Tetesi: Bodi ya Ushauri ya Kimataifa Kuhudhuria Mazungumzo ya Barrick/Acacia na Serikali

Tetesi: Bodi ya Ushauri ya Kimataifa Kuhudhuria Mazungumzo ya Barrick/Acacia na Serikali

Si lazima niandike kujibu swali lako bali nafanya muendelezo wa hoja yako. Hakuna anayewaogopa wazungu na wala msijifarague kwa kukwepa wajibu wa hao mnaowashabikia hivi sasa katika kutufikisha hapa tulipo. Yaani ni rahisi kwenu kuwaambia CHADEMA kwamba wamepoteza dira kwa kumpokea Lowassa lakini inakuwa ngumu kwenu kusema tumefika hapa kwa ajili ya matendo ya Mkapa na Kikwete.

hofu yetu haijengwi kwa kukutana na wazungu bali kwa jinsi wenyewe tulivyoitengeneza njia ya kukutana nao. Nashukuru kwamba safari yangu bado ni ndefu, Mliofika na kujibweteka ndiyo mliotufikisha hapa tulipo!
Huendelezi hoja yangu.

Hakuna sehemu hata moja ambapo nilizungumzia mambo ya Uafrika na uzungumzaji/uandikaji wangu wa lugha ya Kiingereza.

Hayo umeyaleta mwenyewe. Nimekuuliza yanahusianaje na kwenda kwenye meza ya mazungumzo na Acacia, umeshindwa kujibu.

Sasa eti unaongelea mambo ya mwendelezo wa hoja yangu!

Hoja yangu wala hujaielewa ndo uweze kuiendeleza?

Unaumwa wewe!
 
Hilo la kushiriki kwenye bodi halibitaji vichwa wala miguu....na mimi naweza. Suala ni kwenda na agenda ambayo iko clear kabisa. Yaani tunataka walau 50-50 zaidi ya hapo hakuna mazungumzo na madini ni yetu tutakufa nayo basi...

Madini ni yetu watu watupande kichwani????
 
Huendelezi hoja yangu.

Hakuna sehemu hata moja ambapo nilizungumzia mambo ya Uafrika na uzungumzaji/uandikaji wangu wa lugha ya Kiingereza.

Hayo umeyaleta mwenyewe. Nimekuuliza yanahusianaje na kwenda kwenye meza ya mazungumzo na Acacia, umeshindwa kujibu.

Sasa eti unaongelea mambo ya mwendelezo wa hoja yangu!

Hoja yangu wala hujaielewa ndo uweze kuiendeleza?

Unaumwa wewe!
Kama sijaijua inawezekana wewe mwenyewe unaandika usichokijua. Hoja yako ni kwamba wanaopingana na njia inayotumiwa na serikali katika kupambana na Acacia eti wanawaogopa wazungu.

Lugha ni sehemu ya utambulisho wa jamii husika. Unavyotumia Kiingereza kwa mbwembwe kama vile wasioijua hiyo lugha ni majuha ni aina moja wapo ya kuwatukuza wazungu. Ingawa Kiingereza ni Lugha tu kama Kimatumbi lakini inapotumiwa kuonesha utofauti wa hadhi ya mtu ni ulimbukeni!
 
Tunatetea tusije yakatukuta kama yale ya Meli ya Samaki wa wachina. Hivi tunalipa zile hela badala ya kuzitumia kujiletea maendeleo kwa kosa letu sisi ama la hao wana CCM wenzenu?
Huna taarifa za kutosha meli ya masamaki hatukulipa hata shilingi na limeli lenyewe lilizama posta ya zamani.Wahuni Wale capteni wa meli na vibaka wenzie walifungua kesi ili watoke kwa dhamana ambayo ilikuwa meli lenyewe walipotoka tu wakakimbia nchi wakalitelekeza limeli hadi Leo hawajulikani Waliko. Wanasakwa kwa udi na uvumba na mmiliki ambaye hakuwahi kuwatuma kuvua tanzaNia na walikuwa wakivua wanauza pesa wanatia ndani bila mmliki kujua. Kaeni hapo na vitaarifa vyenu koko
 
Wacha kututisha wewe
Hapa lazima watulie
Tumeamu damu itoke isitoke
Tumekataa kuibiwa
 
Madini ni yetu watu watupande kichwani????
Madini ni yetu ila migodi ni yao kwa sisi wenyewe kuwapa kwa mikataba ya kijinga sana iliyoshabikiwa na CCM. Pia kumbuka kuwa masoko ya hayo madini yako kwao wao wenyewe!!

Tatizo CCM haina ajenda ambayo iko "Clear" kwenye mambo yahusuyo rasirimali za taifa letu!!
 
Nyerere alipambana na kundi kubwa na hadi leo wanamuogopa
Mtu mwizi hata angekuwa na cheo haisadii
Hakuna kuogopa kitu
Kwa kila Jambo ni kumtanguliza Mungu!
Hata kama tulisaini , kama kuna udanganyifu , lazima tutavunja
Kulikuwa na biashara ya utumwa ilifutwa
Wazungu walikuwa wanayuuza
 
.Wahuni Wale capteni wa meli na vibaka wenzie walifungua kesi ili watoke kwa dhamana ambayo ilikuwa meli lenyewe walipotoka tu wakakimbia nchi wakalitelekeza limeli hadi Leo hawajulikani Waliko. Wanasakwa kwa udi na uvumba na mmiliki ambaye hakuwahi kuwatuma kuvua tanzaNia na walikuwa wakivua wanauza pesa wanatia ndani bila mmliki kujua. Kaeni hapo na vitaarifa vyenu koko
ALIYEWAAJIRI Wachina wa ‘Samaki wa Magufuli’ walioachiwa huru, amefungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania akiidai Serikali zaidi ya Sh bilioni saba, kutokana na meli iliyozama na samaki waliotaifishwa.

Mdai huyo Said Mohammed alifungua kesi hiyo chini ya hati ya dharura dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), ambapo imepangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Ama-Isario Munisi.


Mdai katika madai yake anadai Meli ya Tawariq 1yenye thamani ya Dola za Marekani 2,300,000 na fedha taslimu za kitanzania Sh 2,074,249,000 za samaki ambazo zilifanyiwa uthamini Oktoba mosi, 2009.

“Meli ya Tawariq 1 ilifanyiwa uthamini mwaka 2008 na kuonyesha kwamba thamani yake ni Dola 2,300,000 , ripoti hiyo ilitolewa na Kampuni ya Cambodia Shipping Services Ltd.

Awali mawakili waliokuwa wakiwatetea Wachina hao walidai Serikali inatakiwa kulipa Sh trilioni 1.3 ikiwa ni gharama zote, ikiwamo meli, samaki, mawakili na mabaharia wake.

Wakili hao walikuwa Kapten Ibrahim Bendera na Wakili John Mapinduzi ambaye aliwahi kudai kwamba ile haikuwa meli ya kawaida, ilikuwa ni kama kiwanda kwani ilikuwa inafanya kazi ya kuvua na kusindika.

Agosti mwaka 2014 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwaachia huru Wachina wa ‘Samaki wa Magufuli’ na kuamuru Jamhuri iwarejeshee vitu vyao, ikiwamo meli ya Tawariq 1.

Wachina hao waliachiwa kwa mara ya pili, mara ya kwanza waliachiwa na Mahakama ya Rufaa Machi 28, 2014 , lakini walikamatwa tena na kushtakiwa upya kwa mashtaka hayo hayo yaliyofutwa.

Washtakiwa hao ni Nahodha wa Meli, Hsu Chin Tai na Wakala wa Meli ya Tawaliq 1, Zhao Hanquing, waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uvuvi haramu katika Ukanda wa Uchumi wa Tanzania.

Jamhuri iliwasilisha maombi ya kuifuta kesi hiyo mbele ya aliyekuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Isaya Harufani.
 
Chifu, ni ukweli mchungu kwamba hata jinsi negotiations za mikataba mbalimbali ya uwekezaji hapa nchi, timu zetu uenda kinyonge. Niliwahi kuhudhuria public consultation ya sera ya madini. Yaani wale wataalamu walikuwa wanaongea kuonyesha kwamba Tanzania kama nchi masikini haina voice mbele ya hao wawekezaji wanaokuja na pesa zao...
Tunaona hata kwa Tundu Lisu. Kitu cha kwanza alichofikiria ni kushitakiwa tu. Eti oh nyinyi hamjui jinsi nchi itakvyoshitakiwa na hawa "wazungu", mara Miga sijui nini. Yaani kujiona tumeshindwa kabla hata ya kujaribu.

Vizuri hao hao wazungu wamemuumbua na kukata kilimilimi chake.
 
Naomba tuziamini ripoti zetu zilizochunguzwa na maprofessor kibao.
Zile ripoti ni zao la utafiti sio Dini, hakuna swala la kuomba ziaminiwe, facts are stubborn, kama ziko sahihi tutapeta na kama ni za kupika au kukariri tumekwisha!
 
Kama sijaijua inawezekana wewe mwenyewe unaandika usichokijua. Hoja yako ni kwamba wanaopingana na njia inayotumiwa na serikali katika kupambana na Acacia eti wanawaogopa wazungu.

Unaona sasa? Unazidi kuonyesha kuwa hujui ninachokiongelea mimi.

Hilo ngoja niliache maana sina muda wa kumpigia mbuzi gitaa.

Lugha ni sehemu ya utambulisho wa jamii husika. Unavyotumia Kiingereza kwa mbwembwe kama vile wasioijua hiyo lugha ni majuha ni aina moja wapo ya kuwatukuza wazungu.

Moja, hivi Allen ni jina la Kiafrika eeh? Hilo jina sijui linamtukuza nani tu[emoji28]

Mbili, pole sana. Si ajabu nawe huwa unatamani sana kuijua vizuri lugha hiyo lakini huna uwezo huo.

Matokeo yake unaishia kuona na kudhani eti naitumia kwa mbwembwe wakati hakuna mbwembwe zozote zile. Mimi hutumia lugha ya kawaida kabisa. Lakini, huenda kwa viwango vyako vilivyo duni, ndo maana hata kawaida unaiona kuwa ni mbwembwe.

Tatu, kutokujua lugha flani hakuna uhusiano wowote ule na ujuha.

Wewe unaona hivyo kwa sababu ya hali yako ya uduni. Ndo maana unahusisha vitu ambavyo wala havina kabisa uhusiano.

Hakuna hata sehemu moja, hakuna mahala popote pale ambapo mimi nimewahi kuhusisha kutokujua Kiingereza na ujuha.

Ni mimi humu JF ambaye kwa muda wote niliokuwemo humu nimekuwa nikiunga mkono matumizi ya Kiswahili mashuleni na mahakamani.

Ni mimi huyu huyu ambaye nimekuwa mstari wa mbele katika kukienzi Kiswahili kwa hali na mali.

Lakini, kama mtu mwenyewe wewe unasoma mambo halafu huelewi ulichokisoma, sitegemei uwe umeshawahi kuyaona hayo maana si ajabu uliyasoma na hukuyaelewa.

Ingawa Kiingereza ni Lugha tu kama Kimatumbi lakini inapotumiwa kuonesha utofauti wa hadhi ya mtu ni ulimbukeni!

Una matatizo wewe.

Matatizo ya kudhani na kusadiki yanayochagizwa na hali yako ya kujiona uko duni na pia ujinga.

Hivi kuna mtu anayenizidi mimi humu katika kupinga kuhusisha lugha ya Kiingereza na hadhi ya binadamu?

Mimi hata kuhusisha tabia tu za kibinadamu na 'uswahili' napinga, seuze kuhusisha Kiingereza na hadhi?

Hahahaaaaa ndo maana nakwambia hujui ulisemalo wewe. Unasoma mambo lakini huelewi unachokisoma.
 
Dah!

Kwani hao nao si ni watu tu kama sisi!

Yaani tayari watu mshaonyesha hali ya kushindwa hata kabla ya kuanza kwa hayo mazungumzo kisa tu eti ya watu waliomo kwenye hiyo bodi ya hiyo kampuni!

Kwani tunaenda kushindana kurusha maroketi angani?

Bure kabisa!!!!!
Lazima tuwe na hofu kwani haya mataifa ndio kila mwaka tunayaangukia yatisaidie kwenye bajeti
 
Kilichowashitua hawa Wazungu ni hayo matrilioni tunayotaka watulipe madai ambayo huenda si realistic hivyo ni lazima nao wajipange.
Unauwakika sio realistic?? Kama bosi wao kaomba msamaha unafikiri akujua kinachoendelea?? Usituletee akilizako zakutazamia.
 
Tunaona hata kwa Tundu Lisu. Kitu cha kwanza alichofikiria ni kushitakiwa tu. Eti oh nyinyi hamjui jinsi nchi itakvyoshitakiwa na hawa "wazungu", mara Miga sijui nini. Yaani kujiona tumeshindwa kabla hata ya kujaribu.

Vizuri hao hao wazungu wamemuumbua na kukata kilimilimi chake.
Hayo ni mazingira mawili tofauti mkuu. Nilichoongelea mimi ni kabla ya uwekezaji. Anachokiongelea Lissu ni baada ya uwekezaji. Sasa kabla ya uwekezaji negotiation zilifanyika kwa Tanzania kujiona mnyonge, matokeo yake ndiyo kuwa na mikataba ambayo haina tija kwa taifa. Sasa alichokisema Lissu ni kwamba tatizo ni tayari tumeshajifunga na mikataba hiyo ya ajabu, hivyo tunapaswa ku-play smart!

Hadi sasa sijaona wazungu wamemuumbua vipi Lissu! Ebu nieleweshe jinsi walivyomuumba. Kwani alichokisema Lissu juu ya uwezekano wa kushitakiwa bado kinawezekana kama negotiations kati ya Barrick/Acacia na serikali hazitofanikiwa. Lissu alisisitiza pia juu ya negotiations na siyo kutumia nguvu na mabavu kukamata mchanga ambao ni mali yao Acacia kwa mujibu wa sheria zetu. Kwa hiyo kimsingi, Magufuli anafanya vile Lissu na wazalendo halisi walivyopendekeza: kufanya majadiliano ili kufikia muafaka.

Sasa tusubiri na kuona nini kitafikiwa! Usianze kutukana mamba kabla hujavuka mto! Mpambano ndiyo kwanza hata halftime bado! Tuombe tu, negotiation team ya Tanzania iwe na watu wanaojielewa! Na tuombe taarifa za ripoti za Mruma na Osoro ziwe za kweli! La sivyo, alichokisema Lissu kitatimia! Maana usitegemee Barrick kulipa trilioni 108 kwa kutegemea ripoti hizo tu! Lazima atataka independent review! Fingers crossed, hoping for the best for Tanzania.
 
Niliwaambia kwanini sera isielekeze kwamba CSR itokane na matatizo ya msingi ya kijamii kwenye eneo husika? Mfano, kama ni uwekezaji kwenye gesi Mtwara, kwanini wawekezaji wasiambiwe part ya CSR ni kujenga world class hospital; ama kuweka miundombinu mikubwa ya barabara, maji, umeme n.k.
Safi sana ndugu nimependa hio suggestion yako kuhusu CSR terms.
 
Halafu utashangaa wawakilishi wa Serikali yetu watakuwa hawa wafuatao:-
1. Bashite
2. Lusinde
3. Deo Sanga
4. Mtemi Chenge
N.k.

Hapo ndipo huwa nasema Tanzania ni watu wa ajabu sana
Naongeza Mwingine. Josephat Kasheku Msukuma. Na yule Jamaa Aliyesema Iwekwe Sanamu ya Almasi Badala ya Sanamu ya Mashujaa.
 
Wakuu kazi haitakuwa ya Kitoto na tunatakiwa tuandae jopo letu la wataalamu na wanasheria vichwa n'a makini sana. Inasemekana Bodi ya Ushauri ya Kimataifa itakuwepo katika mazungumzo yajayo kati ya Barrick/Acacia n'a Serikali ya Tanzania. Kazi ya Bodi hii itakuwa ni kutoa Ushauri katika Mikataba iliyosainiwa zamani n'a pande hizo mbili. Sasa huenda katika mazungumzo hayo tukawashinda n'a tukapata pesa zetu au tukaambulia patupu kwa kuwa Mikataba tuliisaini wenyewe n'a makubaliano tuliingia. Na Nadhan watakuja na ushahidi wa picha, vielelezo na video.
Nisiende mbali, Hebu wajue wajumbe wa Bodi hii ya Ushauri ya kimataifa, tukiwajua itakuwa vizuri kujiandaa na kuwaandaa wataalamu wetu:

Bodi Ina members 12 ambapo wako Mawaziri Wakuu wastaafu wawili na mawaziri wengine wanne wa nchi nne tofauti na inaongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Canada, Brian Mulroney. Pia kuna Waziri Mkuu wa zamani wa Hispania, Jose Maria Aznar na Spika wa zamani wa bunge la wawakilishi la Marekani, Newt Gingrich. Yumo aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, John Baird na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, William Cohen na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Shirikisho la Ujerumani, Karl-Theodor zu Guttenberg. Yumo aliyekuwa Mshauri Mkuu wa Margreth Thatcher na John Major kuhusu masuala ya nchi za nje. Pia yuko Mtanzania na mwafrika pelée Balozi Juma Mwapachu.
Hata aje Babu Abrahamu, bado rasilimali ni ya Tanzania na maamuzi yatatolewa na Tanzania hao Acacia au Barrick ni madalali tu
 
Back
Top Bottom