Mkuu kiranga nimekuwa nikikusoma kwenye maada mbalimbali unapinga uwepo wa Mungu, mimi naomba tu uniambie binadamu na vitu vyote vilivyopo dunia vilitoka wapi kwa uelewa wako?
Sent using
Jamii Forums mobile app
Hilo ni swali la kuchunguzwa, kujulikana, kwa kufuata ukweli.
Kuchunguza na kujua kitu kuko kwa namna nyingi.
Namna moja ya kufikia ukweli ni elimination method", unapewa majibu fulani, unayatahini, yanayoonekana hayafai unayatupa.
Mathalani, ukiambiwa tafuta square root ya 2 ni nini, ukaambiwa jibu ni lazima liwe dogo kuliko 2, mtu akikwambia square root ya 2 ni 10, kitu cha kwanza kabisa, ni kuangalia, je, 10 ni ndogo kuliko 2?
Hasha. Kumi si ndogo kuliko 2, hivyo haiwezi kuwa square root ya 2.
Lakini pia unaweza kuijaribu kwa ubishi tu, 10 x 10 ni ngapi? Ni 100, si 2.
Kwa hivyo 10 haiwezi kuwa square root ya 2, utatafuta square root ya 2 katika namba zilizo ndogo kuliko 2.
Sina ujuzi w akukwambia najua binadamu katokea wapi. Kwa kweli binadamu ni hadithi ya kutungwa tu. Hakuna mtu anayeweza kuthibitisha Aadam aliwahi kuwepo. Neno sahihi zaidi ni mtu. Sina ujuzi wa kukwambia mtu alianzaje, lakini, hilo halina maana kwamba, ukiniambia jibu la uongo, kama mtu aliumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, nitashindwa kujua jibu hilo ni la uongo.
Si lazima nijue jibu la ukweli ili kujua jibu fulani ni la uongo.
Si lazima nijue square root ya 2 ni nini, ili nijue kwamba 10 haiwezi kuwa square root ya 2.
Tuchunguze mambo tuyajue kwa ukweli, tusirukie kutoa majibu ya Mungu, kabla hata ya uchunguzi.