Kuna vitu vikifika level fulani ni ngumu kuvizuia bali kuvitengenezea mazingira na utaratibu mzuri.
Kuna kipindi niliwahi andika uzi humu wa kufanya censorship ya nyimbo kwa utaratibu huu.
1. Mamlaka zinazohusika na kusimamia sanaa ziandae mgawanyo wa kimaudhui. Mfano nyimbo zote zinazotaja mambo ya ngono, vilevi, madawa ya kulevya, matumizi ya silaha ziwekwe kwenye kundi tuliite labda E'rated. Halafu nyingine zenye maudhui ya kawaida ziwe rated kama tuseme labda A'rated. Na mwongozo huu unatakiwa ufuatwe na kila msanii.
2. Msanii anapotaka kutoa wimbo lazima aufanyie tathmini ili ajue unadondokea wapi kati ya E'rated au A'rated na atatakiwa au'lebel kulingana na kundi unapodondokea.
3. Nyimbo zote ambazo ni E'rated hazitatakiwa kuchezwa redioni, kwenye tv, kwenye saluni au eneo lolote la umma. Na yeyote ambaye atabainika itabidi aadhibiwe kulingana na sheria ambayo itakuwa imetungwa (inatakiwa iwe kali sana). Nyimbo ambazo ni E'rated zitapatikana mitandaoni tu sehemu ambapo mtu anainngia kwa ridhaa yake.
4. Kama msanii ana wimbo ambao ni E'rated na anataka uchezwe redioni au kwenye tv, basi anapaswa kutengeneza clean version ambayo itakuwa rated kama A'rated.
Huu ni utaratibu mzuri unaohitajika kwa sasa ila unahitaji usimamizi wa karibu sana ili ufanye kazi. Bora huku kuliko kupiga kelele nyimbo zifungiwe kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wa filamu wanafanya hii kitu, tofauti ni kuwa kwa wao ni lazima upeleke filamu yako wanaikagua then wanaipa daraja.