Tetea sana huu ujinga ila ipo siku yatakukuta tu
Sio ujinga mkuu
Yamenikuta pia kwa sababu ya watu kutofata taratibu.
Inaleta shida kwa wamiliki halali.
Kuna sehemu hivi.
Nimefata taratibu nikamilikishwa eneo na nna hati.
Ila nikitaka kuendeleza wanaojiita wazawa wanashikia mapanga mafundi wetu.
Kuuliza shida ni nininaambiwa miaka 12+ iliyopita wavamizi walijenga kiholela hapo wakaambiwa watoke wakakataa.
Wakabomolewa.
Wakafungua kesi.
Wakashindwa, Serikali ilivyoshinda ikapima viwanja vingi zaidi pale na kuviuza ndio na si tukapata.
Sasa wamebaki wanahaha.
Kwa vurugu zao wanaishi kuwekwa ndani kwa 'tishio la kushambulia watu'.
Nasikia Serikali kwa huruma itawapa viwanja sehemu nyingine
Hv unaona madhara ya uvamizi na umiliki wa kiholela?bila kufuata taratibu za mamlaka husika.
Tabu kwa wazawa tabu kwa mtu mpya.
Bt mwisho wa siku mvamizi ndio anaumia.
Hana document hana chochote
Mapori yana watu jamani fateni taratibu