uoga Watanzania wenzangu, nawasihi sana, ushahidi tulionao sisi ni kama Mbuzi kafia kwa muuza supu, tulieni, nchi nzima si wajinga, wataalamu wetu si wajinga kama mnavyodhani, unajua mtanzania mmoja mmoja anavyojiona kuwa yeye ni tahira au kichwani hamna kitu au uwezo wake mdogo wa kielimu anadhani ndivyo ilivyo kwa timu zilivyochunguza na kutoa report..... tulieni vijana, sisi ni nchi masikini kwa kipato lakini tumejitahidi kusomesha watu wetu, hivo nawaomba sana msiwe na wasiwasi...
Hata vitani si askari wote wanapigana vita, wengine kazi yao ni kutunga nyimbo za kuwahamasisha na kuwatia moyo na ari wenzao ili waweze kupigana kwa nguvu kubwa, hivyo ni sawa na vita hii, ninyi wengine kwa sasa mtuunge tu mkono na kutoa ushauri mzuri, acheni wengine tuingie vitani...