Body(mwili), soul(nafsi) and spirit(roho)

Body(mwili), soul(nafsi) and spirit(roho)

Internal

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
3,579
Reaction score
3,919
Hapa najua kuna watu wakubwa mno, wenye ufahamu sana, nimeamua kujitupa uku nijifunze zaidi.

Je mtu ana mwili na nafsi au mwili nafsi na roho?

Naamini kwa hakika hili ni swali la msingi sana kwa kila mtu anahitaji kupata majibu sahihi na yakuaminika zaidi (correctly an reliable answered).

Ni vyema zaidi kujadili na kufahamu kwa undani juu vitu hivi vitatu ki ujumla wake.

Katika makala hii nitaangazia japo kwa ufupi saana kile ninachofahamu, naamini ni wengi wametia mikono na kuandika na kuchambua kinaga ubaga juu ya mada hii, lakini si vibaya na mimi nikitia mikono na mchango wangu kwa ufupi.

1. Body, Soul And Spirit

Kabla ya kwenda moja kwa moja kwenye mada yetu ya mwili, nafsi na Roho turejee kwanza kwenye kitabu cha mwazno cha biblia (Genesis). Kitabu cha mwanzo ndio msingi mzima kila kitu, kimeandikwa kwa ufupi lakini kimebeba mwanzo wa kila chenye mwanzo, naamini hata mada tajwa hapo juu hapa ndipo inapoanzia.

GENESIS 2:16-17
16 Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, matunda ya kila mti wa bustani wawezakula,
17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku(in the Day.. Biblia ya kingereza) utakayokula matunda ya mti huo utakufa hakika.
Katazo au maagizo Mungu aliompatia adamu ni kwamba asile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, kwa lugha nyepesi ya kueleweka ni kwamba siku atakapoyagusa na kuyala atakufa kwa hakika ndani ya siku hio hio.

NOTE:
Mambo mawili muhimu yanapatikana hapo…
1: in the Day(ndani ya siku hio hio)
2: Surely die ( Hakika utakufa)

Kifo ilikuwa ni 100% kitokee siku adam angegusa na kula matunda ya mti aliokatazwa.

Sasa katika Mwanzo 3:1-6 tunajua vile shetani alivyo mdanganya hawa na adam hatimaye wakavunja agizo walilopewa na Mungu, na kasha wakala tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Baada ya kula tunda kulingana na agizo la Mungu ilikuwa lazima wapatwe na kifo hapo hapo (at a moment) kama Mungu alivyosema Mwanzo 2:17.

17 walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku(in the Day.. Biblia ya kingereza) utakayokula matunda ya mti huo utakufa hakika.

Tatizo liko hapa Mwanzo 5:5-6, Inasemaje kuhusu Adam?

5 “Siku zote za adam alizoishi ni miaka mia kenda na thelathini, naye akafa.

Kwahiyo; kulingana na biblia, adam aliendelea kuwa na maisha au kuwa na uhai ndani yake kwa miaka mingi baadaye baada ya kula tunda hali ya kuwa Mungu alisema kwamba siku utakapo kula hakika utakufa ndani ya siku hio. Sasa nini kilitokea ndani ya siku hio amabapo adam na hwa walipokula tunda? Did they die as God said, au hawakufa?

Who will solve us this problem?
Man’s ideas, theories, religion and tradition? No Only one can give us answer na si mwingine ni Mungu mwenyewe kupitia Neno lake. Na kama unataka biblia kukupatia jibu ni lazima tuiruhusu ijitafsiri yenyewe. Biblia na biblia pekee yatosha.

Kumbuka Hesabu 23:19 inasema.. “mungu si mtu aseme uongo…..”

Tuendelee.. siku Adam na hawa walipokula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya walikufa kwa hakika(they real died). Actually, alikuwa ni sheta aliyesema hamtakufa hakika wakati anamrubuni hawa. Hivyo basi kama wasingekufa siku ile, kama Mungu alivyosema basi shetani angekuwa sahihi kabsa kuwaambia hamtakufa hakika na mungu angekuwa muongo kwa kuwaambia mtakufa hakika, kitu ambacho isingewezekana Mungu kuwa muongo.

Hesabu 23:19. inasema.. “Mungu si mtu aseme uongo…..” Hata hivyo wengi leo hufundisha kwamba wakati Mungu aliposema utakufa hakika alimaanisha kuna mbegu ya kifo itakuwa planted ndai ya adam baada ya kula tunda. Nene la Mungu halihitaji kukingiwa kifua kwa namna hio.

Halihitaji kutetewa wala kukingiwa kifua kwa kile ilichosema kabla badala yake ni ukweli ukweli pekee utasimama. Returning to our topic: Tangu Mungu aliposema wangekufa siku hio, kwa hakika walikufa siku hio hio (SINCE GOD SAID THAT THEY WOULD SURELY DIE THAT VERY DAY, THEY INDEED DIED THAT DAY).

Hata kama waliendelea kuwa na uhai ndani yao baada ya kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ni dhahiri kwamba baada ya kula tunda kuna kitu walikipoteza ndani ya miili yao. Hicho walichokipoteza siku hio baada ya kula tunda kulingana na maneno ya Mungu ndio kifo (absence of a form of life). Hivyo basi tuanapaswa kuangalia ni kitu gani kilichopotea kwa wazaz wetu wa kwanza baada ya kula tunda ambacho ndio kusema adam na hawa walikufa baada ya kukipoteza.

2. Body, soul and spirit: the body and soul aparts

Tunaanza kufanya uchunguzi wetu jinsi gani mtu wakwanza aliumbwa, kitabu cha Mwanzo.

Genesis 2:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi…”(“and the Loard formed man of the dust of the groung……”)
Ni sehemu gani ya mtu Mungu alioifanya kwa mavumbi ya ardhi? Mwili. Ndiyo maana element za mwili wa binadamu zinapatikana kwenye madini ya ardhi. Kwahio sehemu ya kwanza ya mtu ilikuwa ni mwili(body).

Let’s countinue:

Genesis 2:7 …..and breath into his noistrils the breath of life and man become a living soul.

Tumeona jinsi Mungu alivyomuumba mtu kwa mavumbi ya ardhi, hata hivyo haukuwa na uhai ndani yake. Uliumbwa bila uhai, kIsha Mungu akaupilizia ule mwili (body) pumzi katika pua zake pumzi ya uhai na mtu akawa nafsi hai(living soul. Soul is what givies life to the body. Hapa neon la Mungu linatuambia bila nafsi mwili umekufa.

Where is soul(nafsi iko wapi?), uhai wa mwili, the life of the flesh?

Mambo ya walawi 17:11, 13-14
11 “Kwa kuwa uhai wa mwli u Ktika hiyo damu;….. “(for the life of the flesh is in the blood…)
13 ‘’Mtu yeyote aliye wa wana wa Israeli, au hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake;atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga. 14 kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu ni moja na uhai wake……”

Tumekwisha kuona katika kitabu cha mwanzo kuwa nafsi(soul) ndiyo huupa mwili uhai. Hapa katika mambo ya walawi tunaona uhai wa mwili upo katika damu, kwahio uhai wa mwili ni nafsi. How this soul life passes from generation to generation? Through the blood. Acts 17:26“and he has mada from one blood every nation of men to dwell on all the face of the earth”.

Actually, sol is not something only man has. Animals have also soul which again is in the blood.

Mwanzo 1:20-21.
20 Mungu akasema maji na yajawe kwa wingi a kitu kiendacho chenye uhai……..
21 Mungu akaumba nyangumi wakubwa na kila kiumbe chenye uhai kiendacho…….”

Kwahiyo, sio binadamu tu bali hata wanyama wana nafsi hai, hili naamini sio jipya, kama tumeelewa kuwa nafsi hai(soul) ndio huupa mwili uhai, wakati tunapokufa hatuna uhai tena hatuna nafsi(soul). Vile vile hata kwa wanyama nao.although, there is no problem about what is defined as soul in the bible, the problem is created when we go to the bible with the preconceived ideas that soul is immortal. Soul is not something immortal. It just gives life to the body. When you stop having life in your body, you have no more soul.

Sasa tumeona vile Mungu alivyomfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi kasha akapulizia pumzi katika pua zake pumzi ya uhai ili kuupa mwili uhai. Kila mmoja wetu anakubali kabsa kwamba ana mwili na nafsi, tunaweza kuhitimisha kuwa adamu wakati anakufa akiwa na umri wa miaka930, wakati anakula tunda la mti wa mema na mabaya kwa hakika hakupoteza mwili wala nafsi.
Ikiwa hakupoteza mwili wala nafsi wakati alipokula tunda je alipoteza nini ambacho ndio kifo kama alivyosema Mungu?

Let’s continue searching…..

3: Body, Soul And Spirit: The Spirit Apart.

Mwanzo 1:26-27
The god said “Let us make man in our image, according to our likeness… so God created man in his own image, in the image of God he created him; male and female he created them.”

Kulingana na aya hii, mungu alimuumba mtu kwa mfano wa sura yake( zingatia sana hii point) swali la kujiuliza what is the image of God?? Anaonekanaje(what does he look like?

Yohana 4:24 inatuambi hivi…
God is not flesh but is spirit….(Mungu ni roho..). that is his image. Kwahiyo biblia inaposema Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake na kwa sura yke, ina maana kando ya mwili na nafsi bali pia alikuwa na mfanano na Mungu yaani roho.
God is not flesh. He does not have feet, hands,head, yeye ni roho.kama Mungu ni roho na adamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu ni dhahiri kuwa adamu naye ni roho. Mmoja anaweza akauliza kwanini Mungu amuumbe adamu na mwili, nafsi na roho pia?

Jibu rahisi ni kuwa bila adamu kuwa na form ya roho asingeweza kumuona mungu na kuwasiliana naye ana kwa ana kama walivyokuwa wanaonana katika bustani ya edeni, ikiwa mmoja angekuwa kiumbe cha roho na mwingine kiumbe chenye mwili isingekuwa rahisi adamu kumuona mungu maana mungu ni roho. Kama vile usivyoweza kupokea mawimbi ya sauti kutoka radio station nyumbani kwako bila kuwa na radio receiver ndivyo isingewezekana kwa adamu na Mungu.

Unahitaji radio receiver kusudi kupata mawimbi ya suti kutoka radio station.

1wakorintho 2:14 “basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuuzi,wala hawezi kuyafahamu, maana yatambulikana kwa jinsi ya rohoni”.

“But the natural, man does not receive the things of spirit of God, for they are foolishness to him: nor can he know, because they are spiritually discerned.”

Kulingana aya hapo juu mtu ambaye ana mwili na nafsi does not receive the things of the spirit of God. Kama nilivyokwisha kusema mambo ya roho ya mungu. Ili kuwasiliana na mungu unapaswa uwe na receiver i.e. spirit.

Summary
Adam alikuwa na mwili uliumbwa kutoka katika mavumbi ya ardhi, akapewa nafsi kwa kupuliziwa pumzi puni ilioupa flesh body uhai kisha akapewa na roho ili kuwasiliana na mungu. He was body, soul and spirit.baada ya adamu na hawa kula tunda ambapo mungu aliwaambia wakila hakika watakufasiku hio, ni hakika walikufa siku hio hio. Bearing in mind that death means the absence of form of life, tunaweza kuona sasa kifo kilichotokea siku ile.

Adam alikuwa ni mwili, nafsi na roho na mwili wake ulikufa miaka mingi baadaye after tht day that he ate, nafsi ndio inayoupa mwili uhai kama tulivyoona hapo awali, hivyo ni kusema baada ya kula tunda mwili na nafsi bado viliendelea kuishi miangi tu.

Mungu alisema kwa hakika siku utakayo kula utakufa hakika, tumeona vile mungu asingeweza kusema uongo kwamba adamu ale na asife, kabla ya admu kula alikuwa na sifa zote tatu body, soul, and spirit ilikuwa ni lazima afe maana alishakiuka masharti ya muumba wake. Baada ya kula tunda adamu alipoteza roho ambacho ndicho kifo chenyewe cha kiroho.

Baada ya adamu kula tunda alikuwa mfu mbele za Mungu, alikosa sifa ya kuwa na sura ya mfano wa mungu, hivyo akawA mfu. Na huu ndio ulikuwa mpango wa shetani kumfanya mungu na mwanadamu wakosane ili wasiweze kuwasiliana tena.
But God is I love, kupitia kwa mwanae tunakuwa viumbe vipya tena kwa kumuamuni tunarejeshewa kile kilichopotea pale tu adamu alipokula tunda.

1 Wathesalonike 5:23 “Mungu wa amani mwenyeweawatakase kabsa;nanyi nafsi zenu na roho zenuna miili yenu mhifadhiwemuwe kamili,……”

Asanteni...

Karibuni siwezi ku-tag, ningewatag wengi tu. Karibuni kwa ujumla wenu.
 
Huu uzi ulipotea ghafla jana wakati nikitaka kuchangia, anyway ngoja nikameze videsa kwanza ntarudi baadaye na mimi kusema chochote.
 
Sioni wapi Mungu amesema utakufa siku hiyo hiyo,neno linasema utakufa hakika,ikiwa na maana kuwa kuanzia pale kutakuwa na kufa na sio kuishi milele,ndio maana baada ya hiyo miaka 139 Adam alikufa...
 
Rekebeshia mpendwa, biblia imetofautisha kati ya Mungu na mungu, God and god

Rekebisha ili tuelewe najua ni typing error.
Asante
 
Siku utakayo kula matunda hakika utakufa utakufa,

Ahadi ya Mungu ilikuwa ni kuishi milele katik hii dunia.
Na Mungu kila jioni alikuwa anaenda kuwatembelea,

Walipokula ndicho kilicho tokea kufa ni adhabu, Mungu hakuweka kifo mwanzoni kifo kilitokana na adhabu ilitokana na kukiuka maagizo ya Mungu katika bustani ya Edeni

Ukisoma mwanzo vizuri utaona adhabu iliyo tolewa na laana ilitolewa

Katika adhabu hizo kifo ni kimojawapo
 
Hamna namna ya kuzipa nyuzi class, maana hii inafaa iwe first in the hi class thread, Hata Kiranga hana pakutokea.[emoji122] [emoji122] [emoji122]
Nimesoma, nikajiuliza, kuna kipi ambacho sijawahi kuandika naweza kuandika hapa?

Sijaona chochote.

Kiranga si mtu wa kuandika tu kwa kuwa anapenda kusikika, au anapenda kujipaza, au anapenda maoni yake mwenyewe.

Mara nyingine, kuwapa nafasi wengine nao waandike, Kiranga awe msomaji, apate kujifunza kutoka kwa wengine, weledi wao na mapungufu yao, ni kitu bora.

Ukiona Kiranga hajaandika, si kwa sababu hana cha kuandika, bali, sababu zinazopelekea hilo zinaweza kuwa nyingi sana.

Naweza kuwa naona kwamba katika kipimo cha usemaji kwa wiki hii nishapitiliza kusema, nahitaji kusikiliza zaidi.

Utanilazimisha niseme hata pale ninapoona kwamba natakiwa kuwaachia wenzangu nao waseme ili mimi nami niwe msikilizaji?

Hivi kila mtu aikitaka kusema katika kila anachoona anaweza kusema kunaweza kuwa na mazungumzo ya kusikilizana hapa?
 
Uzi ni mtamu sana na unafikirisha kweli kweli.
Lakini kuna hoja nitazipangua hapa.

Kwanza mwanadamu ni roho inayoishi katika nyumba inaoitwa mwili...
Kwa maana hiyo ni kwamba mwanadamu anatakiwa kuangaliwa kwa kigezo cha kiroho na sio nyumba yake anayoishi kwayo, na ndio maana hata hukumu ya mwisho haitakuwa kwa mwili ila kwa roho yake.

Kuna kitu kimoja cha muhimu sana ambacho watu huwa tunachanganya.
Biblia inasema hukumu za Mungu huwa zinatoka lakini kwa rehema zake Mungu huwa zinacheleweshwa kutekelezwa mara moja.

Mfano ni kipindi cha mnara wa Babeli, Mungu alipunguza urefu wa miaka ya mwanadamu kuishi kutoka miaka 900 na ushehe mpaka miaka 120, lakini punguzo hilo halikutokea ndani ya siku moja.


Watu waliendelea kuishi kwa miaka mingi mfano Ibrahimu na Yakobo waliishi miaka zaidi ya 170.
Na punguzo lile liianza rasmi kutekelezeka mpaka kipindi cha Musa.

Ukisoma kwenye Zaburi Daudi mwenyewe anasema kuwa miaka ya kuishi mwanadamu ni miaka 70 mpaka 80, lakini Daudi huyo huyo akaishi miaka 120.

Kwa hiyo nyingi ya hukumu za Kimungu huwa hazitekelezeki kwa kwa timeframe ya kibinadamu katika time limit yetu, ila katika timeframe ya kiroho.

Ni kweli kabisa kuwa siku Adamu alipokula tunda alikufa, lakini kifo kile kilikuwa ni cha kiroho, kilikuja kudhihirika mwilini baadaye kabisa, na ndio maana Biblia inasema "Mlikuwa wafu kwa sababu ya dhambi na makosa yenu".
Kwa hiyo mtu anapotenda dhambi anakuwa mfu pale pale kiroho, Japo anakuwa anatembea na maisha yake yananawiri kama kawaida.

Mfano mzuri ni antivirus ya computer, ukiikatisha kuingia mtandaoni kuji-update inakuwa imekufa maana umeiblock kuingia kwenye source ya life yake, haifanyi kazi, ila kwenye computer itaendelea kuwepo japo haitakuwa inakamata virus.

Kwa hiyo si kwamba Adam siku alipotenda dhambi roho ilichomoka akabaki na nafsi na mwili, ila ni kweli kiroho alikufa.
Na kifo cha kiroho haina maana ya kuzimika kiroho na kukakamaa, hapana.
Kumbuka hata Jehunum ya moto Mungu anaiita kifo cha pili.
Ni kweli watu wataendelea kupumua na kuwa hai, lakini kiroho ile ni mauti.

Nikupenyezee ubuyu tu kuwa Adamu tangu amekufa mpaka wakati Yesu anakufa, hakuna mtu aiyewahi kwenda mbinguni, wote waliishia kuzimu, ni mpaka Yesu alipotoa ruhusa ya nani aende na ani abaki, maana yeye ndiye aliyeishinda mauti.

Na kweli mara baada ya kufa tu msalabani, alishuka huko chini kufanya kazi part tu, ambayo ni kuzihubiria roho za wafu na zilizomkubali zikapata kibali cha kuondoka naye.

Ni kama Yesu aliposema kuwa tubuni kwa kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia, watu wakajua kiama kimekaribia, lakini mpaka leo miaka buku mbili imepita bado tunadunda.
 
Mungu hakusema (instantly )or (immeadiately) mtakufa amesema " you shall surely die"

[emoji115] [emoji115] [emoji115]

Hivyo ni kweli walikufa, ile ahadi ya kuishi milele ikaondoka,

Ndio maana ya hakika utakufa. Hii "uta" ni wakati ujao na wakafa baada ya miaka mingi adhabu ya Mungu ikatekelezeka.
 
Kingine katika summary yako

Adamu hakufa hapo hapo

Adamu alipoteza nafasi(position) ambayo Mungu alimpa alipoteza nafasi ya kuwasiliana na Mungu sababu ya dhambi aliyo itenda

Baada ya kupoteza nafasi ndipo adhabu na laana ikatolewa kutolewa nje ya bustani, kuzaa kwa uchungu, ardhi ikalaaniwa.

Ambayo hii nafasi imekuja kurudishwa na Adamu wa mwisho ambaye ni Yesu
 
Hivi tunaposema ``mwili wa fulani`` huyu fulani tunayemrefer ni nafsi au roho?
 
Mungu hakusema (instantly )or (immeadiately) mtakufa amesema " you shall surely die"

emoji115.png
emoji115.png
emoji115.png


Hivyo ni kweli walikufa, ile ahadi ya kuishi milele ikaondoka,

Ndio maana ya hakika utakufa. Hii "uta" ni wakati ujao na wakafa baada ya miaka mingi adhabu ya Mungu ikatekelezeka.


Kwahiyo Adam aliendelea kuwa na mwili, nafsi na roho hata baada ya adhabu kutolewa na Mungu?
 
Kwahiyo Adam aliendelea kuwa na mwili, nafsi na roho hata baada ya adhabu kutolewa na Mungu?
Alikuwa nazo zote, roho, nafsi na mwili

Ndio maana ukisoma vizur mwanzo sura ya 3 utaona

Laana iliyo tolewa kwa nyoka na laana pamoja na adhabu aliyo pewa Adamu

Adamu (ambaye ni msaidizi naye alipata adhabu yake)

Mwisho wa adhabu ndio inakamilika kuwa hakika utakufa na mwishoni wakafa baada ya miaka kupita

Kutolewa tu nje ya bustani ilikuwa adhabu tosha kwao, hawkuzoea kulima, hawakutakiwa kula kwa jasho, haikutakiwa kuzaa kwa uchungu
Ndani ya ile hakika mtakufa ndani yake kumebeba adhabu hiyo

Mauti ni pigo la mwisho.
 
Hivi tunaposema ``mwili wa fulani`` huyu fulani tunayemrefer ni nafsi au roho?
Mwili umewekwa tayar kubeba nafsi na roho

Mwili ni kibebeo tu

Nataka niwaze kwa upana, walipo kula hilo tunda la mti wa ujuz wa mema na mabaya

Nawaza hivi kwanini walijiona uchi?
Kwan mwanzo hawakuwa uchi?
Ina maana kuna vazi ambalo Mungu aliwaficha nalo liliondoka muda ule

Ni kama mtu aliyefunikwa baadaye akaondolewa ktk mfuniko huo ndio akajua yupo uchi
Na hicho ndicho kitu shetan alitaka akipate

Asingeweza kuwagusa katika lile vazi ambalo Mungu aliwavisha na shetan asingeweza kuwadhuru hadi wawe uchi

Kama wakiwa hawana nguo ndio ilimpa shetan uhalali wa kuwagusa sasa
Ndio maana Mungu akaamua kutekeleza adhabu aliyo waambia kuwa hakika mtakufa

Nawaza katika Roho kuwa
Kuna uwepo ambao Mungu aliwafunika nao kias kwamba alikuwa na uwezo wa kuja jioni kuwatembelea

Kuwa kwao uchi walipoteza kibali, nafasi na nguo ambayo Mungu aliwapa
Nawaza kuwa lilikuwa vazi special ktk Roho
Vazi ambalo ukilipoteza kulipata ni gharama kubwa sana kuirudisha

Ndio maana utakuja kukuta Yesu alikufa ili atukomboe

Mtu kufa kwaajil ya wengi nawaza ni kipi Adamu alichopoteza Eden hadi Mungu kuamua kumachilia mtoto wa pekee afe

Kilikuwa kitu kikubwa mno, ulinzi mkubwa mno, tena cha thamani ambacho kinacost Damu imwagike

Hivyo Adamu alibak na mwil nafsi na roho alichopoteza ni kitu kama hicho juu

Ushirika na Mungu uliondoka, uhusiano na Mungu ulipotea, urafiki na Mungu ulipotea

Yesu atupe kujua thamani Yetu rohoni
Amen
 
Mungu hakusema (instantly )or (immeadiately) mtakufa amesema " you shall surely die"

emoji115.png
emoji115.png
emoji115.png


Hivyo ni kweli walikufa, ile ahadi ya kuishi milele ikaondoka,

Ndio maana ya hakika utakufa. Hii "uta" ni wakati ujao na wakafa baada ya miaka mingi adhabu ya Mungu ikatekelezeka.


Kwahiyo Adam aliendelea kuwa na mwili, nafsi na roho hata baada ya adhabu kutolewa na Munhu
Mwili umewekwa tayar kubeba nafsi na roho

Mwili ni kibebeo tu

Nataka niwaze kwa upana, walipo kula hilo tunda la mti wa ujuz wa mema na mabaya

Nawaza hivi kwanini walijiona uchi?
Kwan mwanzo hawakuwa uchi?
Ina maana kuna vazi ambalo Mungu aliwaficha nalo liliondoka muda ule

Ni kama mtu aliyefunikwa baadaye akaondolewa ktk mfuniko huo ndio akajua yupo uchi
Na hicho ndicho kitu shetan alitaka akipate

Asingeweza kuwagusa katika lile vazi ambalo Mungu aliwavisha na shetan asingeweza kuwadhuru hadi wawe uchi

Kama wakiwa hawana nguo ndio ilimpa shetan uhalali wa kuwagusa sasa
Ndio maana Mungu akaamua kutekeleza adhabu aliyo waambia kuwa hakika mtakufa

Nawaza katika Roho kuwa
Kuna uwepo ambao Mungu aliwafunika nao kias kwamba alikuwa na uwezo wa kuja jioni kuwatembelea

Kuwa kwao uchi walipoteza kibali, nafasi na nguo ambayo Mungu aliwapa
Nawaza kuwa lilikuwa vazi special ktk Roho
Vazi ambalo ukilipoteza kulipata ni gharama kubwa sana kuirudisha

Ndio maana utakuja kukuta Yesu alikufa ili atukomboe

Mtu kufa kwaajil ya wengi nawaza ni kipi Adamu alichopoteza Eden hadi Mungu kuamua kumachilia mtoto wa pekee afe

Kilikuwa kitu kikubwa mno, ulinzi mkubwa mno, tena cha thamani ambacho kinacost Damu imwagike

Hivyo Adamu alibak na mwil nafsi na roho alichopoteza ni kitu kama hicho juu

Ushirika na Mungu uliondoka, uhusiano na Mungu ulipotea, urafiki na Mungu ulipotea

Yesu atupe kujua thamani Yetu rohoni
Amen


Shukran sana kwa ufafanuzi huu.
 
Back
Top Bottom