Bodi ya Utalii Tanzania: Hatujamtuma Mwijaku Kutangaza Utalii Mitaani Ujerumani

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Bodi ya Utalii imemkana Mwijaku πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema haijamtumia wala kumtuma mtangazaji na mwigizaji, Mwemba Burtony maarufu kama Mwijaku nchini Ufaransa kutangaza utalii mitaani, akiwa balozi wa utalii kwa niaba au kwa gharama za Serikali.

Katika taarifa iliyotolewa na TTB, imesema mwaka huu TTB ilishirikiana na Sekta Binafsi kwenye maonyesho ya utalii ya Ufaransa ambayo yalifanyika kuanzia Oktoba 03 hadi 05, 2023 na ilikwenda na kampuni 12 ikiwemo kampuni ya Asha Tours EK ambayo ndiyo ilimgharamia Mwijaku kwenda kufanya utangazaji wa kampuni yake inayofanya biashara ya utalii yenye makao makuu Hamburg, Ujerumani.


Mwijaku

β€œTTB inakanusha kumtumia Mwijaku na inatoa tamko kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote asiye na dhamana ya kutangaza wala kuhamasisha utalii kwa mujibu wa sheria za Tanzania na taratibu zilizowekwa.” imesema taarifa.

Aidha, Bodi ya Utalii imewataka watu wote kuzingatia sheria kwenye utoaji wa taarifa au utangazaji na uhamasisha wa utalii ndani na nje ya nchi.



Swali.
Kwani mtu akiamua kutangaza Utalii ni lazima atumwe na Bodi ya Utalii? Akili za Kijima ni tatizo jingine kubwa Tanzania.
 
Kila sector Ina weledi wake the "Dos and the Don'ts" akitoa boko anaua brand ya destination
Weledi upi? Anachofanya Wade Maya kina maana na impacts kuliko nyie mliokariri mavitabu na hamjielewi
 
Ninachoona wanaweka ambo sawa kwakua mwijaku hakawii kusema kagharamiwa na serikali kwahyo na wao wanajitetea. Kwenye swala la kutangaza utalii sio lazima awe mwijaku yeye akifanya ni kwa kupenda kwake.
 
Hakuna haja ya salamu.

Nimesoma hii barua. Nikauliza Bwijaku ni nani nikaambiwa ni mtangazaji anatangaza Utalii ufaransa. Bodi ya Utalii yasema haijamtuma. Nikajiuliza sikupata majibu.
 
Teh teh teh teh

Akili ndogo inapohatamu akili kubwa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…