Body(mwili), soul(nafsi) and spirit(roho)

Body(mwili), soul(nafsi) and spirit(roho)

Kwahiyo Adam aliendelea kuwa na mwili, nafsi na roho hata baada ya adhabu kutolewa na Mungu?
Alikuwa nazo zote, roho, nafsi na mwili

Ndio maana ukisoma vizur mwanzo sura ya 3 utaona

Laana iliyo tolewa kwa nyoka na laana pamoja na adhabu aliyo pewa Adamu

Adamu (ambaye ni msaidizi naye alipata adhabu yake)

Mwisho wa adhabu ndio inakamilika kuwa hakika utakufa na mwishoni wakafa baada ya miaka kupita

Kutolewa tu nje ya bustani ilikuwa adhabu tosha kwao, hawkuzoea kulima, hawakutakiwa kula kwa jasho, haikutakiwa kuzaa kwa uchungu
Ndani ya ile hakika mtakufa ndani yake kumebeba adhabu hiyo

Mauti ni pigo la mwisho.
Mwili umewekwa tayar kubeba nafsi na roho

Mwili ni kibebeo tu

Nataka niwaze kwa upana, walipo kula hilo tunda la mti wa ujuz wa mema na mabaya

Nawaza hivi kwanini walijiona uchi?
Kwan mwanzo hawakuwa uchi?
Ina maana kuna vazi ambalo Mungu aliwaficha nalo liliondoka muda ule

Ni kama mtu aliyefunikwa baadaye akaondolewa ktk mfuniko huo ndio akajua yupo uchi
Na hicho ndicho kitu shetan alitaka akipate

Asingeweza kuwagusa katika lile vazi ambalo Mungu aliwavisha na shetan asingeweza kuwadhuru hadi wawe uchi

Kama wakiwa hawana nguo ndio ilimpa shetan uhalali wa kuwagusa sasa
Ndio maana Mungu akaamua kutekeleza adhabu aliyo waambia kuwa hakika mtakufa

Nawaza katika Roho kuwa
Kuna uwepo ambao Mungu aliwafunika nao kias kwamba alikuwa na uwezo wa kuja jioni kuwatembelea

Kuwa kwao uchi walipoteza kibali, nafasi na nguo ambayo Mungu aliwapa
Nawaza kuwa lilikuwa vazi special ktk Roho
Vazi ambalo ukilipoteza kulipata ni gharama kubwa sana kuirudisha

Ndio maana utakuja kukuta Yesu alikufa ili atukomboe

Mtu kufa kwaajil ya wengi nawaza ni kipi Adamu alichopoteza Eden hadi Mungu kuamua kumachilia mtoto wa pekee afe

Kilikuwa kitu kikubwa mno, ulinzi mkubwa mno, tena cha thamani ambacho kinacost Damu imwagike

Hivyo Adamu alibak na mwil nafsi na roho alichopoteza ni kitu kama hicho juu

Ushirika na Mungu uliondoka, uhusiano na Mungu ulipotea, urafiki na Mungu ulipotea

Yesu atupe kujua thamani Yetu rohoni
Amen
Shukrani Sana wadau kwa hoja zenu mnanifanya nizid kugain vitu ambavyo nivyamsingi sana kuvijua.

Naanza na hoja ya kuwa je adam baada ya kula tunda alibaki kuwa na mwili, nafsi na roho au mwili na nafsi pekee ??

Divine: maelezo yako hapo juu nimeyaelewa sana na siitaji kutia neno tena apo maana umeeleza hata zaidi ya nilivyokuwa nawaza mimi.

Adam alibakia kuwa na sifa mbili tu ! Nazo ni mwili na nafsi(kuna uzi nitaweka chini hapo kuelezea zaidi hili navyofahamu ila hapa najibh kwa ufupi tu).

Tusome haya maandiko yatatusaidia kuelewa zaidi

Thessalonians 5:23 says:

“Now may the God of peace Himself sanctify you completely; and may your whole spirit, soul, and bodybe preserved blameless at the coming of our Lord Jesus Christ.”
(23 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.)

Kulingana aya hii, inaonyesha wazi kuwa hatuko kamili yaani kuna kitu kimepungua kwetu, viko vitatu amejaribu kuviorodhesha hapo. Mwili, nafsi na roho.

Wote tunakubaliana kuwa mwili ni kibebeo cha nafsi na roho, sasa swali la kujiuliza ni kipi ambacho hakijakamilika kinachoelezwa hapo ? Je ni nafsi au Roho ?
Mwanzoni nilieleza kwa mafungu kuwa mwili hauwezi kuwa hai bila nafsi hivyo nafsi ndiyo inayoupatia mwili uhai. Kwa maelezo haya tunaona kuwa hatuko kamili kwa kukosa sifa ya tatu yaani roho(spirit).

John 3:1-6
"There was a man of the Pharisees named Nicodemus, a ruler of the Jews. This man came to Jesus by night and said to him, "Rabbi, we know that you are a teacher come from God; for no one can do these signs that you do unless God is with him." Jesus answered and said to him, "Most assuredly, I say unto you, unless one is born again [the Greek text reads "born from above"], he cannot see the kingdom of God."
(1 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi.
2 Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye.
3 Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili,........


Baada ya adamu kula tunda ni wazi kuwa alikufa maana alipoteza form of life ya spirit(ukiroho), hivyo akawa mfu mbele za Mungu, hapa kristo anasema ili tuingie kwenye ufalme wa mbinguni au ili tuonane na Mungu ni lazima tuzaliwe tena mara ya pili. Tuzaliwe ndio maana hatupo, kinachozaliwa ni kana kwamba hakikuwepo hivyo kinazaliwa ili kiwepo. Na sisi ni kana kwamba hatupo maana hatuna sifa ya ukiroho ambayo ndio image of God.

Questions may come immediately to our minds: "How does this birth occur?"
birth?", "what do I receive from this birth?".

John 3:4-5
"Nicodemus said to him, "How can a man be born when he is old? Can he enter a second time into his mother’s womb and be born? Jesus answered, "Most assuredly, I say to you, unless one is born of water and of the Spirit, he cannot enter the kingdom of God."
(4 Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?
5 Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho,.......)

In this passage Jesus Christ explains us that for a man to enter the kingdom of God he should be born of water and of the spirit. To be born of water means the first birth. Without having been born once, how could you be born again? He tells us also that one should be born of the spirit.

John 3:6
"That which is born of the flesh is flesh, and that which is born of the Spirit is spirit."
(6 Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.)

Again the two births are put together in the same sentence but this time the purpose is to contrast them and to show that they are entirely different. From the first birth you received what your parents are i.e. flesh. Similarly, from the second birth you received what your parent, God, is i.e. spirit

Karibuni tena tuendelee na mada.
 
Hivi inakuwaje Biblia na Msaafu tu ndio kiwe kimomo cha uthibitisho wa uwepo wa Roho na Mungu? Binafsi uzi huu tangu mwanzo nilipoupitia naona ni blah blah tuu...
Kiranga Njoo umchukue ndugu yako uku.
 
Uzi mzuri. Japo nimesoma kwa kuscan.

Tuanzie kwenye uliyoyasema kwenye uzi wako. Hivyo ili kugupisha, "kusummarise" sitarefer qoutes maana ushazionyesha na mimi nazitudia tu.

Kwenye hadithi ya piliya uumbaji( hadithi ambayo binadamu kaubwa kwa udongo). Hadithi imetanabaisha jinsi binadamu alivyo asili ya ardhi(mwili) na Mungu(roho).


Mungu akamfinyanga binafamu kwa vumbi la nchi, kisha akampulizia pumzi yake puani. Na binadamu akawa nafsi hai.

Binadamu alimbwa kwa udongo. Japo haielezewa kwenye biblia. Ila binadamu alimbwa kwa udongo akawa kiumbe hai.

Hivyo baada tu ya kufinyangwa kwa udongo, tayari alikua na nafsi.

Hata hivyo hakua na roho.

Ama kwa maana nyingine nafsi yake haikua hai.

Ila baada ya kupuliziwa Pumzi ya Mungu. Nafsi yale ilihuishwa.

Hivyo kiroho, nafsi ya binadamu ni zao la "reaction kati ya pumzi ya Mungu(roho) na mwili wa binadamu.

Hivyo ndan yetu binadamu, mna roho ya Mungu ilipaswa na inapaswa iwe hivyo.

Pia ndani mwetu mna roho zetu. Roho zetu zi hai. Pale tu ambapo roho ya Mungu i ndani mwetu.

Mda roho ya Mungu inatoka ndani mwetu. Roho zetu zimekufa. Ni hadi zitakapo huishwa tena kwa Roho wa Mungu kurudi ndani mwetu, ndipo zinapo pata na kufanya kazi inavyo paswa.

Binadamu alimbwa kwa udongo. Japo haielezewa kwenye biblia. Ila binadamu alimbwa kwa udongo akawa kiumbe hai.
Jibu:
Mwanzo 2:7 7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
Hivyo baada tu ya kufinyangwa kwa udongo, tayari alikua na nafsi.
[emoji404] Jibu:
Mwanzo 7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]

Hata hivyo hakua na roho.
[emoji404] Jibu:
John 4:24 tells us:
"God is Spirit"
Genesis 1:27 So God created man in his own image, in the image of God created he him; male and female created he them.

Adam alikuwa na hali zote tatu, mwili, nafsi na roho. Hii ni kwasabu Mungu aliamua kumpatia sifa ya roho kusudi waweze kuwasiliana kwa urahisi. Kumbuka aliumbwa kwa image of God na Mungu ni roho ilikuwa lazima adam naye awe na sifa hio ya ukiroho maana nfiyo iliokuwa image of God yaani ndiyo ilikuwa muonekano wa Mungu.
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]

Ama kwa maana nyingine nafsi yake haikua hai.

[emoji404] Jibu: kwenye mada kuu nimejaribu kueleza kuwa mwili umeumbwa kwa mavumbi ya ardhi tukaina kuwa kilichoumbwa kwa mavumbi ya udongo ni mwili(Body/flesh). The Mungu akapuliza pumzi yake kwenye pua za huo mwili kisha mtu akawa nafsi hai, hivyo nikasema kinachoupa mwili uhai ni nafsi ambayo hutokana na pumzi ya Mungu. Mwili bila nafsi ni mfu au si kitu.
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]
Hivyo kiroho, nafsi ya binadamu ni zao la "reaction kati ya pumzi ya Mungu(roho) na mwili wa binadamu.

[emoji404] Asante sana.
[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]

Hivyo ndan yetu binadamu, mna roho ya Mungu ilipaswa na inapaswa iwe hivyo.

Pia ndani mwetu mna roho zetu. Roho zetu zi hai. Pale tu ambapo roho ya Mungu i ndani mwetu.

Mda roho ya Mungu inatoka ndani mwetu. Roho zetu zimekufa. Ni hadi zitakapo huishwa tena kwa Roho wa Mungu kurudi ndani mwetu, ndipo zinapo pata na kufanya kazi inavyo paswa.[/

[emoji404] Naomba hili nisieleze hapa, nitaandaa uzi wa muendelezo
 
Nakumbuka nimeshawahi kuandika kuhusu hili jambo kwa urefu sana japokuwa si hapa jamiiforums, nilijikita kueleza uhusiano wa mwili na roho katika utendaji wake katika mwanadamu. Lakini hapa nimeona kuna kitu kimeongezeka, “nafsi”. Kuhusiana na neno nafsi tangu awali na hata sasa hivi nimejaribu kupitia ili kujiridhisha zaidi kutoka kwa waandishi wengi na hata kwenye biblia pia, wameileza nafsi kama mwili, kiumbe kilicho hai. Kwa hiyo kwangu mimi nafsi=mwili. Kwa hiyo kwa mantiki hiyo, vitu vinavyomjenga mwanadamu ni mwili(nafsi) na roho.

Vitu vinavyomjenga mwanadamu ni MWILI na ROHO. Tunaweza kuuchukulia muunganiko huu wa mwili na roho uzaao mwanadamu kama vile kompyuta ifanyavyo kazi. Kompyuta ili iwe kompyuta (ifanye kazi) ni lazima kuwe na muunganiko wa vitu viwili nanvyo ni hardware (umbo lionekanalo nje kama vile kioo, motherboard na vingine vingi) pamoja na software (m(i)fumo endeshi ambayo kikawaida haionekani kwa macho). Muunganiko wa software na hardware ndio huwezesha kompyuta kufanya kazi na kukosekana kwa kimoja wapo hufanya kompyuta isiweze kufanya kazi. Uwepo wa mwili na roho ndivyo unaomtengeneza mwanadamu. Kukosekana kwa kitu kimoja kati ya hiki mtu hukosa sifa ya kuwa mwanadamu. Ufanyaji kazi kwa kushirikiana kati ya mwili na roho ndivyo huzaa utendaji kazi wa aina yoyote ile tunaouona katika macho ya kawaida ya kibinadamu. Sasa tuanze kukiangalia kimoja baada ya kingine.

1: ROHO NI NINI
Roho ni umbo lisiloonekana kwa macho ya kawaida ya kibinadaumu(ni kama software kwenye kompyuta). Ni umbo linalobeba utambuzi yakini ambao hufanya kazi ndani mwili katika kumuongoza mwanadamu. Ninaposema utambuzi yakini namaanisha uwezo wa kudhibiti na kuratibu ni kipi cha kufanya na ni kipi si cha kufanya kwa muda husika. Kwa maana hiyo roho zote ni zenye kufanana na zote zina sifa sawa. Lakini utambuzi yakini hauwezi kufanyika kama roho haijawahi kuingia katika mwili wa mwanadamu. Hii ina maana kuwa roho yenyewe haiwezi kufanya kitu chochote chenye kuweza kuleta matokeo yenye kuonekana kiroho au kimwili mpaka iwe ndani ya mwili wa mwanadamu au iwe iliwahi kukaa ndani ya mwili wa binadamu kwa kipindi Fulani japokuwa pia haiwezi kufanya hayo kwa utashi wale pekeyake bali kama kuna mtu anayeiongoza kufanya hayo kwa kutumia nguvu iliyo nje ya uwezo wa kibinadamu.

KABLA YA KUINGIA NDANI YA MWILI, ROHO HUKAA WAPI?
Hili ni swali ambalo majibu yake hayawezi kupatikana kirahisi na hata kama yakipatikana hayawezi kuwa yenye kuaminika. Lakini tunaweza kujibu hili swali kwa kutumia mawazo makuu ya zile nadharia kuu mbili zinazielezea mwanzo wa maisha. Nazo ni; ile inayoeleza kuwa maisha yalijitokeza yenyewe kwa nasibu na ile inayoeleza kuwa maisha yalitokana na uumbaji wa Mungu.

Kwa wale wanaoamini maisha yalijitokeza yenyewe majibu yao majibu yao yanaweza kuwa rahisi na yenye kushangaza hata kutia shaka sana. Ni kwamba kabla ya kuingia katika mwili wa binadamu roho haikuwa mahala popote pale. Kwa maana rahisi ni kuwa roho haiajawahi kuwepo mahala popote pale kwa hiyo roho ni kitu cha kinadharia, HAKIPO.

Kwa wale wanaoamini uwepo wa mungu(nikiwemo mimi) wanaamini kuwa roho zote ni zao la uumbaji wa Mungu. Kwa maana hiyo ni kwamba roho hutoka kwa Mungu. Na katika nadharia hii, kwa kuwa Mungu ndiye muumbaji wa roho zote na ni yeye anayezipa kazi ya kufanya katika miili ambayo ameamuru ziingie.

2 MWILI NI NINI
Mwili ni umbo lenye kuonekana kwa macho ya kawaida ya kibinadamu(ni kama hardware kwenye kompyuta). Mwili ni zao la muunganiko wa kibaiolojia kati ya mbegu ya kiume na ya kike kupitia tendo la ndoa (japokuwa siku hizi muunganiko huu si lazima utokee wakati wa tendo la ndoa, hii haibadili maana. Muunganiko ni muunganiko tu). Katika muunganiko huu, mwili huu mpya unaotengenezwa hubeba sifa za moja za upande wa watu waliohusika ama upande mmoja pekee. Mwili ni ambao hasa hufanya utendaji wa mambo mengi yanayoonekana kwa kuwa unabeba ‘sifa pambanuzi’ ambazo ni muonekano(weupe, weusi urefu, ufupi nk..) na hisia(kupenda, kuchukua, kukasirika, kufurahi, kuhuzunika nk..). sifa pambanuzi hubebwa kwenye vinasaba na ndiyo maana waweza kusikia watu wakisema “Yule mtoto ana hasira kama baba yake”, au “Yule binti ni mrembo kama mama yake”. Hii na kwa sababu sifa pambanuzi hubebwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kupitia vinasaba.

BINADAMU NI NINI(NANI)
Binadamu ni muunganiko wa mwili na roho. Vyote hivi vikiungana kwa pamoja ndipo tokeo lake huitwa mwanadamu. Kwa maana hiyo ni muunganiko wa umbo linaloonekana na umbo lisiloonekana. Utendaji wa mwanadamu unategemea ushirikiano wa hali wa juu kabisa kati ya mwili na roho. Kazi ya roho ni kuhakikisha mwili unatenda kuendana na matakwa yake (matakwa ya kiroho au matakwa aliyeiumba roho). kwa nini ninasema kutokana na matakwa ya…… ni kwa sababu, mwanzo nimesema kuwa roho zote ziko sawa kwa kuwa muumbaji wake ni mmoja(kama yupo, lakini kwa imani yangu naamini kuwa yupo). Na kazi kazi ya roho ni kudhibiti utedaji wa mwili kwa kuzuia matendo mabaya na kuruhusu matendo mazuri juu ya mwili. Sasa kwa mfano roho ikauingia mwili wenye tabia za hasira na majivuno (nimeshasema kuwa tabia hurithiwa kutoka kizazi na kizazi kwa kupitia vinasaba), kwa hiyo roho inatakiwa kudhibiti tabia ya hasira na majivuno yaliyo katika mwili huo. Na roho ikifanikiwa kudhibiti tabia hizo hapo inahesabika kuwa roho imeweza kutimiza jukumu lake na kama ikawa kinyume chake hapo inachukuliwa kuwa roho imeshindwa kutimiza jukumu lake.

MWILI NA ROHO HUUNGANA WAKATI GANI?
Hapo zamani iliaminika kuwa roho ilikuwa inaingia ndani ya mwili wa mwanadamu punde mtoto anapozaliwa. Na watu waliokuwa wakiamini hivi walitumia ushahidi wa kilio cha mtoto pale anapozaliwa. Kwamba kilio kile ndo kinatambulisha kuwa sasa roho imeingia ndani ya mwili wa mtoto huyo na hii ikiwa na maana kuwa kabla ya hapo mtoto huyu alikuwa na mwili pekee. Wazo hili lilichangia sana vitendo vya utoaji mimba kwa kuwa waliamini kuwa ukitoa mimba hakuna roho inayotolewa kwenye mwili, kwa hiyo hakuna mauaji. Dhana hii ilikuja kukosolewa na wasayansi walipokuja na ushahidi wa sababu yakini zinazoeleza sababu halisi za ni kwa nini mtoto hulia wakati anazaliwa ambazo ni
totauti ya jotoridi katika mji wa uzazi na mazingira ya nje hii humfanya ahisi mabadiliko Fulani na hivyo kulia ni rection yake baada ya kutambua mabadiliko
(ii) kwa kuwa mtoto akiwa tumboni hakuna hewa inayokuwa inaingia mapafuni hivyo mapafu huwa yamesinyaa, kwa hiyo anapozaliwa hewa huingia kwa mara ya kwanza katika mapafu hivyo mapafu hutanuka kwa ghafla na kusababisha maumivu kwa kichanga na kukifanya kilie.
Pia mikwaruzo wakati anatoka katika mji wa muzazi husababisha maimivu hivyo kumfanya alie.
Kwa hiyo, dhana inayokubalika kueleza ni wakati gani mwili na roho huungana ni pale tu mbegu ya kiume naya kike zinapoungana, ndipo roho huingia ndani ya mwili. Na kuanzia muda huo kila kimoja huanza kuwajibika juu ya kingine.
Na ili roho iweze kuingia ndani ya mwili na lizima mwili uwe katika hali ya kukamilika kibailojia katika namna inayoweza kuufanya mwili uwe hai. Ni lazima kuwe na seli hai.
Kwa hiyo hata kwenye kesi ya adam, Mungu alipomuumba adam alimuumba kwa udongo kwa hiyo hiyo kabla ya kupuziliwa pumzi ya uhai adam alikuwa ni donde la udongo lisilo na uhai. Na alipopuliziwa pumzi ya uhai ndipo adam akawa hai. Kwa hiyo mimi naamini kuwa pumzi ya uhai iliupa mwili seli hai na papo hapo roho iliingia kwa adam kwa sababu binadamu ili awe binadamu, muunganiko wa mwili na roho unatakiwa utokee katika wakati mmoja na si kimoja kianze na kingine kikikute kingine.
Huo ndio mtazamo wangu, nakaribisha wengine ili tuzidi kujifunza.
Shukran mkuu Internal
Mkuu, Hapa siogezi wala kupunguza kitu, heshima kwako.
Nikirudi nitakuwa nimeframe tu maswali kadhaa nijiridhishe zaidi kwa kile ulichonipatia.
 
Kweli yameniingia, Kumbe dhambi ni kifo. Na je kama ndio hivo mbona kuna mahali inasema tukisema hatuna dhambi tunajidanganya? Pili na je kama mtu akitenda dhambi anakufa kiroho, Je Petro alipomkana BWANA alikufa kiroho? Tatu Kama Roho wa MUNGU ndio pumzi je roho ya kibinadamu ni ipi?


Mimi kwa uwela wangu kuna Mambo haya Mwili wa binadamu unaobeba Nafsi ambayo ndio roho ya kibinadamu kwa maana nyingine ni Dhamira au nia. 2.ROHO wa MUNGU ambayo mtu hupata kwa kumtii MUNGU na kumwomba MUNGU na kuwa mtakatifu, na 3.Ni roho ya shetani ambayo huingia kwa mtu ambaye hana roho wa MUNGU pia humshawish mtu kutenda mabaya.

Ndo kusema roho ya kibinadamu hafanya kazi kwa 1.utashi wake 2.Kwa kumsikiliza ROHO WA MUNGU au neno la MUNGU na sauti yake au Mwisho Roho ya shetani,mapepo,majini n.k.

Roho ya kibinadamu hufanya kazi kwa kusikia kuona kuisi n.k Roho ya kibinadamu ndo nafsi hapo sasa kwenye kufa kwa dhambi ni Ipi kati ya Tatu hizo hufa yaani Dhamiri njema a.k.a ROHO WA MUNGU au Dhamiri ya kawaida a.k.a nia a.k.a utu a.ka Roho ya kibinadamu au Roho mbaya a.k.a Roho ya shetani nijibu ni ipi hufa? Kwa kutenda dhambi?
 
Kweli yameniingia, Kumbe dhambi ni kifo. Na je kama ndio hivo mbona kuna mahali inasema tukisema hatuna dhambi tunajidanganya? Pili na je kama mtu akitenda dhambi anakufa kiroho, Je Petro alipomkana BWANA alikufa kiroho? Tatu Kama Roho wa MUNGU ndio pumzi je roho ya kibinadamu ni ipi?


Mimi kwa uwela wangu kuna Mambo haya Mwili wa binadamu unaobeba Nafsi ambayo ndio roho ya kibinadamu kwa maana nyingine ni Dhamira au nia. 2.ROHO wa MUNGU ambayo mtu hupata kwa kumtii MUNGU na kumwomba MUNGU na kuwa mtakatifu, na 3.Ni roho ya shetani ambayo huingia kwa mtu ambaye hana roho wa MUNGU pia humshawish mtu kutenda mabaya.

Ndo kusema roho ya kibinadamu hafanya kazi kwa 1.utashi wake 2.Kwa kumsikiliza ROHO WA MUNGU au neno la MUNGU na sauti yake au Mwisho Roho ya shetani,mapepo,majini n.k.

Roho ya kibinadamu hufanya kazi kwa kusikia kuona kuisi n.k Roho ya kibinadamu ndo nafsi hapo sasa kwenye kufa kwa dhambi ni Ipi kati ya Tatu hizo hufa yaani Dhamiri njema a.k.a ROHO WA MUNGU au Dhamiri ya kawaida a.k.a nia a.k.a utu a.ka Roho ya kibinadamu au Roho mbaya a.k.a Roho ya shetani nijibu ni ipi hufa? Kwa kutenda dhambi?
Asante mkuu, kesho nitajitahidi kujibu hizi hoja zako, now mda umesonga sana.
 
Unaposema miguu yangu inauma, ni nani huyo anayesema? Miguu ni ya nani?
 
Unalazimisha roho na Mungu vipo wakati hujathibitisha hilo, kwa sababu huwezi kuthibitisha, kwa sababu havipo.


Nieleze maana ya Mungu na Roho ni nini?Kabla ya kusema vitu venye maana hiyo havipo. Unaweza kuserma vitu havipo kumbe hata huvijui.
 
Kweli yameniingia, Kumbe dhambi ni kifo. Na je kama ndio hivo mbona kuna mahali inasema tukisema hatuna dhambi tunajidanganya? Pili na je kama mtu akitenda dhambi anakufa kiroho, Je Petro alipomkana BWANA alikufa kiroho? Tatu Kama Roho wa MUNGU ndio pumzi je roho ya kibinadamu ni ipi?


Mimi kwa uwela wangu kuna Mambo haya Mwili wa binadamu unaobeba Nafsi ambayo ndio roho ya kibinadamu kwa maana nyingine ni Dhamira au nia. 2.ROHO wa MUNGU ambayo mtu hupata kwa kumtii MUNGU na kumwomba MUNGU na kuwa mtakatifu, na 3.Ni roho ya shetani ambayo huingia kwa mtu ambaye hana roho wa MUNGU pia humshawish mtu kutenda mabaya.

Ndo kusema roho ya kibinadamu hafanya kazi kwa 1.utashi wake 2.Kwa kumsikiliza ROHO WA MUNGU au neno la MUNGU na sauti yake au Mwisho Roho ya shetani,mapepo,majini n.k.

Roho ya kibinadamu hufanya kazi kwa kusikia kuona kuisi n.k Roho ya kibinadamu ndo nafsi hapo sasa kwenye kufa kwa dhambi ni Ipi kati ya Tatu hizo hufa yaani Dhamiri njema a.k.a ROHO WA MUNGU au Dhamiri ya kawaida a.k.a nia a.k.a utu a.ka Roho ya kibinadamu au Roho mbaya a.k.a Roho ya shetani nijibu ni ipi hufa? Kwa kutenda dhambi?

Kwa mijibu wa Biblia ziko aina mbili za mwili. Mwili unao haribika na mwili usio haribika. Sasa naomba ueleze hizo roho zako ulizo zifafanua hapa ukitilia maanani kuwaepo kwa hizi aina mbili za miili.

Nataka uniambie kwa nini Bwana Yesu alitoa amri ya kubatizwa kwa maji na kwa Jina la Baba nala Mwana nala Roho Mtakatifu? Je unajua kuhusu ubatizo wa moto?
 
Back
Top Bottom