Bondia Mwakinyo ni Mfano halisi wa Watanzania walio wengi katika nyanja mbalimbali!

Bondia Mwakinyo ni Mfano halisi wa Watanzania walio wengi katika nyanja mbalimbali!

Umeandika utopolo.

Kama alionyesha kumudu pambano kwanini a-pretend kuumia? Mwakinyo hataki ushinidi?

Wewe ambae umejua waTZ wana lack of confidence umefika wapi? Umefanya nini kama hata mtaani kwako hujulikani? Una hata robo ya mafanikio ya Mwakinyo?

Huwa mnakuwa wa kwanza pindi watu kama Mwakinyo na Dayamondi wanapoteleza wakati wamepambana kwa juhudi zao binafsi bila mbeleko yeyote si serikali wala nani. They don't owe anybody nothing. Kila jambo lao ni juhudi zao binafsi. Kama unadhani ni rahidi fanya na wewe tukujue but until then hata kwenye ukoo wenu hujulikani. STFU.
Too myopic
 
Boxing ukiwa nnje ya uwanja unaweza hisi zile ngumi ni nyepesi

ingia ulingoni usikilizie uzito wa hayo makonde,yani kuna michezo

ya kutegea au kugawa ushindi ila sio boxing unaweza ukahisi sio ngumi ni mtwangio.
 
Ukiangalia hata body lauguage yake wakati anaingia ulingoni utaona kabisa huyu jamaa alipanda ulingoni kwa maelekezo...ilikua kama sinema tu.watu wanalipa hela zao kuja kukuangalia wewe....lakni kwa tamaa ya fedha unakubali kununuliwa..ni wizi uliopitiliza
 
Muda mfupi uliopita nimetoka kuangalia pambano la ngumi kati ya Bondia Mwakinyo na Smith,pambano ambalo limeniudhi na hata kunitoa machozi!

Kama kawaida Mwakinyo ameonyesha tabia halisi ya Watanzania walio wengi!

Watu wasiokuwa na confidence,malengo wala ndoto kubwa (big dreams)!

Watu wanaoridhika na vitu vya viwango vya chini kabisa au hali ya kawaida sana.

Mtu aliyeangalia pambano round 2 kwa makini ange-conclude tu kwamba hii game ilikuwa ya Mwakinyo.
Alipata Bondia "Mzee" na mchovu, fursa ambayo angetumia kuionyesha Dunia who is Mwakinyo na Tanzania ni wapi!,lakini kwa ujinga, lack of confidence na kuridhika mapema akaanza kufanya pretence kwamba mara kaumia mguu mara kateleza! UJINGA MTUPU!

Watanzania wengi tuna tatizo kubwa sana kwenye international arena,iwe ni kwenye uongozi wa kisiasa, Uchumi au michezo, watu wetu hawana Confidence kabisa!

Sisi ni mabingwa wa umbea, udaku na mambo mengine ya hovyo hovyo basi!
Wewe mwenyewe hapa unafanya haya "Sisi ni mabingwa wa umbea, udaku na mambo mengine ya hovyo hovyo basi!".
 
Back
Top Bottom