Nakumbuka nimeshawahi kuandika kuhusu hili jambo kwa urefu sana japokuwa si hapa jamiiforums, nilijikita kueleza uhusiano wa mwili na roho katika utendaji wake katika mwanadamu. Lakini hapa nimeona kuna kitu kimeongezeka, “nafsi”. Kuhusiana na neno nafsi tangu awali na hata sasa hivi nimejaribu kupitia ili kujiridhisha zaidi kutoka kwa waandishi wengi na hata kwenye biblia pia, wameileza nafsi kama mwili, kiumbe kilicho hai. Kwa hiyo kwangu mimi nafsi=mwili. Kwa hiyo kwa mantiki hiyo, vitu vinavyomjenga mwanadamu ni mwili(nafsi) na roho.
Vitu vinavyomjenga mwanadamu ni MWILI na ROHO. Tunaweza kuuchukulia muunganiko huu wa mwili na roho uzaao mwanadamu kama vile kompyuta ifanyavyo kazi. Kompyuta ili iwe kompyuta (ifanye kazi) ni lazima kuwe na muunganiko wa vitu viwili nanvyo ni hardware (umbo lionekanalo nje kama vile kioo, motherboard na vingine vingi) pamoja na software (m(i)fumo endeshi ambayo kikawaida haionekani kwa macho). Muunganiko wa software na hardware ndio huwezesha kompyuta kufanya kazi na kukosekana kwa kimoja wapo hufanya kompyuta isiweze kufanya kazi. Uwepo wa mwili na roho ndivyo unaomtengeneza mwanadamu. Kukosekana kwa kitu kimoja kati ya hiki mtu hukosa sifa ya kuwa mwanadamu. Ufanyaji kazi kwa kushirikiana kati ya mwili na roho ndivyo huzaa utendaji kazi wa aina yoyote ile tunaouona katika macho ya kawaida ya kibinadamu. Sasa tuanze kukiangalia kimoja baada ya kingine.
1: ROHO NI NINI
Roho ni umbo lisiloonekana kwa macho ya kawaida ya kibinadaumu(ni kama software kwenye kompyuta). Ni umbo linalobeba utambuzi yakini ambao hufanya kazi ndani mwili katika kumuongoza mwanadamu. Ninaposema utambuzi yakini namaanisha uwezo wa kudhibiti na kuratibu ni kipi cha kufanya na ni kipi si cha kufanya kwa muda husika. Kwa maana hiyo roho zote ni zenye kufanana na zote zina sifa sawa. Lakini utambuzi yakini hauwezi kufanyika kama roho haijawahi kuingia katika mwili wa mwanadamu. Hii ina maana kuwa roho yenyewe haiwezi kufanya kitu chochote chenye kuweza kuleta matokeo yenye kuonekana kiroho au kimwili mpaka iwe ndani ya mwili wa mwanadamu au iwe iliwahi kukaa ndani ya mwili wa binadamu kwa kipindi Fulani japokuwa pia haiwezi kufanya hayo kwa utashi wale pekeyake bali kama kuna mtu anayeiongoza kufanya hayo kwa kutumia nguvu iliyo nje ya uwezo wa kibinadamu.
KABLA YA KUINGIA NDANI YA MWILI, ROHO HUKAA WAPI?
Hili ni swali ambalo majibu yake hayawezi kupatikana kirahisi na hata kama yakipatikana hayawezi kuwa yenye kuaminika. Lakini tunaweza kujibu hili swali kwa kutumia mawazo makuu ya zile nadharia kuu mbili zinazielezea mwanzo wa maisha. Nazo ni; ile inayoeleza kuwa maisha yalijitokeza yenyewe kwa nasibu na ile inayoeleza kuwa maisha yalitokana na uumbaji wa Mungu.
Kwa wale wanaoamini maisha yalijitokeza yenyewe majibu yao majibu yao yanaweza kuwa rahisi na yenye kushangaza hata kutia shaka sana. Ni kwamba kabla ya kuingia katika mwili wa binadamu roho haikuwa mahala popote pale. Kwa maana rahisi ni kuwa roho haiajawahi kuwepo mahala popote pale kwa hiyo roho ni kitu cha kinadharia, HAKIPO.
Kwa wale wanaoamini uwepo wa mungu(nikiwemo mimi) wanaamini kuwa roho zote ni zao la uumbaji wa Mungu. Kwa maana hiyo ni kwamba roho hutoka kwa Mungu. Na katika nadharia hii, kwa kuwa Mungu ndiye muumbaji wa roho zote na ni yeye anayezipa kazi ya kufanya katika miili ambayo ameamuru ziingie.
2 MWILI NI NINI
Mwili ni umbo lenye kuonekana kwa macho ya kawaida ya kibinadamu(ni kama hardware kwenye kompyuta). Mwili ni zao la muunganiko wa kibaiolojia kati ya mbegu ya kiume na ya kike kupitia tendo la ndoa (japokuwa siku hizi muunganiko huu si lazima utokee wakati wa tendo la ndoa, hii haibadili maana. Muunganiko ni muunganiko tu). Katika muunganiko huu, mwili huu mpya unaotengenezwa hubeba sifa za moja za upande wa watu waliohusika ama upande mmoja pekee. Mwili ni ambao hasa hufanya utendaji wa mambo mengi yanayoonekana kwa kuwa unabeba ‘sifa pambanuzi’ ambazo ni muonekano(weupe, weusi urefu, ufupi nk..) na hisia(kupenda, kuchukua, kukasirika, kufurahi, kuhuzunika nk..). sifa pambanuzi hubebwa kwenye vinasaba na ndiyo maana waweza kusikia watu wakisema “Yule mtoto ana hasira kama baba yake”, au “Yule binti ni mrembo kama mama yake”. Hii na kwa sababu sifa pambanuzi hubebwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kupitia vinasaba.
BINADAMU NI NINI(NANI)
Binadamu ni muunganiko wa mwili na roho. Vyote hivi vikiungana kwa pamoja ndipo tokeo lake huitwa mwanadamu. Kwa maana hiyo ni muunganiko wa umbo linaloonekana na umbo lisiloonekana. Utendaji wa mwanadamu unategemea ushirikiano wa hali wa juu kabisa kati ya mwili na roho. Kazi ya roho ni kuhakikisha mwili unatenda kuendana na matakwa yake (matakwa ya kiroho au matakwa aliyeiumba roho). kwa nini ninasema kutokana na matakwa ya…… ni kwa sababu, mwanzo nimesema kuwa roho zote ziko sawa kwa kuwa muumbaji wake ni mmoja(kama yupo, lakini kwa imani yangu naamini kuwa yupo). Na kazi kazi ya roho ni kudhibiti utedaji wa mwili kwa kuzuia matendo mabaya na kuruhusu matendo mazuri juu ya mwili. Sasa kwa mfano roho ikauingia mwili wenye tabia za hasira na majivuno (nimeshasema kuwa tabia hurithiwa kutoka kizazi na kizazi kwa kupitia vinasaba), kwa hiyo roho inatakiwa kudhibiti tabia ya hasira na majivuno yaliyo katika mwili huo. Na roho ikifanikiwa kudhibiti tabia hizo hapo inahesabika kuwa roho imeweza kutimiza jukumu lake na kama ikawa kinyume chake hapo inachukuliwa kuwa roho imeshindwa kutimiza jukumu lake.
MWILI NA ROHO HUUNGANA WAKATI GANI?
Hapo zamani iliaminika kuwa roho ilikuwa inaingia ndani ya mwili wa mwanadamu punde mtoto anapozaliwa. Na watu waliokuwa wakiamini hivi walitumia ushahidi wa kilio cha mtoto pale anapozaliwa. Kwamba kilio kile ndo kinatambulisha kuwa sasa roho imeingia ndani ya mwili wa mtoto huyo na hii ikiwa na maana kuwa kabla ya hapo mtoto huyu alikuwa na mwili pekee. Wazo hili lilichangia sana vitendo vya utoaji mimba kwa kuwa waliamini kuwa ukitoa mimba hakuna roho inayotolewa kwenye mwili, kwa hiyo hakuna mauaji. Dhana hii ilikuja kukosolewa na wasayansi walipokuja na ushahidi wa sababu yakini zinazoeleza sababu halisi za ni kwa nini mtoto hulia wakati anazaliwa ambazo ni
totauti ya jotoridi katika mji wa uzazi na mazingira ya nje hii humfanya ahisi mabadiliko Fulani na hivyo kulia ni rection yake baada ya kutambua mabadiliko
(ii) kwa kuwa mtoto akiwa tumboni hakuna hewa inayokuwa inaingia mapafuni hivyo mapafu huwa yamesinyaa, kwa hiyo anapozaliwa hewa huingia kwa mara ya kwanza katika mapafu hivyo mapafu hutanuka kwa ghafla na kusababisha maumivu kwa kichanga na kukifanya kilie.
Pia mikwaruzo wakati anatoka katika mji wa muzazi husababisha maimivu hivyo kumfanya alie.
Kwa hiyo, dhana inayokubalika kueleza ni wakati gani mwili na roho huungana ni pale tu mbegu ya kiume naya kike zinapoungana, ndipo roho huingia ndani ya mwili. Na kuanzia muda huo kila kimoja huanza kuwajibika juu ya kingine.
Na ili roho iweze kuingia ndani ya mwili na lizima mwili uwe katika hali ya kukamilika kibailojia katika namna inayoweza kuufanya mwili uwe hai. Ni lazima kuwe na seli hai.
Kwa hiyo hata kwenye kesi ya adam, Mungu alipomuumba adam alimuumba kwa udongo kwa hiyo hiyo kabla ya kupuziliwa pumzi ya uhai adam alikuwa ni donde la udongo lisilo na uhai. Na alipopuliziwa pumzi ya uhai ndipo adam akawa hai. Kwa hiyo mimi naamini kuwa pumzi ya uhai iliupa mwili seli hai na papo hapo roho iliingia kwa adam kwa sababu binadamu ili awe binadamu, muunganiko wa mwili na roho unatakiwa utokee katika wakati mmoja na si kimoja kianze na kingine kikikute kingine.
Huo ndio mtazamo wangu, nakaribisha wengine ili tuzidi kujifunza.
Shukran mkuu
Internal