Mkuu kiranga nimekuwa nikikusoma kwenye maada mbalimbali unapinga uwepo wa Mungu, mimi naomba tu uniambie binadamu na vitu vyote vilivyopo dunia vilitoka wapi kwa uelewa wako?Hujathibitisha lolote zaidi ya ukweli kwamba huwezi kuthibitisha.
Jamani majibu hapa tafadhaliniMkuu nyoka pia alipewa adhabu ya kutembelea tumbo, sasa nina maswali mawili madogo, mosi je kabla ya hapo alikuwa anatembeaje?
Pili, kwanini adhabu iende kwa nyoka wakati shetani ndiye aliyemdanganya Eva kupitia umbo la nyoka?
Hilo ni swali la kuchunguzwa, kujulikana, kwa kufuata ukweli.Mkuu kiranga nimekuwa nikikusoma kwenye maada mbalimbali unapinga uwepo wa Mungu, mimi naomba tu uniambie binadamu na vitu vyote vilivyopo dunia vilitoka wapi kwa uelewa wako?
Sent using Jamii Forums mobile app
Uzi ni mtamu sana na unafikirisha kweli kweli.
Lakini kuna hoja nitazipangua hapa.
Kwanza mwanadamu ni roho inayoishi katika nyumba inaoitwa mwili...
Kwa maana hiyo ni kwamba mwanadamu anatakiwa kuangaliwa kwa kigezo cha kiroho na sio nyumba yake anayoishi kwayo, na ndio maana hata hukumu ya mwisho haitakuwa kwa mwili ila kwa roho yake.
Kuna kitu kimoja cha muhimu sana ambacho watu huwa tunachanganya.
Biblia inasema hukumu za Mungu huwa zinatoka lakini kwa rehema zake Mungu huwa zinacheleweshwa kutekelezwa mara moja.
Mfano ni kipindi cha mnara wa Babeli, Mungu alipunguza urefu wa miaka ya mwanadamu kuishi kutoka miaka 900 na ushehe mpaka miaka 120, lakini punguzo hilo halikutokea ndani ya siku moja.
Watu waliendelea kuishi kwa miaka mingi mfano Ibrahimu na Yakobo waliishi miaka zaidi ya 170.
Na punguzo lile liianza rasmi kutekelezeka mpaka kipindi cha Musa.
Ukisoma kwenye Zaburi Daudi mwenyewe anasema kuwa miaka ya kuishi mwanadamu ni miaka 70 mpaka 80, lakini Daudi huyo huyo akaishi miaka 120.
Kwa hiyo nyingi ya hukumu za Kimungu huwa hazitekelezeki kwa kwa timeframe ya kibinadamu katika time limit yetu, ila katika timeframe ya kiroho.
Ni kweli kabisa kuwa siku Adamu alipokula tunda alikufa, lakini kifo kile kilikuwa ni cha kiroho, kilikuja kudhihirika mwilini baadaye kabisa, na ndio maana Biblia inasema "Mlikuwa wafu kwa sababu ya dhambi na makosa yenu".
Kwa hiyo mtu anapotenda dhambi anakuwa mfu pale pale kiroho, Japo anakuwa anatembea na maisha yake yananawiri kama kawaida.
Mfano mzuri ni antivirus ya computer, ukiikatisha kuingia mtandaoni kuji-update inakuwa imekufa maana umeiblock kuingia kwenye source ya life yake, haifanyi kazi, ila kwenye computer itaendelea kuwepo japo haitakuwa inakamata virus.
Kwa hiyo si kwamba Adam siku alipotenda dhambi roho ilichomoka akabaki na nafsi na mwili, ila ni kweli kiroho alikufa.
Na kifo cha kiroho haina maana ya kuzimika kiroho na kukakamaa, hapana.
Kumbuka hata Jehunum ya moto Mungu anaiita kifo cha pili.
Ni kweli watu wataendelea kupumua na kuwa hai, lakini kiroho ile ni mauti.
Nikupenyezee ubuyu tu kuwa Adamu tangu amekufa mpaka wakati Yesu anakufa, hakuna mtu aiyewahi kwenda mbinguni, wote waliishia kuzimu, ni mpaka Yesu alipotoa ruhusa ya nani aende na ani abaki, maana yeye ndiye aliyeishinda mauti.
Na kweli mara baada ya kufa tu msalabani, alishuka huko chini kufanya kazi part tu, ambayo ni kuzihubiria roho za wafu na zilizomkubali zikapata kibali cha kuondoka naye.
Ni kama Yesu aliposema kuwa tubuni kwa kuwa Ufalme wa Mungu umekaribia, watu wakajua kiama kimekaribia, lakini mpaka leo miaka buku mbili imepita bado tunadunda.