Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Nimefanya kazi za documentary kama msimamizi na pia za matangazo, naelewa nini nachozungumza, nilitengeneza script ya tangazo ambalo lilionekana bora kuliko waliosomea.
Point yako haina msingi hata kama sijawahi kutengeneza movie mwisho wa siku ukitengeneza unaotegemea kununua kazi zako sio walio na ujuzi wa movie industry lakini kitakachovutia kazi zako kununiliwa ni ubora wa kazi yako si kinginecho.
Kwa jinsi ulivyonijibu ndivyo inavyoonyesha upeo wenu ulivyo.
Nataka nikupe somo wewe na wenzako, Hollywood kuna watu wanaitwa criticism ambao movie ikitoka wao wanaangalia kabla haijaenda sokoni, wengi ni waandishi wa magazeti au watangazaji wa tv maoni yao ndio yanaiganya movie iuzwe au ikose soko na kazi yao kubwa ni kukosoa lakini nyinyi mkiambiwa ukweli mnabaki kubisha ndio maana movie zenu za hapahapa hazina mbele wala.nyuma.
 
Waziri kama shangingi[emoji23][emoji23], hata mimi nilishangaa, Tatizo hawafanyi research maisha ya waziri yanakuaje akiwa nyumbani , the way wanavyoongea Yan utadhan mmama anayeuza wanawake malaya
Hahahaha yaani nimecheeeka, sio utadhani shangingi ni lishangingi flan hivi kama sio la Magomeni basi la Kigogo linalomiliki danguro eti ndio waziri aiseee!
 
Kwa jinsi wanavyoshupaza shingo wakikosolewa ndivyo wanavyozidi kwenda kuharibu, yaani wanaambiwa kuhusu story zao kukosa ubunifu na msisimko wanasema bajeti, Wanaambiwa waoneshe uhalisia wa hayo maigizo yao wanasema bajeti, wanaambiwa watafute location nzuri hapa hapa Tanzania tuna vivutio teleeee wanasema bajeti,

Basi watupishe wenye bajeti zetu tufanye kazi napo wanasema Bajeti, hehehehehe kazi kweli kweli.
 

Umesema vizuri sana

Niliwahi kufikiria kuwekeza huko Bongo Movies ili nimtafute director na mwandishi mzuri anayejua theater arts sawasawa kusudi awe anachagua waigizaji na kupanga maudhi siyo hawa wanaodhani movie ni urembo na kuigiza raha raha tu. Nilitaka tuanze kwa kuwa tunatengeneza movie zinazohusu uharifu na usimamizi wa sheria: kuwe na waharifu wazuri, polisi wazuri, wapelelezi wazuri, waendesha mashtaka wazuri, mawakili wazuri na mahakimu wazuri katika setting ambayo mtazamaji atadhani ni kweli kabisa. Nilipata miguu ya baridi baada ya kutoelewana na mtu ambaye nilitegemea awe msimamizi wa mradi huo.

Ni wazi kuwa Bongo movies hamna kitu kabisa ingawa Kanumba (RIP) alikuwa anajitahidi kidogo lakini naye alikuwa hajaiva sawasawa; movie zao ni za mambo ya kitoto, hazibuniwi vizuri na zina ujinga mwingi sana. Kuna muvi niliangalia zamani kidogo eti jambazi anavamia nyumba ya kifahari lakini alipofika mlangoni akuvua viatu kwanza kabla ya kuingia ndani. Huwezi kutengeneza movi nzuri kwa wiki moja tu!!
 
Bongo movie noma eti movie ya maisha ya hayati rais Magufuli tayari imekamilika. Kwa Maisha ya rais Magufuli eti movie yake ikamilike ndani ya wiki tatu hawa bongo movie hamna kitu hata kama hiyo movie sijaiona ila itakuwa utopolo tu.
 
Labda useme ujuzi ndo watakuelewa ukisema Elimu what comes in their mind is bachelor degrees. Unaweza tu kujifunza mambo ya film kupitia platform mbali mbali kuongeza ujuzi, tasnia ya uigizaji inahitaji akili zisizo za kawaida

Mkuu yeye huyo mleta mada ndie anaemaanisha Bachelor Degrees, mimi nimezungumza wazi kuwa taaluma ni muhimu na taaluma unajifunza kwa njia nyingi tu, nilichopinga mimi ni hii moja kwa moja kuamini Bachelor degree kitu ambacho hakina uhalisia kwenye masuala ya kuigiza. Yeye yupo kutolea povu watu walioishia darasa la 10.
 
NI HITIMISHE KWA KUSEMA,
WAIGIZAJI VILAZA WANA ANDAA MUVI KWA AJILI YA VILAZA WENZAO. NI VIGUMU WASOMI KUINGIA HUKO KWANI WATALAZIMISHWA KUSHABIKIA CHAMA CHAO

View attachment 1746116

Kwahili nikae kimya tu, ila hila tatizo sio kwa hawa tu hata wale Bongo fleva ambao mnawasifia nao ndio haya haya
 

Critics daima hawajawahi kuamua hatma ya biashara za filamu, nayaelewa vizuri haya mambo.
 

Kwani umekatazwa si ukatengeneze?
 
Wewe ndio huelewi, filamu zenu mnakurupuka hamfanyi tafiti zozote, hamjui kuhusu masoko ya sinema zenu ndio maana mnatoa sababu zisizo na kichwa wala miguu

Kwanza mkuu mimi sihusiki na masuala ya Movie industry, na wala sio mshabiki wao. Naongea hapa ninachokielewa tu.

Kuendelea kuwashutumu waigizaji wakati hao waigizaji hawazidi hata asilimia 20% ya tatizo ni kuwaonea tu. Tatizo la bongo movie ni pana sana.
 
Critics daima hawajawahi kuamua hatma ya biashara za filamu, nayaelewa vizuri haya mambo.

Hawafahamu hayo mambo mkuu. Kuna movies zina very small ratings rotten tomatoes na metacritic lakini zimefanya vizuri kwenye soko na box office.

Hawafahamu haya mambo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…