Bomoabomoa yaacha simanzi Mabwepande, nyumba za matajiri zaachwa

Tetea sana huu ujinga ila ipo siku yatakukuta tu
 
nyumba kuukuu si ndo za maskini au umemaanisha nini??
 
Husikii wanaharakati uchwara wakipigia kelele hii ishu ila wakati wale wamasai wanahamishwa kule Ngorongoro Kelele zilikua Kila kona. Ubaguzi? Siasa? Au wanaangalia wapi watapata political mileage zaidi?
Watu walibomolewa Mbweni Kwa style hii hii hakuna mwanaharakati aliinua mdomo. Wanalamba asali sasa hivi
 
Tetea sana huu ujinga ila ipo siku yatakukuta tu
Sio ujinga mkuu

Yamenikuta pia kwa sababu ya watu kutofata taratibu.

Inaleta shida kwa wamiliki halali.

Kuna sehemu hivi.

Nimefata taratibu nikamilikishwa eneo na nna hati.

Ila nikitaka kuendeleza wanaojiita wazawa wanashikia mapanga mafundi wetu.

Kuuliza shida ni nininaambiwa miaka 12+ iliyopita wavamizi walijenga kiholela hapo wakaambiwa watoke wakakataa.

Wakabomolewa.

Wakafungua kesi.

Wakashindwa, Serikali ilivyoshinda ikapima viwanja vingi zaidi pale na kuviuza ndio na si tukapata.

Sasa wamebaki wanahaha.

Kwa vurugu zao wanaishi kuwekwa ndani kwa 'tishio la kushambulia watu'.

Nasikia Serikali kwa huruma itawapa viwanja sehemu nyingine

Hv unaona madhara ya uvamizi na umiliki wa kiholela?bila kufuata taratibu za mamlaka husika.

Tabu kwa wazawa tabu kwa mtu mpya.

Bt mwisho wa siku mvamizi ndio anaumia.

Hana document hana chochote

Mapori yana watu jamani fateni taratibu
 
Katiba mpya itasimamia sheria ya ardhi pasipo kujali umaskini au utajiri wa mtu wala hakutakuwa na kuonewa tena wala kjimilikisha ardhi kiholela kama ilivyo Sasa!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA!!
 
Hayo maeneo yalikua ni mapori makubwa(non-habitable) tokea uhuru. Wavamizi wamesafisha, wameokota mafuvu ya watu, wamefukuza chatu hadi pameonekana panafaa kuishi binadamu...
Hilo eneo mda mrefu ni la nssf, na kesi ipo mda mrefu sana. wavamizi waondoke wakiendekezwa wataendelea na tabia za kuvamia

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
shetani yule nyumba za kimara - kibaha alilipa fidia?
kisa hawakumpgia kura mfyuuuu

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Bila shaka Nyumba ya Mzee wangu Butiku ( one of Nyerere's Think Tank ) haijavunjwa.

Na baadae Mchana naenda Kuhakikisha na ole Wao nikute wameivunja ndiyo watanijua Mzanaki, Mmakuwa na Mtutsi MImi.
Butiku aliendaje kujenga Mapwepande?
 
True story

Kikubwa tujifunza kufuata taratibu
Kwa Tz huna cha kujifunza mkuu unaweza kupimiwa kiwanja ukapewa kibali cha ujenzi ramani na hati ukawa nayo ila utashangaa unaishi hapo miaka 20 alafu baadae unaambiwa kuna miundombinu ya railway inataka kupitishwa hapo unapoishi na kwamba hauishi kihalali ni eneo lililopimwa tangu miaka ya 60.

Yani kinacho fanyika ni dhulma ili tu wasikulipe maana hawana hela ya kukulipa
 
Kwanini maeneo mengi ya wakatoliki hatuskii kesi za uvamizi. Kuna haja ya kujifunza kutoka kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…