Body(mwili), soul(nafsi) and spirit(roho)

Mwili wa kuharibika ni mwili wa Nyama uliobeba roho ya kibinadamu ila mwili usiharibika ROHO YA KIBINADAMU iliyohuishwa kwa ROHO WA MUNGU ambao mtu hupata kwa kubatizwa kwa Moto
 
Mwili wa kuharibika ni mwili wa Nyama uliobeba roho ya kibinadamu ila mwili usiharibika ROHO YA KIBINADAMU iliyohuishwa kwa ROHO WA MUNGU ambao mtu hupata kwa kubatizwa kwa Moto

Kwa nini ubatizo wa maji? Na kwa nini uwe kwa jina la Baba nala Mwana nala Roho Mtakatifu?
 
Hivi tunaposema ``mwili wa fulani`` huyu fulani tunayemrefer ni nafsi au roho?
Ngoja nijaribu. Kama utakuwa umepitia mchango wangu (sijui ni post namba ngapi). Nimejaribu kuonyesha ni vitu gani vinamtenheneza mwanadamu. Vitu hivyo ni mwili na roho. Kwa mfano; mimi naitwa stephen chelu, na nimetengenezwa na mwili na roho. Siku nikifa mtauita mwili wangu 'mwili wa stephen chelu'. Sasa stephen chelu ni yupi ambaye ameuacha mwili wake hapo. Stephen chelu ni ule muunganiko wa mwili na roho. Kwa hiyo mwili na roho kutengana ndo stephen ameondoka hivyo. Kwa hiyo stephen siyo roho wala mwili, bali ni muunganiko.

Shukran.
 
Neno 'Eden' kwa kiebrania maana yake ni 'Presence[uwepo][uwepo wa Mungu in fact].
Kwahiyo tunaona Adam na Mkewe walikuwa kwenye uwepo[eden>presence of God].
Kifo sio tukio,kufa sio kuyeyuka, kifo ni [utengano/separation kati ya mwili na roho].
Roho yako ikutengana na mwili wako tunaita kifo.
So, Adam alipoteza sifa za kuishi kwenye uwepo wa Mungu[Eden] akatengwa na Mungu: kiroho alikufa.
Ref: Ufunuo wa Yohana "...bali waongo,waabuduo sanamu,wachawi, wazinzi na wanaofanana na hao mahali pao ni ziwa la moto[jehanam], naam hii ndio mauti ya pili..."
Kumbe watu waliotajwa hapo juu watatengwa na Mungu, [mauti ya pili].
Kwahiyo kifo au mauti ni utengano wa mwili na roho, pia ni utengano wa roho ya binadamu na Mungu[jehanam ya moto,mauti ya pili].

I can enfasize
Sprit[roho>pumzi]
Body[mwili>udongo]
Soul[nafsi>pumzi+body]
 
Sasa kama ndio hivyo kwanini tunatubu
 
Hizo gharama ni zipi ambazo tunatakiwa kuziripia ili tulipate hilo vazi.
 
Hapa kuna kitu nimekiona,

Mwili, Nafsi (damu kwa maelezo yako) & Roho

Tukianza na nafsi,
Umeichambua juu juu kama damu (kimiminika), kwa mtizamo wangu msingi wa nafsi ambayo ni damu ndicho kiwakilishi cha mabaya, (ego), namaanisha dhana ya dhambi. Nafsi ndio kiini cha mtu kutenda jambo kwa kujali upande wake au kujilinda ( njaa, hasira, wasi wasi chuki na tamaa).

Nafsi ndio dhana ya ubaya ktk mti ule,
Nafsi ndio chanzo cha dhambi,
Asilimia 90 ya wanadamu wanaongozwa na nafsi,

NAFSI NI GIZA.

Tukija ktk dhana ya roho,
Roho ni mema,
ROHO NI NURU (mwanga)
Roho ni kinyume cha nafsi.


Muunganyiko wa NAFSI na ROHO,,
Ndio mti wa mema na mabaya unaozungumziwa,
Katika mti huu ndipo penye lile tunda linalozungumziwa,
Ambalo kipo ktk tawi la nafsi,

Roho na nafsi zinaishi pamoja,
Lakini nafsi inanguvu zaidi ktk kumpumbaza mwanadamu,
Kwa sababu nafsi ndio mchakato wa kujitegemea na dhana ya kutajirika au umaarufu,
Kuishinda nafsi ni kazi kubwa sana,
Aliyeweza ni yesu peke yake.

Kumbuka zile nafsi zilizo shangilia zilizo mtesa yesu akiwa msalabani zilifanya maamuzi kwa kuangalia nafsi zao,
BINADAMU NI MATEKA WA NAFSI,
Lakini yesu alisema (kumbuka wakati huo anamisumari mkononi na miguuni pamoja na taji la miimba kichwani lakini hakuyajali maumivu hayo na kejeli hizo kwa sababu alikuwa anajua hivyo vitu ni nafsi) eee baba mwenyezi mungu wasamehe watu hawa maana hawajui walitendalo,

Pia rejea yule jamaa wa kulia na kushoto pale msalabani, yule wa kushoto alimwambia yesu kama kweli wewe ni mwana wa mungu jiokoe, kujiokoa hiyo ni nafsi.

KUISHINDA NAFSI UNAHITAJI KUTAMBUA UWEPO WA ROHO NA KUISHI KIROHO,

Ndio maana tunaambiwa watakao shinda dhambi (nafsi), wataishi milele huko mbinguni.

DHANA YA UBATIZO,
Kwamba mtu abatizwe kwa maji (sio maji kama unavyofikiria),
Hapo maji yame tumika kama kiwakilishi cha roho ambacho ni damu kwa muujibu wa maelezo yako(roho).

Kwahiyo mtu kuzaliwa upya kiroho kumwagiwa maji kichwani bali NI UTAMBUZI WA NGUVU YA ROHO ILI KUISHINDA NAFSI,

ndipo upate lile vazi alilokuwa nalo adamu na hawa kwa muujibu wa DIVINE.

Hayo ni maoni yangu tu.
 
Dhambi sio kifo, kifo ni matokeo ya dhambi, Dhambi ni nafsi,

Kuishinda dhambi unaihitaji kutambua kuwa una roho,
Na utambuzi huo ni kuishinda nafsi.

Mungu asingetupa nafsi pasingekuwa na dhambi wala kifo.

Kabla ya adam na eva kula tunda nafsi ilikuwa dormant,

Nafsi ni kama virus wanaoshambulia kompyuta aina ya roho.
 
Bado nawaza kwa sauti, kwa nini hilo tunda la mti wa mema na mabaya liliumbwa.
Boss hiyo hadith yq biblia ilikua hadithi tu, yakujaribu kijenga mantik ya uumbaji na kukosa utii kwa mwanadamu.

Kuna uwezekano mkubwa kwamba hakukua na mti(binafsi siamini amini kama kulikua na mti).


Ila hoja ambayo hadithi ya uumbaji ilitaka kuwasilisha, ni kwamba binadamu alipewa (hupewa) maagizo na Mungu. Ika siku zote hukosa utiii. Na kukosa utii huko ndiko kunamletea taabu sana. .. .
Hapa duniani.

Na endapo binadamu asingekua na muelekeo wa kukosa utii asingepata taabu hizi za dunia
 
Shukrani Sana mkuu umefikiria mbali kidogo zaidi ya pale nilipofikiria.

Dhana ya ubatizo nimegusia tu kuonyesha vile tunavyoitaji kukamilishwa pale tulipopunguka ila siitaji tuzame sana uko mana sio mada kuu yetu.

Dhana ya Nafsi=Dhambi apo kama vile tumetofautiana mtazamo maana kwa jinsi mimi ninavyoelewa ni hivi, Nafsi ni Uhai, yaan mwili bila nafsi ni mfu(Udongo tu), Nikajaribu kuonyesha kwa mafungu kuwa je ikiwa nafsi ni uhai huu uhai tunaozungumzia unaebdaje kizazi hadi kizazi ?

Tukaona kuwa kumbe uhai umo katika Damu, hivyo husafiri kutoka kizaz hadi kizazi kupitia Damu. Kwa lugha nyingine uhai hupatikana ndani ya Damu ?
Ikiwa mtu atakosa Damu ni kwamba yeye hana uhai ndani yake kitendo cha kukosa Damu ni kama huyo mtu hana nafsi ndani yake, maana nafsi ndio humpa mtu uhai ambao unakaa ndani ya Damu.

Kuna kitu umeongea cha namna ya kuishinda nafsi kwamba nibkutambua uwepo wa roho, hii ni sawa kabsa, naweka uzi soon kuhusu hii mada mana nayo ni pana pia.
 

Mkuu nyoka pia alipewa adhabu ya kutembelea tumbo, sasa nina maswali mawili madogo, mosi je kabla ya hapo alikuwa anatembeaje?
Pili, kwanini adhabu iende kwa nyoka wakati shetani ndiye aliyemdanganya Eva kupitia umbo la nyoka?
 
"Msiwaogope wale wauao 'mwili' kisha hawawezi kufanya zaidi. Mwogopeni Mungu Yeye aweza Kuangamiza 'mwili' na 'roho' pia.
 
Sioni wapi Mungu amesema utakufa siku hiyo hiyo,neno linasema utakufa hakika,ikiwa na maana kuwa kuanzia pale kutakuwa na kufa na sio kuishi milele,ndio maana baada ya hiyo miaka 139 Adam alikufa...
Pia hakuna sehemu aliyosema atakufa baadae baada ya kumega tunda na kimwana, hii nayo vipi mkuu?
 
Daaaah,nimekuelewa sana mkuu naomba ni copy sijui n paste kwenye group langu la.kidini i think itachange sana mtazamo wa watu wengi..plzplz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umenena vyema lakini vipi kuhusu kitabu cha Petro kinachosena miaka elfu moja kwa mwanadamu ni sawa na siku moja kwa Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umenitoa tongotongo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umedadavua vyema hongera

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…