Bodi ya Utalii Tanzania: Hatujamtuma Mwijaku Kutangaza Utalii Mitaani Ujerumani

Bodi ya Utalii Tanzania: Hatujamtuma Mwijaku Kutangaza Utalii Mitaani Ujerumani

inatoa tamko kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote asiye na dhamana ya kutangaza wala kuhamasisha utalii kwa mujibu wa sheria za Tanzania

Kwamba kutangaza vivutio vya Tanzania ni hadi uwe na kibali...duh!
 
Wewe ni mpumbavu msanii wa Nini?, Ana maisha gani? Yakushinda anaombaomba kwa kina Ali kiba na Mondi?.
Upumbavu wako ni beyond limit
download.jpg
 
Bodi ya Utalii imemkana Mwijaku 😂😂😂

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema haijamtumia wala kumtuma mtangazaji na mwigizaji, Mwemba Burtony maarufu kama Mwijaku nchini Ufaransa kutangaza utalii mitaani, akiwa balozi wa utalii kwa niaba au kwa gharama za Serikali.

Katika taarifa iliyotolewa na TTB, imesema mwaka huu TTB ilishirikiana na Sekta Binafsi kwenye maonyesho ya utalii ya Ufaransa ambayo yalifanyika kuanzia Oktoba 03 hadi 05, 2023 na ilikwenda na kampuni 12 ikiwemo kampuni ya Asha Tours EK ambayo ndiyo ilimgharamia Mwijaku kwenda kufanya utangazaji wa kampuni yake inayofanya biashara ya utalii yenye makao makuu Hamburg, Ujerumani.


“TTB inakanusha kumtumia Mwijaku na inatoa tamko kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote asiye na dhamana ya kutangaza wala kuhamasisha utalii kwa mujibu wa sheria za Tanzania na taratibu zilizowekwa.” imesema taarifa.

Aidha, Bodi ya Utalii imewataka watu wote kuzingatia sheria kwenye utoaji wa taarifa au utangazaji na uhamasisha wa utalii ndani na nje ya nchi.

View attachment 2777107

Swali.
Kwani mtu akiamua kutangaza Utalii ni lazima atumwe na Bodi ya Utalii? Akili za Kijima ni tatizo jingine kubwa Tanzania.


Yes, lazima kama anatangaza upumbavu bila busara na uwashilishwaji mzuri, mbona hawajawahi mkana bongozozo?
 
Wahuni Ni Kuwabaini Popote Walipo Na Kuwakataa
 
Bodi ya hovyo sana hiyo hamjui mnafanya nini badala ya kushukuru watu wanatangaza utalii ninyi mnadhani kwa sababu mbuga zipo wageni watakuja tuu Tanzania ndio Nchi yenye vitu asili ambavyo Nchi nyingi hawana ila kwa sababu Bodi yenyewe ndio hawa tunabaki kushindwa na hao wanaotengeneza Mbuga...
Inatakiwa Timu zote ziwe na nembo za Mbuga zetu au Mlima Kilimanjaro...
Kuandaa matamasha Spain ambayo yatatangaza Mbuga zetu...
Utalii utangazwe mpaka kwenye mashirika makubwa ya ndege na viwanja vyao...
Mkifanya mambo ya Utalii kwa usahihi mtaacha kwenda kuomba hela kwa Waarabu ni vile hatuna akili wakati mali tunazo....
Bodi ya Utalii wapo bize kuhkikisha wamasai wanaondoka huko kwanza🤣
 
Sawa mwijaku ni chizi, mpenda sifa za kijinga, hilo liko wazi.
Ni chawa na huenda hili analifanya kwa malengo yake ya uchawa chawa, lakini hajakosea..
Pili wanasema kampuni waliyoingia nayo mkataba ndio wanamtumia mwijaku, hapo case closed

Yaani mie nipande ndege mpaka mjini london kwa gharama yangu, kisha niutangaze mlima Kilimanjaro,kosa langu lipi hapo.
 
Wangesema kavunja Sheria gani au utaratibu gani mbona kama wanamuogopa vile.
Na wale wanaomponda Mwijaku hivi kawafanya nini?
Mtu anapambana kivyake nini tatizo?
Lazima tukubali hatuwezi kufanana na nchi isiyo na diversity haitaendelea.
 
Bodi ya Utalii wapo bize kuhkikisha wamasai wanaondoka huko kwanza🤣
Watu wa Bodi ya Utalii niliona wanaulizwa na wageni kipindi cha kutalii Tanzania wanajibu eti kuanzia September kwa hiyo miezi mingine hata kama ni low season wanyama wanakua hakuna? Badala ya kusema karibuni Tanzania through out the year wao wanajibana nilichoka sana ndio maana wana mambo ya hovyo hovyo sana...
 
Mwijaku Akirudi apekuliwe.
_90282820_c7d3098f-eb19-4577-bafd-2f8379c96d7c.jpg
Asije kuwa amebeba Kunguni.

Hivi karibuni kumetokea taarifa kuwa kunguni wamezagaa Ufaransa na wana uwezo wa kupanda daladala, mabegi, masanduku, suruali na chupa za marashi.😅
 
Back
Top Bottom