In his early days, Lawrence did comedy shows in the Washington, D.C., area and supported himself through odd jobs. Comedian Ritch Snyder saw his act and suggested Lawrence make connections in New York.
[6] Lawrence ended up moving to New York City and found his way to the legendary
The Improv. Shortly after appearing at The Improv, Lawrence won a performance spot on
Star Search.
[1] He did well on the show and made it to the final round, but did not win. However, executives at
Columbia Pictures Television saw Martin's performance and offered him the role of Maurice Warfield
Katika siku zake za mwanzo, Lawrence alifanya maonyesho ya ucheshi katika eneo la Washington, D.C. na akajisaidia kupitia kazi isiyo ya kawaida. Mchekeshaji Ritch Snyder aliona kitendo chake na akapendekeza Lawrence aunganishe New York. [6] Lawrence aliishia kuhamia New York City na akapata njia ya hadithi ya The Improv. Muda mfupi baada ya kuonekana katika The Improv, Lawrence alishinda nafasi ya utendaji kwenye Star Search. [1] Alifanya vizuri kwenye onyesho na akafanya raundi ya mwisho, lakini hakushinda. Walakini, watendaji katika Televisheni ya Picha ya Columbia waliona utendaji wa Martin na wakampa jukumu la Maurice Warfield
Nimejaribu kuweka hayo maelezo ya mmoja wa Waigizaji wa Hollywood, Martin Lawrence waliotokea mtaani tu...ambao kama Eddy Murphy na wengine kipaji kilitangulia.
Nikisoma bandiko la Mleta uzi ninaona zaidi ni kama ameamua kuzimwaga hasira zake kwa hawa Wana tasnia ya Filamu labda kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe.
Ni kweli inahitajika Elimu ili kufanya jambo lolote kwa ufanisi lakini sio kila Mwenye Elimu hufanya mambo kwa ufanisi au aliyekosa Elimu anaharibu kila anachokifanya.
Na tunapoongelea Filamu tukumbuke kuwa hii ni zao la kazi ya TIMU....na timu inahusisha Watu wa aina tofauti, hivyo wapo wanaohitaji Elimu ya kina,wapo wanaohitaji Elimu kiasi, wapo wanaohitaji kipaji (talent) zaidi...haswa Waigizaji.
Ni kweli unaweza kumfundisha Mtu kuigiza lakini utapata matokeo mazuri zaidi iwapo utamfundisha Mtu ambaye tayari ana kipaji cha kuigiza.
Changamoto tunayokumbana nayo hapa kwetu ni namna wanavyopatikana hao Wenye Vipaji vya Uigizaji hapa kwetu ukilinganisha na Nchi nyingine haswa zilizoendelea....kwa Wenzetu Mtu Kujihisi ana uwezo wa kuigiza na Mfumo kumkubali kuwa ana uwezo huo ni tofauti na huku kwetu ambapo wengi huingia huko kama tu kujaribu bahati zao na kwa isivyo bahati mfumo dhaifu uliopo unawapokea tu vivyo hivyo.
Kwa upande mwingine ukiangalia hata wanaosimamia , ambao labda walitarajiwa kutoa msaada (support) nao ni kama wanafuata mkumbo tu....ndio maana ukiangalia kwa makini utaona kila wanapoongelea kuinua tasnia basi nguvu zote na akilia wanaelekeza kwa Wasanii....na kwa kuwa Wasanii nao ni "Wasanii" basi wanawapokea na mwisho wa siku hakuna matokeo yoyote chanya yanayopatikana.
Wanachopaswa kufahamu ni kuwa Msanii/Muigizaji ni sehemu tu ya timu, Filamu nzuri ni matokeo ya Screenplay nzuri, Upigaji picha mzuri na Uigizaji mzuri...mengine ni ziada lakini kama yanapatikana ni sawa.
Na kama kweli wanataka kukuza tasnia basi ni lazima nguvu iwekwe kwa Watayarishaji na sio Wasanii..kama ni kuwasaisia Wasanii basi wao ni kuwatafutia kozi za kuboresha uigizaji wao...Filamu bora zitatokana na Wazalishaji (Producers) Imara na wenye weledi...chini ya Mwamvuli wa Wazalishaji tutapata Waelekezi (Directors), Wapiga Picha(Cinematographer) n.k....Wasanii huajiriwa tu kwenye Filamu....sasa hapa kwetu ukisikia mikakati ya kuinua tasnia watawatafuta kina JB, Ray n.k....na kwa kiasi kikubwa huwa ni mikakati ya kisiasa zaidi kuliko kiuhalisia.
Nchi ikiwa na Vipaji vya kutosha swala la Elimu rasmi ya darasani sio tatizo kubwa ki hivyo kiasi kukwamisha mambo...ingawa tofauti ya ajabu niionayo ni kwa Mbongo akikwambia hajaenda shule ni tofauti na Chris Rock akikwambia hajaenda shule..Chris Rock au Dave Chapelle akisimama jukwaani kuongea hata unahisi labda angeenda hizo shule kivile angepoteza uwezo ule alionao.
Ushauri ninaodhani unaweza kubadilisha mtazamo wa tasnia ni kupokea damu changa zenye mawazo tofauti, damu changa zenye walau abcd za haswa nini maana ya kuwa Muigizaji...Damu changa waingie wakijua umuhimu na maana ya Screenplay/Script kwenye Filamu. Wakongwe tulionao wengi wanategemea uigizaji wa kuongea/kubwabwaja tu kama silaha yao kuu ya kuigiza ambamo ndani yake ndimo huficha udhaifu wao wa kuigiza...tutafute damu changa wenye vipaji waheshimu na wajue nidhamu ya Screenplay/Script..Filamu ni sanaa ya maonesho na sio ya kuelezea kwa maongezi tu.