Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Niliona sinema moja hivi wanaonyesha mhusika akikumbuka matukio ya mwaka 1990. Kituko ni pale mhusika anapanda Bajaj, gari lina namba hizi za sasa za T...
Nakubaliana na uzi huu.

Watu wanaweza wakadhani unatania Mkuu kumbe ni kweli
 

Unajua uigizaji unahitaji akili iliyochangamka, uwezo wa kumficha mtazamaji nini kinafuata, lakini bongo movies wao picha likianza tuu ukishaona baadhi ya wahusika tayari ushajua mwisho wa filamu
 
Tatizo mazingira ndy hayaruhusu, wataalamu wapo Changamoto ni mazingira wezeshi kwa hao wataalamu..

Mazingira gani hayo Boss?

Unajua Movies wanazoigiza hizi hizi kama zingeigizwa na watu wenye uwezo mkubwa zingekuwa tofauti kabisa?
 

πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Zinaibiwa kwa sababu wengi uwezo mdogo
 

Wewe mpaka sasa hakuna aliyeigiza filamu kisiasa, na hii ni kutokana hawana Idea na hayo mambo.

Hakuan filamu za migomo na maandamano,
Hakuna filamu za chuoni zaidi ya kudhani kuwa chuoni ni sehemu ya starehe kazi kuvaa nguo za uchi, ajabu sana hii
 
Hivi yule jamaa wa timamu movie mbona projects zake huwa hazifiki mwisho ? Kuna movie alikuwa anaitangaza tofauti na sema ila kabla project haijaisha analeta mpya nayo haifik mwisho

Sijajua Mkuu
 

Mitaji sio shida mkuu.

Hizo hizo filamu wanazoigiza mbona wanaigiza utumbo mtupu?

Shida ni shule Mkuu,
Mtunzi hana shule
Muongozaji hana shule
Mtayarishaji hana shule
Mchukua kamera hana shule
Waigizaji hawana shule unategemea nini hapo?

Hizo filamu zingine kama Siri ya Mtungi, Chumo zimeongozwa na watu wenye shule,
 
Ni kweli kabisa mambo mengi ambayo hata si ya kibajeti kiviile wanakuwa hawako makini nayo kama vile subtitle kwa lugha ya kiingereza wanachapia sana.

Embu angalia Series nyingi za Kikorea au Kifilipino Bajeti ni yakawaida, mazingira ni ya dailojia tuu lakini filamu zao zinakuwa nzuri, embu angalia Wanaijeria halikadhalika
 
Mkuu jinsi ulivyo tukandia sisi vilaza ni wazi kuwa unachuki nasisi na sio filamu. Kwa hiyo tulipokimbia shule na kuwaacha nyie majinias iliwauma eee? mlitegemea maisha yatuchape siyo?
 

Mkuu hizo hizo wanazoigiza zenye bajeti ndogo mbona hakuna wanachofanya.
Hivi unafuatilia filamu za kikorea au kifilipino?
Yaani kuna filamu ukiiangalia tuu ukiikadiria bajeti yake sio kubwa haina mambo mengi, lakini filamu inakuwa nzuri,

Haya niambie Kanumba aliwezaje?
 

Yaani mambo ya ajabu sana, yaani wale walinzi wa Suma Jkt ndio wapo hivyo?

Mtu na akili yake anawezaje muajiri mlinzi tahahira au comedy, sijui waliipata wapi hiyo
 

Shida ndio ilipo hapa,
 
Wasomi tunatamani sana kuingia humo tatizo wenyeji wana majungu, fitna, roho mbaya, chuki, husda na zaidi ulozi,

Tunaogopaaaa.

Soko lao litakuwa mashakani,

Embu angalia ile Movie ya The Dance aliyoigiza Irene Uwoya, Idea ilikuwa nzuri lakini Uwoya ile movie aliyumba hasa kwenye kipengele cha mawasiliano kwa kutumia kingereza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…