Bondia Hassan alilipwa elfu 60 tu kwenye pambano lililoondoa uhai wake

Bondia Hassan alilipwa elfu 60 tu kwenye pambano lililoondoa uhai wake

Bondia Hassan Mgaya aliyepoteza maisha tarehe 29 December, 2024 baada ya kupigwa TKO.

Baada ya kupigwa TKO alilipwa Tsh 60,000 kama malipo ya PAMBANO hilo

Kiasi hicho kilitajwa na Shehe ambaye alikuwa akitaka vitu vilivyokuwa halali ya marehemu, na kutaja Tsh 60,000 kama malipo ya bondia huyo

Soma Pia: Bondia Hassan Mgaya afariki Dunia baada ya kupigwa kwa TKO

Hili lisitaajabisha kijana kufanya kazi ya hatari Kwa malipo kiduchu sana

Mapromota wa ndondi acheni unyonyaji Kwa Watanzania wenzetu, Chama cha ngumi wateteeni hawa vijana wapate maslahi yanayolingana na kazi zao
Kiasi hicho kilitajwa na Shehe ambaye alikuwa akitaka vitu vilivyokuwa halali ya marehemu, na kutaja Tsh 60,000 kama malipo ya bondia huyo😭😭😭
 
elf 60 au milion 60? hivi kweli unaenda kupigana ili ulipwe kumi kumi 6?
Usishangae mkuu!

Tuliamuakama taifa siasa ndio ilipe sana kuliko KAZI kubwa za kuvuja jasho!!yaani chawa wa Rais ateuliwe au ashindishwe ubunge alipwe mapesa mengi Kwa kukaa TU lakini mkulima ,wasomi waonekane ni duni maskini wenye kesho ya kufikirika!
 
Kabla sijashutumu unaweza kunipa full breakdown ?
  • Kiingilio kilikuwa kiasi gani
  • Watu wangapi waliingia
  • Sponsorship ilikuwa Kiasi gani
  • Mwenzake alilipwa ngapi
  • Na overheads za kuandaa mtanange mzima zilikuwa kiasi gani
Haya mambo sidhani kama ni rahisi hivyo nina uhakika promoter unaweza ukainvest kwenye mpambano pesa yako isirudi na sidhani kama ndondi kwa nchi hii kwa sasa ni that much of a cash cow...
 
Bondia Hassan Mgaya aliyepoteza maisha tarehe 29 December, 2024 baada ya kupigwa TKO.

Baada ya kupigwa TKO alilipwa Tsh 60,000 kama malipo ya PAMBANO hilo

Kiasi hicho kilitajwa na Shehe ambaye alikuwa akitaka vitu vilivyokuwa halali ya marehemu, na kutaja Tsh 60,000 kama malipo ya bondia huyo

Soma Pia: Bondia Hassan Mgaya afariki Dunia baada ya kupigwa kwa TKO

Hili lisitaajabisha kijana kufanya kazi ya hatari Kwa malipo kiduchu sana

Mapromota wa ndondi acheni unyonyaji Kwa Watanzania wenzetu, Chama cha ngumi wateteeni hawa vijana wapate maslahi yanayolingana na kazi zao
Duuh kweli Umaskini mbaya, Bora kulima bustani!
 
Back
Top Bottom