Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
Watu wajiandae kisaikolojia tu. Kumbe maviwanja ni ya low density hayo. Hapo mpango ni kuwafukuza tu ili wabakie wao matajiri.Hayo maeneo yalikua ni mapori makubwa(non-habitable) tokea uhuru. Wavamizi wamesafisha, wameokota mafuvu ya watu, wamefukuza chatu hadi pameonekana panafaa kuishi binadamu. Wamepelekewa umeme na kufungiwa na TANESCO, TARURA wakatengeneza barabara na DAWASA wamewapeleka maji na kuwafungia kabisa. Leo wanakuja na kudai ni eneo la serikali na kuwavunjia waondoke ili wapime viwanja wauziane wenyewe kwa wenyewe viwanja vya low-density. Hao maskini wataweza kununua viwanja 20m? Kwanini wasiwafikirie japo wawapunguzie bei? Na walioachwa kubomolewa ni wale walioweza kulipa hiyo pesa. Kiufupi matajiri wametamani lile eneo maana limekamilika (habitable) na sasa njia ni kuwafutilia mbali waanzilishi
Haki ya mungu huu ushenzi Magufuli asingeubariki kabisa kwa sababu una roots za ouvu wa matajiri dhidi ya watu maskini. Hakika mtamkumbuka sana yule jamaa.