Bongo Flava ya sasa ni uozo mtupu

Bongo Flava ya sasa ni uozo mtupu

Mabaharia toka Buza tumefika, waweke fence tunarukaga ukuta... kama mafisi hatuachagi hata mifupaaaaa!! MIFUPA

Cha mtu mavi wanashikaga ukuta, bia tatu ila baadae utajuta!!

Gusanisha, nyama kwa nyama.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna vitu vikifika level fulani ni ngumu kuvizuia bali kuvitengenezea mazingira na utaratibu mzuri.
Kuna kipindi niliwahi andika uzi humu wa kufanya censorship ya nyimbo kwa utaratibu huu.

1. Mamlaka zinazohusika na kusimamia sanaa ziandae mgawanyo wa kimaudhui. Mfano nyimbo zote zinazotaja mambo ya ngono, vilevi, madawa ya kulevya, matumizi ya silaha ziwekwe kwenye kundi tuliite labda E'rated. Halafu nyingine zenye maudhui ya kawaida ziwe rated kama tuseme labda A'rated. Na mwongozo huu unatakiwa ufuatwe na kila msanii.

2. Msanii anapotaka kutoa wimbo lazima aufanyie tathmini ili ajue unadondokea wapi kati ya E'rated au A'rated na atatakiwa au'lebel kulingana na kundi unapodondokea.

3. Nyimbo zote ambazo ni E'rated hazitatakiwa kuchezwa redioni, kwenye tv, kwenye saluni au eneo lolote la umma. Na yeyote ambaye atabainika itabidi aadhibiwe kulingana na sheria ambayo itakuwa imetungwa (inatakiwa iwe kali sana). Nyimbo ambazo ni E'rated zitapatikana mitandaoni tu sehemu ambapo mtu anainngia kwa ridhaa yake.

4. Kama msanii ana wimbo ambao ni E'rated na anataka uchezwe redioni au kwenye tv, basi anapaswa kutengeneza clean version ambayo itakuwa rated kama A'rated.

Huu ni utaratibu mzuri unaohitajika kwa sasa ila unahitaji usimamizi wa karibu sana ili ufanye kazi. Bora huku kuliko kupiga kelele nyimbo zifungiwe kitu ambacho hakiwezekani.
Kwa upande wa filamu wanafanya hii kitu, tofauti ni kuwa kwa wao ni lazima upeleke filamu yako wanaikagua then wanaipa daraja.
Hii ndio pointi haswaaa….Likifanyiwa kazi hili kwa kuwatumia BASATA na TCRA …. tutatatua changamoto hiyo na kulinda maadili na Sanaa..Big up ndugu
 
Nilikuwa na maana kwamba, waache watu wafanye kazi zao usiwapangie cha kuimba kisa wewe una watoto. Ndio maana nikakutolea mfano wa Nicki Minaj, kasema mimi sio mama yao. Lea watoto watoto wako kwa hayo maadili unayotaka wewe. Huu ni Ulimwengu wa utandawazi, usitake Young Lunya aimbe unavyotaka wewe kisa unalea watoto. Watoto wako hao.

Mkuu una akili sana
 
Shida JF wengi ni watu wazima na Familia zao. Ila mimi kama msanii siwezi kuacha kutunga wimbo kisa eti kuna watoto. Watoto Wana wazazi na walezi kazi yao ni Nini? Arguments zenu nyingi it's about "watoto watajifunza nini? Hawa wasanii SIO BABYSITTERS hawako kwa ajili ya kukulelea wewe mtoto wako.

Mbona hamsemi pombe zifutwe, kwani watoto hawaoni hizo pombe? Mtoto wako akiwa mlevi utailaumu TBL au wewe mzazi mwenyewe ndo inabidi ulaumiwe?

Huo muziki wa kuelimisha vitu km ukimwi n.k ni wa kipindi hicho ambapo Watanzania wengi walikuwa hawana elimu. Ila kwenye hii nchi ambayo hata mtoto wa darasa La Tatu anafundishwa kuhusiana na Ukimwi, kweli Kuna ulazima wa wasanii kuimba nyimbo kama hizo? Kuna mtu asiyejua ukimwi Unaua? Au nyimbo sijui kuhusiana na ndoa, kweli? Kwenye age hii ambayo everything is found on the internet yaani?

As a country going to a middle class phase muziki na entertainment vinafanya kazi moja tu. Kuburudisha. That's it. Hayo mambo ya kuelimisha sijui kutoa elimu kwa jamii sio jukumu La wasanii. Shule zina kazi gani sasa?

Alafu mbona juzi juzi tu hapa Rayvanny alitoa wimbo wa "kuelimisha" kuhusu Corona? Hamkuskia?
 
Shida ya wafrika hawajui wanachokitafuta.
Katika maisha kuna aina nyingi ya vitu/mambo kwahiyo unatakiwa uchague kile unachokihitaji. Shida ya wafrika hawana chaguzi, wenyewe chochote kinachokuja mbele yao wanataka kuchukua.
Ulimwengu wa sasa, ni wa pesa mbele. Muziki biashara, nani atasikiliza au kuangalia nyimbo yako umevaa dela? Angalia nyimbo ya Nick Minaj Anaconda au The one ya Dj Khalid.
Kuna nyimbo nyingi zipo lakini umeng'ang'ania mpelekee moto. Hiyo nyimbo ya mpelekee moto unajua inashika namba ngapi kwenye vituo vya radio na televishen? Ukipata jibu ujue tupo kwenye karne ya 21. Sasa hivi ukienda kila mkoa utakuta maeneo maarufu ya wadada wanauza miili yao. Hata haushituki? Si shabikii haya mambo ila ujue kuwa ulimwengu umebadilika na tunapaswa kuchague kile kinachokufaa ww.
Mkuu mzee ni nani?, ninavyojua wazee mziki wao ni rhumba za taratibu za akina mbaraka na marijani.
 
Shida ya wafrika hawajui wanachokitafuta.
Katika maisha kuna aina nyingi ya vitu/mambo kwahiyo unatakiwa uchague kile unachokihitaji. Shida ya wafrika hawana chaguzi, wenyewe chochote kinachokuja mbele yao wanataka kuchukua.
Ulimwengu wa sasa, ni wa pesa mbele. Muziki biashara, nani atasikiliza au kuangalia nyimbo yako umevaa dela? Angalia nyimbo ya Nick Minaj Anaconda au The one ya Dj Khalid.
Kuna nyimbo nyingi zipo lakini umeng'ang'ania mpelekee moto. Hiyo nyimbo ya mpelekee moto unajua inashika namba ngapi kwenye vituo vya radio na televishen? Ukipata jibu ujue tupo kwenye karne ya 21. Sasa hivi ukienda kila mkoa utakuta maeneo maarufu ya wadada wanauza miili yao. Hata haushituki? Si shabikii haya mambo ila ujue kuwa ulimwengu umebadilika na tunapaswa kuchague kile kinachokufaa ww.

Mkuu watu wanataka zile nyimbo za kina feruzi za kipindi za kuhusu ukimwi. Wanataka wawafanye wasanii kuwa baby sitters,

Cha ajabu sasa hata hizo nyimbo za zamani zilikuwa na matusi mengi tu nashangaa wamewakomalia wakina the baddest & whozu
 
Hizo nyimbo za kina Feruzi. Nani atasikiliza sasa? Hawa wasanii wetu ni wadogo sana na hawawezi kuharibu maadili. Ashajiuliza kuhusu wasanii wa nje kama kina Nick Minaj, Beyonce n.k?
Vipi kuhusu video za ngono? Hapa Tanzania hakuna watu wanaocheza video za ngono lkn mpaka DVD zake zipo. Na watu wanazo kwenye simu na wanaangalia. Kile wanachoimba wasanii ni matokeo ya jamii.
Mkuu watu wanataka zile nyimbo za kina feruzi za kipindi za kuhusu ukimwi. Wanataka wawafanye wasanii kuwa baby sitters,

Cha ajabu sasa hata hizo nyimbo za zamani zilikuwa na matusi mengi tu nashangaa wamewakomalia wakina the baddest & whozu
 
"mpelekee moto"

Naona ichi kipande huwa unakitafakari sana😀😀🤣🤣

Yaani hawa watu watatu wamekuja na mziki wa peke yao Baddest47, Whozu na Young lunya.
 
"Hizo bia unazomnunulia brother ukipiga kimoko ukalala atatangaza ,sio pesa usipokaza utaitwa kilaza ,we mpelekee moto peleka motooooo"

Haahaaaa

Lunya sasa

"Harafu akiwa ameshoboka na ofaa za bia akasahau kumpelekea moto itafatia ....

Pisi nyingine zinatabia za kitoto nishatuma nauli kufika ndio changamoto ,akifika geto hakuna story Wa maji mpelekeeee motooo pelekaaa motooo"

Aisee hili gomaa linabamba redion....
 
Back
Top Bottom