TANZIA Bondia Hassan Mgaya afariki Dunia baada ya kupigwa kwa TKO

TANZIA Bondia Hassan Mgaya afariki Dunia baada ya kupigwa kwa TKO

Nina uhakika huyu bondia hajipima Afya.

Pia nina uhakika huyu ni wale bondia hutumia vitu Fulani kabla ya kulivamia jukwaa.

Pole Sana FAMILIA naona udhaifu mkubwa juu ya hili swala la boxing
Kuanzia maandalizi , lishe na n.k .
 
Huo mchezo ni hatari sana
Sio hata mchezo hatari kama wakizingatia mambo ya muhimu katika Boxing

Kuna Mtu alipigwa ngumi nyingi kama Evander Hollyfield au Muhammad Ally?

TATIZO, Hizi ngumi za uswahilini unakuta Bondia hapimwi vizuri afya na specialists au hazingatii mlo kamili unaoendana na shughuli ya Ubondia
 
Ndondi kwasasa imekuwa ni mchezo wa vijana wengi wenye hali duni, wanajitafuta, ni vizuri mtaalamu wa lishe awepo kila pambano awakague kabla ya kupanda ulingoni, anaoona hawana lishe wazuiwe, bila hivyo tutapoteza mabondia wengi.
RIP
 
Sio hata mchezo hatari kama wakizingatia mambo ya muhimu katika Boxing

Kuna Mtu alipigwa ngumi nyingi kama Evander Hollyfield au Muhammad Ally?

TATIZO, Hizi ngumi za uswahilini unakuta Bondia hapimwi vizuri afya na specialists au hazingatii mlo kamili unaoendana na shughuli ya Ubondia
Hatari sana, kama bondia atategemea hela ya Pambano ndo ale!
 
Tunatakiwa kuambiwa uzito aliokua nao. Aliopimwa kabla ya pambano, vipimo vya afya alivyofanyiwa kabla ya pambano kisha ndiyo waanze kujigamba kwamba watasimamia mazishi mwanzo hadi mwisho
 
Boxing siyo mchezo, kina gypsy king tu alipigwa Moja na usyk ile first match wenge aliloona siyo mchezo kabisa. Huu mchezo unahitaji maandalizi sana hasa ya kimwili na kiakili, huwezi kuniambia unakula mo energy na chapati au mihogo Kila asubuhi, mchana ukila vizuri sana ni dagaa au visamaki viwili, usiku chipsi au chapati mbili na maharage then unapigiwa simu tu from nowhere ukapigane kesho, this is insane. Poleni sana.
 
Tatizo la Boxing huwa hakuna kutegea waamuzi wa Ndondi Bongo wawe wanaangalia dalili za kabla ya mtu kupatwa na Brain damage.
Wanazijua basi hata dalili zake?

Ukizingatia hata huduma alizopewa zilikuwa duni mno,ilibidi mwamuzi atoe taarifa kwa kamisheni ya pambano bondia asipelekwe Sinza apelekwe moja kwa moja M/nyamala then M/nyamala wamrufae Muhimbili.
 
Bondia Hassan Mgaya amefariki dunia, siku moja baada ya kupigwa TKO katika pambano la raundi sita lililofanyika Tandale kwa Mtogole, Dar es Salaam katika ukumbi wa Dunia Ndogo, na kupoteza fahamu dakika chache baadaye.

Mgaya alicheza pambano hilo lililofanyika Desemba 28, yaani usiku wa kuamkia leo, jijini Dar es Salaam. Pambano hilo, ambalo halikuwa la ubingwa, lilimkutanisha na mpinzani wake, Paulo Elias.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika Mgaya alidondoka ulingoni na mwamuzi akamhesabia na kumpa mpinzani wake ushindi wa TKO. “Mgaya alipigwa na kwenda chini, mwamuzi akamhesabia, na ikawa TKO kwa sababu marehemu alishindwa kuendelea. Baada ya mwamuzi kumaliza kuhesabu, alitembea hatua kadhaa hapo hapo ulingoni kisha akaanguka na kuzimia,” amesema shuhuda.

Ameongeza; “Baada ya kuzimia, Mgaya alipewa huduma ya kwanza kutoka kwa madaktari waliokuwepo kwenye pambano na akazinduka, kisha akapelekwa Hospitali ya Sinza kwa ajili ya matibabu,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kufikishwa Hospitali ya Sinza, kutokana na hali yake alipatiwa rufaa ya kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambako umauti umemkuta leo. Pambano hilo liliandaliwa na Golden Gloves wakishirikiana na Ngoswe Uwezo.

Kwa upande wake, bondia Cosmas Cheka, ambaye ni Mweka Hazina wa Chama cha Mabondia nchini Tanzania, amesema suala la msiba wa marehemu Mgaya wanalishughulikia wao kama mabondia kuanzia mwanzo hadi mazishi.

Pia, Cheka amesema chama cha mabondia wapo mbioni kuandaa utaratibu wa kumsimamisha mwandaaji wa pambano hilo, Haji Ngoswe. “Nimemshauri Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mabondia Tanzania, Japhet Kaseba, kuandika barua ya kupeleka TPBRC ya kumsimamisha Promota Haji Ngoswe kwa kutoonyesha ushirikiano kwa bondia aliyefariki dunia,” amesema Cosmas Cheka akionesha masikitiko.
View attachment 3188183
R.I.Pkamanda amefariki akiwa anapambania nyota
 
Back
Top Bottom