Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Kuna siku nliona Daktari wa bongo movie akisema "presha iko sawa, maleria pia iko sawa...." Nikatoka nje make nlikua kwa watu ningekua kwangu ningezima tv.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].. Dahh
 
Kuna siku nliona Daktari wa bongo movie akisema "presha iko sawa, maleria pia iko sawa...." Nikatoka nje make nlikua kwa watu ningekua kwangu ningezima tv.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] hhh
 
Mkuu umetisha sana, tena SANA ..
Point tupu toka mwanzo mpaka mwisho..
Btw naweza nkasema sio muangaliaji sana wa hizi movies unless sina usingizi au bored sna,
Best movies nlizozikubali ni ile girlfriend ya kina t.i.d,
Kuna action movie moja hivi mpaka wanapgana juu ya train (jina sjui) na nyingine ni action pia villain ni castrol Dickson mtangazji km sjakosea,humo ndani yumo uwoya na jeshi la police liliplay part nzuri.
Wanaojua majina ya hizi movies ntashukuru mkitaja
 
Jambazi likiwa linanyata utasikia ngingiiiiiiiii ngingiiiiiii..... Mtu Yuko beach anawaza nusu saa nzima , kichekesho kwenye sauti aisee inabidi remote yako iwe standby ....
Bongo movie Mungu anawaona aisee
 
Pamoja na kwamba nakubaliana na mleta UZI kwa sehemu but mengine kayakuza sana. Nitajie elimu za kina Bruce Lee, Chuck Norris, Anold Schwezneeger, Bill Blanks nk. Weka elimu zao wakati wakiwa wanatingisha sana soko la filamu those years; ukimaliza njo kwa wana music almost wote duniani kuanzia kwa kina Michael Jackson, Steve Wonder hadi hawa wa sasa. Binafsi bado natazama sana filamu zetu, ni shabiki wa kina JB, Rich Mtambalike, kina Nandy (utasema Nandy ni msomi) yule mama wa kingoni ambaye kacheza kama mama mkwe kwa igizo la HUBA kule DSTV, Bi Sikitu nk

Sijaona makosa makubwa kwa kina JB, Richie nk, yapo makosa ya kawaida sana ambayo hata hizo filamu za hao uliowataja hua yapo. Tasnia yetu Bongo sidhani kama shida ni elimu, waigizaji wanaweza wasiwe na shule kubwa sana but waongozaji labda script editors hao yes shule inatakiwa. Nitajie ubora wa Kanumba enzi hizo halafu nitajie udhaif wa kina JB leo; industry ya filamu bado ni changa as i said, kadiri siku zinavyo kwenda unaona kabisa wanavyo improve, to me wasani wanakua na sanaa yao inakua sana.
 
Mkuu naomba unitajie jina la hiyo muvi ambayo koplo anampigia saluti koplo au ni mwigizaji gani aliigiza kwa hiyo movie ili niitafute.

Tusije tukawa tunaongelea vitu ambavyo havipo ili tu tufurahishe umma
Labda misukosuko ya jayplus
 
Nafikiri hoja yako sijui kama ina maana la zaidi ni post ya udhalilishaji. Kuna vitu ni talent. Kuwa akili ya kujibu physics hakukupi talent ya kuwa muigizaji nzuri. Nafikiri unashindwa kuheshimu kwamba uigizaji unahitaji kipaji na sio kila mtu.
Najuhudi mkuu mf ukiangalia series ya KELELE iliyoandaliwa na Hayati Ruge ni dhahiri jamaa angepewa saport hakika angeiinua Bongo mvie
 
Pia kuna kampuni ilikuwepo ilikua inaitwa Wananchi video productions store ambayo ilikuwa inasambaza film za Jumanne kihangala na Mussa Banzi nayo ilisitisha usambazaji kipindi cha kikwete na 7bu ilikua ni uigizaji mmbovu wa wasanii
 
Mkuu mtake radhi mzee Jengua ni marehemu kwasasa
 

Unataja watu waliowika enzi za giza dunia ikiwa gizani,

waambie sasa hivi waigize Movie uone kama hutaona vituko.

Hata hawa Bongo Movie wangeigiza hizi movie miaka ya 90 huko zingeonekana ni nzuri kutokana na akili za wakati huo.

Huna shule itaigiza nini kama sio utumbo tuu
 
Wewe umeongea bonge la POINT kweli ma director ndio kiini cha UBORA au UTOPOLO wa movies
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kaka tuhurumie mbavu zetu ah ah ah ah[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Tuwakele kidogo ili wakae kikao wajifikilie tena
 
William Wayne Blanks is an American fitness guru, martial artist, actor, and the creator of the Tae Bo exercise program. In 1981 won men's karate medal representing USA.

Carlos Ray "Chuck" Norris is an American martial artist, actor, film producer, and screenwriter. After serving in the United States Air Force, Norris won many martial arts championships and later founded his own discipline Chun Kuk Do. Norris is a black belt in Tang Soo Do, Brazilian jiu jitsu and judo.

Bruce Lee was introduced to the film industry by his father and appeared in several films as a child actor. His early martial arts experience included Wing Chun, tai chi, street fighting, and boxing, winning the Hong Kong schools boxing tournament; he also learnt cha-cha dancing, winning the Hong Kong cha-cha championship. Lee moved to the United States at the age of 18 to receive his higher education at the University of Washington in Seattle; it was during this time that he began teaching martial arts, later drawing significant attention at the 1964 Long Beach International Karate Championships.

Schwarzenegger served in the Austrian Army in 1965 to fulfill the one year of service required at the time of all 18-year-old Austrian males. During his army service, he won the Junior Mr. Europe contest. He went AWOL during basic training so he could take part in the competition and then spent a week in military prison.

Nafkiri umeona vigezo vyao hao wote, wote wametoka mbali, wana experience kibao tangu wakiwa watoto ndio maana hata movie zenyewe walizicheza kama ukweli vile, walijua walichokuwa wanakifanya na pia kupitia mentors wao wakaendelea kufaulu.
Haya mambo ya kuokotana vijiweni ati msela ashakua actor/actress wakati hata hakuna chembe ya experience ako nayo be it academically or life ones ni utopolo unaoangusha filamu za Bongo na nchi zingine tu😂
✌️
 

Huyo hujui anachokitetea Mkuu

Ili uigize pasipo elimu yakupasa uigize movie aina za kina Bushman yaani vituko vituko, lakini movie za akili hutoweza asilani.

Hata hivyo movie zenye maudhui ya kati ya masuala ya kawaida ya kijamii zinaweza igizwa hata na watu wenye elimu ya kawaida kama vile TAMTHILIA YA SIRI YA MTU. lakini Director wake ni wamoto kielimu Mr Jordan
 
Sidhani kama elimu ya waigizaji ndo tatizo maana kile ni kipaji. Tatizo ni directors na watunga hadithi. Unless mwigizaji ndo awe director.
Tatizo mnadhani elimu ni degrees au Diploma, Elimu kwa maana ya kujifunza vitu vipya, kurekebisha ya zamani, ndio maana kuna shule za mambo ya uigizaji, kipaji bila kuongezea udambwi dambwi ni kazi bure, kila siku utatoa kitu kile kile na hadhira itakuchoka,
 
Wewe umeongea bonge la POINT kweli ma director ndio kiini cha UBORA au UTOPOLO wa movies

Kwa ma directors wa Bongo movies, hata umtoe Robert Di Nero Hollywood ukimuingiza ndani ya bongo movie na pia utamuona utopolo tu
 
Anayeigiza sasa hapo kosa lake lipi? Si director ndo anajua nani anafaa hapa nani hafai? Kama muigizaji hana udambwi dambwi si ni kazi ya director kutokumpa nafasi? We sema mifilamu yenu muigizaji huyo huyo director.
 
In his early days, Lawrence did comedy shows in the Washington, D.C., area and supported himself through odd jobs. Comedian Ritch Snyder saw his act and suggested Lawrence make connections in New York.[6] Lawrence ended up moving to New York City and found his way to the legendary The Improv. Shortly after appearing at The Improv, Lawrence won a performance spot on Star Search.[1] He did well on the show and made it to the final round, but did not win. However, executives at Columbia Pictures Television saw Martin's performance and offered him the role of Maurice Warfield

Katika siku zake za mwanzo, Lawrence alifanya maonesho ya ucheshi katika eneo la Washington, D.C. na akajisaidia kupitia kazi ndogondogo za mitaani. Mchekeshaji Ritch Snyder aliona kipaji chake na akapendekeza Lawrence aunganishwe New York. [6] Lawrence aliishia kuhamia New York City na akapata shavu kwenye kazi za The Improv. Muda mfupi baada ya kuonekana katika The Improv, Lawrence alishinda nafasi ya ushiriki kwenye Star Search. [1] Alifanya vizuri kwenye onesho hilo na kufika hadi raundi ya mwisho, ingawa hakushinda. Wakuu wa Columbia Pictures Television waliona uwezo wa Martin na wakampa nafasi ya kucheza kama Maurice Warfield.

Nimejaribu kuweka hayo maelezo ya mmoja wa Waigizaji wa Hollywood, Martin Lawrence waliotokea mtaani tu...ambao kama Eddy Murphy na wengine kipaji kilitangulia.

Nikisoma bandiko la Mleta uzi ninaona zaidi ni kama ameamua kuzimwaga hasira zake kwa hawa Wana tasnia ya Filamu labda kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe.

Ni kweli inahitajika Elimu ili kufanya jambo lolote kwa ufanisi lakini sio kila Mwenye Elimu hufanya mambo kwa ufanisi au aliyekosa Elimu anaharibu kila anachokifanya.

Na tunapoongelea Filamu tukumbuke kuwa hii ni zao la kazi ya TIMU....na timu inahusisha Watu wa aina tofauti, hivyo wapo wanaohitaji Elimu ya kina,wapo wanaohitaji Elimu kiasi, wapo wanaohitaji kipaji (talent) zaidi...haswa Waigizaji.

Ni kweli unaweza kumfundisha Mtu kuigiza lakini utapata matokeo mazuri zaidi iwapo utamfundisha Mtu ambaye tayari ana kipaji cha kuigiza.

Changamoto tunayokumbana nayo hapa kwetu ni namna wanavyopatikana hao Wenye Vipaji vya Uigizaji. Hapa kwetu ukilinganisha na Nchi nyingine haswa zilizoendelea Mtu Kujihisi ana uwezo wa kuigiza na Mfumo kumkubali kuwa ana uwezo huo ni tofauti na huku kwetu ambapo wengi huingia huko kama tu kujaribu bahati zao na kwa isivyo bahati mfumo dhaifu uliopo unawapokea tu vivyo hivyo.

Kwa upande mwingine ukiangalia hata wanaosimamia , ambao labda walitarajiwa kutoa msaada (support) nao ni kama wanafuata mkumbo tu....ndio maana ukiangalia kwa makini utaona kila wanapoongelea kuinua tasnia basi nguvu zote na akilia wanaelekeza kwa Wasanii moja kwa moja....na kwa kuwa Wasanii nao ni "Wasanii" basi wanawapokea na mwisho wa siku hakuna matokeo yoyote chanya yanayopatikana.

Wanachopaswa kufahamu ni kuwa Msanii/Muigizaji ni sehemu tu ya timu, Filamu nzuri ni matokeo ya Screenplay nzuri, Upigaji picha mzuri na Uigizaji mzuri...mengine ni ziada lakini kama yanapatikana ni sawa.

Na kama kweli wanataka kukuza tasnia basi ni lazima nguvu iwekwe kwa Watayarishaji na sio Wasanii..kama ni kuwasaisia Wasanii basi wao ni kuwatafutia kozi za kuboresha uigizaji wao...Filamu bora zitatokana na Wazalishaji (Producers) Imara na wenye weledi...chini ya Mwamvuli wa Wazalishaji tutapata Waelekezi (Directors), Wapiga Picha(Cinematographer) n.k....Wasanii huajiriwa tu kwenye Filamu....sasa hapa kwetu ukisikia mikakati ya kuinua tasnia watawatafuta kina JB, Ray n.k....na kwa kiasi kikubwa huwa ni mikakati ya kisiasa zaidi kuliko kiuhalisia.

Nchi ikiwa na Vipaji vya kutosha swala la Elimu rasmi ya darasani sio tatizo kubwa ki hivyo kiasi kukwamisha mambo...ingawa tofauti ya ajabu niionayo ni kwa Mbongo akikwambia hajaenda shule ni tofauti na Chris Rock akikwambia hajaenda shule..Chris Rock au Dave Chapelle akisimama jukwaani kuongea hata unahisi labda angeenda hizo shule kivile angepoteza uwezo ule alionao.

Ushauri ninaodhani unaweza kubadilisha mtazamo wa tasnia ni kupokea damu changa zenye mawazo tofauti, damu changa zenye walau abcd za haswa nini maana ya kuwa Muigizaji...Damu changa waingie wakijua umuhimu na maana ya Screenplay/Script kwenye Filamu. Wakongwe tulionao wengi wanategemea uigizaji wa kuongea/kubwabwaja tu kama silaha yao kuu ya kuigiza ambamo ndani yake ndimo huficha udhaifu wao wa kuigiza...tutafute damu changa wenye vipaji waheshimu na wajue nidhamu ya Screenplay/Script..Filamu ni sanaa ya maonesho na sio ya kuelezea kwa maongezi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…