Bodi ya Utalii Tanzania: Hatujamtuma Mwijaku Kutangaza Utalii Mitaani Ujerumani

Bodi ya Utalii Tanzania: Hatujamtuma Mwijaku Kutangaza Utalii Mitaani Ujerumani

Hao walioandika hiyo barua hawana akili....hawakuwa na sababu ya kuuaminisha umma eti hawausiki,wangekaa kimya ingekuwa busara zaidi.....kwanza kutangaza utalii wa nchi Yako mpaka utumwe
 
Bodi ya Utalii imemkana Mwijaku 😂😂😂

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesema haijamtumia wala kumtuma mtangazaji na mwigizaji, Mwemba Burtony maarufu kama Mwijaku nchini Ufaransa kutangaza utalii mitaani, akiwa balozi wa utalii kwa niaba au kwa gharama za Serikali.

Katika taarifa iliyotolewa na TTB, imesema mwaka huu TTB ilishirikiana na Sekta Binafsi kwenye maonyesho ya utalii ya Ufaransa ambayo yalifanyika kuanzia Oktoba 03 hadi 05, 2023 na ilikwenda na kampuni 12 ikiwemo kampuni ya Asha Tours EK ambayo ndiyo ilimgharamia Mwijaku kwenda kufanya utangazaji wa kampuni yake inayofanya biashara ya utalii yenye makao makuu Hamburg, Ujerumani.


“TTB inakanusha kumtumia Mwijaku na inatoa tamko kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote asiye na dhamana ya kutangaza wala kuhamasisha utalii kwa mujibu wa sheria za Tanzania na taratibu zilizowekwa.” imesema taarifa.

Aidha, Bodi ya Utalii imewataka watu wote kuzingatia sheria kwenye utoaji wa taarifa au utangazaji na uhamasisha wa utalii ndani na nje ya nchi.

View attachment 2777107

Swali.
Kwani mtu akiamua kutangaza Utalii ni lazima atumwe na Bodi ya Utalii? Akili za Kijima ni tatizo jingine kubwa Tanzania.
Kuitangaza nchi kunahitaji kibali? Duh, hii ni kali aise, yaani ni kali sana kama picha la Cyborg vile.
 
Kwani mtu kutangaza Utalii Hadi atumwe na Bodi ya Utalii.Akili za kipunda punda za Majitu ya hovyo huko maofisini.
Mkuu pengine ,mwijaku kuna maneno atakuwa kayazungumza ndio maana TTB , wamekuja kuzuia hiyo Tabia,

Badala ya yeye(mwejaku) kuitangaza tz yeye anaitia auibu taifa
 
Watu wa Bodi ya Utalii niliona wanaulizwa na wageni kipindi cha kutalii Tanzania wanajibu eti kuanzia September kwa hiyo miezi mingine hata kama ni low season wanyama wanakua hakuna? Badala ya kusema karibuni Tanzania through out the year wao wanajibana nilichoka sana ndio maana wana mambo ya hovyo hovyo sana...
Wasomi wetu wengi ni wapumbavu sana
 
Mwaka jana nilienda Spain,France kutangaza Utalii ili wageni waje Tanzania kupitia Mothercitysafaris.Company Ltd watoe tamko basi hatutakiwi kuungaza Utalii ni wao walio ofisini ndio wafanye hivyo...
Makampuni yanajitegemea kwa kila kitu kwenye utangazaji kwa gharama kubwa hawa wasiojua kitu wanajifanya ndio wasemaji wetu hata ukiwauliza faida ya kutangaza Utalii wetu hawajui kitu..
 
Hawa tunaowaita wasomi .maofisini uko ni mazuzu kbis hamn kitu kichwani. Bongo zozo alianza kufanyag hiv hiv mwsh WA siku aliitwa mpaka bungeni adi wizara nazan alipew na deal. Sas mtz akifany muna mkana. Daah
 
Bongo zozo huwa anatangaza sana utalii wa Tanzania. I hope ana kibali cha TTB
 
Back
Top Bottom