Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Umemaliza kila kitu mkuu ikibidi fungua uzi wako wasanii wajue nini cha kufanya, pia kitu kingine kinachouwa tasni ni mashabi ama hadhila kwa ujumla kukalilishwa kuwa bila msanii fulani hiyo film haiwezi kuwa mzuri
 
Mkuu na kwenye Bongo Flava wamo wengi tuu...
 
Sijaona shule zao hapo mkuu; nimeona mambo ya kijeshi na Bruce kua introduced na baba yake huko kwenye martial artists. Uzi unazungumza habari za shule za wasanii, nami nimeleta kama changamoto ya hao wachache kwamba nitajiwe elimu zao; labda sielewi kingereza, kuna sehemu Chuck Norris imeoneshwa kasoma hadi level gani ya elimu hapo?
 
Mkuu, unajua bado hao unaosema waliigiza enzi za giza bado movies zao zinabamba youtubes kwa zama hizi za mwanga? But again but watu wana nunua CD zao madukani until now, picha zina zaidi ya miaka 50 lakini hadi leo bado zipo madukani.
 
Mkuu, hao jamaa experience zao ni shule tosha, na pia katika maisha yao wamepishana na wacheza film na ma director wakubwa ndio maana wakaonekana uwezo wao huo. Sio lazma uwe na Degree wala nini, kama huna experience yoyote ya kimaisha kama za hao jamaa hata ukipewa scene uicheze itakuzingua. Kwa wale wako shule za uigizaji, atleast hao huwa na knowledge kiasi ya kuigiza lakini sio kila mtu anayemuona unataka kumpatia Chance ya kuigiza, ndio hayo maneno ya movie za utopolo sasa.
 
Kama umenifatilia kuanzia mwanzo kabisa utagundua lugha unayo ongea ndio ninayo ongea as well; nilimalizia kwa kusema, "bongo movie inakua kadiri siku zinavyo kwenda" kwa hiyo statement,ndio experience yenyewe unayoisema wewe, kua na shule kubwa sio kigezo. Mdau kazungumzia degree za hao Wanageria, tuweni wakweli, nani ananunua CD za picha za Nigeria za miaka 10-20 iliopita? Au nani ana dowload youtube ile picha ya Nigeria ya pastor Ken sasa hivi? Jibu ni either hakuna, kama wapo basi may be ni less than 1000, kwa Bongo hapa ndio sidhani kabisa so tusiwakatishe tamaa wasanii wetu wa ndani kwa kigezo cha degree, by the way hata hao Wakorea ambao jamaa kawatolea mfano, huenda tuki search CV zao utagundua hata wenyewe wenye degree huenda ni wachache sana.
 
Kweli hapo, ila utaalamu wa kuigiza pia unahitajika na kuna vyuo vinavyotoa tauluma hiyo. Huwezi linganisha aliyepitia chuo cha uigizaji na aliyechukuliwa tu mtaani sababu ati alikuwa akiigiza vizuri shule za msingi, haiwezekani. Akili zao ni tofauti na hapo ndipo ubora wa filamu unapoingilia.
 

Kutumia nguvu nyingi kuwa criticize waigizaji ni wazi kuwa tunashindwa kufahamu tatizo halisi la tasnia yenyewe. Waigizaji ni sehemu ndogo tu ya tatizo.
 
Elimu ya Darasani sio msing ila inasaidia,hata ukiangalia huko Hollywood kuna big directors lkn hawana hizo elimu za degree za film kuna big actors lkn hawana elimu

Tatizo la Bongo movie linasababishwa na hao wadau wabongo movie wenyewe.kuhusu bajeti hilo sio tatizo maana ukiangalia hizo tamthilia wanazoigiza watu wamepiga makeup nzuri,nguo Kali,wamekodi majumba makali,location za gharama kabisa, gari za gharama, kamera zina quality unaona kabisa bajeti sio shida.
Shida hawa watu wnafanya kimazoea mazoea.
Nlibahatika kufanya kaz na star wa bongo movie mkubwa tu mwaka Jana kma intern bwana tukawa tumeenda location ikatokea lights na equipment zake hazijafika kwa sababu mwenye nazo alikuwa kapata gig nyingne, sasa huyo star mwenyew ambay ni director,producer na main actor pia akasema tushoot hivyo hivyo bila lights dah nlishangaa sana,na movie within two days ilikuwa tayari
 
Bongo movie INA safari ndefu sana maana.mm naamin wakiwa serious na wakafanya kazi nzur wawekezaji watakuja weng na wakutosha,nenda kaangalie wasouth na wanaija huko Netflix.
Kuna series mmoja huko Netflix y kisauzi jina lake sikumbuki ila inahusu msichna mmoja anaenda shule ya matajiri kumtafuta pacha wake,ni series ya kawaida hata aina budget kubwa ila n nzuri
 
Serikali isipotia mkono hata huo ujinga unaofanywa na vijana hautaisha. Hiyo sanaa iliyopo inafanywa sababu kuu ikiwa kuganga njaa na sio vipaji. Serikali haina la kujitetea katika hili
 
Serikali isipotia mkono hata huo ujinga unaofanywa na vijana hautaisha. Hiyo sanaa iliyopo inafanywa sababu kuu ikiwa kuganga njaa na sio vipaji. Serikali haina la kujitetea katika hili
Kwa wasanii wa muziki serikali ilitia mkono gani mpaka leo tunaona kina diamond wanapaa?? Tusiilaumu tu serikali ilhali watu hawana jitihada binafsi.

Hukohuko bongomovie, enzi za kanumba hadi kupaa namna ile serikali ilitia mkono gani katika yale mafanikio, ni jitihada tu mkuu.
 

Huwezi kufananisha muziki na film industry, filamu industry ni tasnia inayohitaji uekezaji mkubwa pamoja na taaluma kubwa.
 
Huwezi kufananisha muziki na film industry, filamu industry ni tasnia inayohitaji uekezaji mkubwa pamoja na taaluma kubwa.
Hata muziki unahitaji uwekezaji na taaluma vilevile. Huwezi kufanya vitu hovyo ukategemea kufanikiwa mkuu, wasanii wa muziki wanaenda kushoot video zao nje ya nchi kwa gharama, wanawatumia directors kwa gharama kubwa halafu unasema huwezi kufananisha mkuu una maana gani hapo?? Wasanii wa muziki wengine wanakwambia video zao wametumia zaidi ya 50M mpaka kukamilisha. Kuna siku nilimskia msanii anasema wametumia 14M kukamilisha movie, hebu linganisha hapo wimbo una dakika 4 tu 50M imetumika lakini filamu masaa zaidi ya 2 na location tofaut tofaut na mambo kibao eti 14M tu. Wakati huo filamu nyingine hazitumii hata 1M.

Wajitathmini mkuu.
 

hiyo filamu iliyotumika kukamilika kwa milion 14 ndio hayo matatizo yenyewe ya filamu zetu. Filamu zinatakiwa kwa kuanzia tu zianzie alau milion 200 kwenda mbele.
Lakini nani atawekeza pesa zake nyingi bila ya kutarajia return?
Filamu zinategemea mauzo makubwa kwa kupitia cinemas, bongo hatuna kabisa tamaduni za kwenda cinema.
Filamu zinategemea kupata hela kwa kupitia streaming webs, bongo hatuna kabisa tamaduni za kujiunga na kulipia hizo streaming webs.

Mzunguko wa uingizaji pesa muziki ni mwepesi sana ndio mana wanaweza kurisk hizo 50 m, Ila kwa filamu ni ngumu ku risk hele ndefu hata ukatungiwe story na mtunzi kutoka Hollywood.
 
Mimi bado nakupinga mkuu ni vile tu hatujajizatiti huko naungana na mtoa uzi 100%. Tasnia imejaa wasioelimika kuhusu hiyo kazi yao. Japo uchumi ni changamoto lakini unaona kabisa jinsi hata hiyo pesa kidogo wanavotumia kutuonesha madudu kwenye filamu zao nyingi zenye story moja yenye kisa kinachofanana (MAPENZI).

Wasanii wa muziki miaka ya zamani hawakua watu wa kwenda kushoot video zao nje na kushirikisha saana wasanii toka nje ya nchi. Lakini hivi karibuni baada ya kuona wenzao wanaenda sana kushoot nje na wanashirikisha wasanii wakubwa wa nje nao wameiga icho kitu na kinawapa matokeo chanya. Ona jinsi tasnia ya muziki inavopaa, mfano ni hawa wasanii kina maroo,mboso na wanaofanana na hao.

Haya tuje kwenye filamu zamani ilikua inafanya poa sana na iliteka sana soko la bongo ikichuana na nigeria, hizi za kikorea zimekuja hivi karibuni tu labda za kihindi na kizungu ndio zilitamba sana enzi hizo nazo ilikua ni vibanda umiza majumbani ilikua bongo movies. Akaja kanumba nae akaipaisha mno, Ray nae hakua nyuma. Je hawa wasanii waliobaki walicopy nini toka kipindi kile sanaa iko juu, enzi za kanumba & Ray, yaan hakuna la kujifunza kabisa kwa hivyo vyote kama wenzao wa muziki wanavyonata na soko lao.
 
Ila mkuu ukienda mkoani huko Film za kibongo zinakiki
 
Ila mkuu ukienda mkoani huko Film za kibongo zinakiki
Sijajua mikoa mingine ila kwa michache niliyotembelea naona ni hizi series za kikorea zilizotafsiliwa. Na wengine ndo izo movies na series za nje, nyuzi zilizopo humu kuhusu masuala ya filamu pendwa zinathibitisha hilo. Hawajadili movie za bongo ni za nje tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…