Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

movie zetu kuna ule utamaduni sijui nani kawakalilisha, watu wapo kwenye mazungumzo alafu kuna mdundo unapiga yan adi kero ata watu wenyewe hauwasikii unasikia beat tu.. mbona movie za ulaya zipo silence watu wanapoongea yaan unayasikia maneno murua kabisa
 
Sina hata iko kipaji cha kuigiza nimetoa tu maoni yangu
Ooh kumbe, okey Sawa ... hao ndugu zako wanatania, mbna kanumba alijitahd kupindua meza ?? Mbna Diamond kaipaisha bongo fleva , bongo movie kule hakuna wapambanaji Zaid ya wadangaji na akina super Mario wazee wa kujilamba midomo , kupaka piko na kutafta majimama ya kuwalea ...
 
Wewe mpaka sasa hakuna aliyeigiza filamu kisiasa, na hii ni kutokana hawana Idea na hayo mambo.

Hakuan filamu za migomo na maandamano,
Hakuna filamu za chuoni zaidi ya kudhani kuwa chuoni ni sehemu ya starehe kazi kuvaa nguo za uchi, ajabu sana hii
Wenzetu tukio likitokea haraka wanakaa.na kutengeneza movie lakini sisi story zetu ni zilezile kqma sio mapenzi ni uchawi matukio mengine hatuyaoni
 
Mtoa mada umeongea Jambo la mbolea Sana , nilifatilia CV ya Michael Scofield kwenye series ya Prison Break ,aisee jamaa mpak ana master's ya uigizaji , yaani kiufupi Tu Holywood huwez kupewa script kama shule ni zero kichwani.

Bongo movie hawana jipya Kwa sababu ni poor in education , hebu niambie kama kuna kipande cha kuiendesha ndege au meli nani atacheza ?.? Hata masuala ya ku-crack code za Mawasiliano hcho kipengele Nani atacheza ?? Wanabaki Tu na vitu normal kama Mapenzi , kuendesha vigali basi., na kufunguliana mageti huku wakiwaza
mbona nyalile yule aliegiza Gods must be crazy hana elimu yoyote na script alipewa na hollywood,,,,,Acheni ufala na vielimu vyenu uchwaraa hivyo muanze kuzalau walioishia kidato cha nne
 
Acheni ujinga watanzania wengi mnakawaida ya kutopenda vya kwenu inawezekana kweli kuna mapungufu kwenye bongo movie lakini si kwa ukubwa uo mnaoongela hapa,,,,,
Mtoa mada unaponda bongo movie alfu unakuja kusifia movie ya kihindi wewe ndo Bogaz kabisa wahindi wale mtu anapigwa ngumi anarushwa mita50 had anabomoa ukuta ule ndo uhalisia,,,[emoji15]
 
Mengi uliyoyaeleza yana ukweli. Maeneo mingi ya technical yanahitaji elimu, ila acting ni kipaji pamoja na bidii ya mtu. Elimu tupu haitoshi.
Kuwa na Master hakuwezi kukufanya uwe muigizaji bora, Huko Marekani hizo degree ni mambo ya kawaida mitaani kila mtu anazo tofauti ya huku kwetu wengi wetu ni form 4.
Kiufupi actor ni mtu anaetakiwa awe anajifunza Sanaa kila siku sio kuridhika alivyo. Tatizo kubwa la bongo movie hawajiongezi.
 
Wenzetu tukio likitokea haraka wanakaa.na kutengeneza movie lakini sisi story zetu ni zilezile kqma sio mapenzi ni uchawi matukio mengine hatuyaoni

Mkuu kutengeneza filamu sio jambo rahisi, bongo budget nalo ni tatizo sugu, shooting za open space nalo ni shida sana
 
Wakuu nani ana connection ya huyu Irene Uwoya? nina idea mbili tatu ningetamani nimfikishie
 
Acheni ujinga watanzania wengi mnakawaida ya kutopenda vya kwenu inawezekana kweli kuna mapungufu kwenye bongo movie lakini si kwa ukubwa uo mnaoongela hapa,,,,,
Mtoa mada unaponda bongo movie alfu unakuja kusifia movie ya kihindi wewe ndo Bogaz kabisa wahindi wale mtu anapigwa ngumi anarushwa mita50 had anabomoa ukuta ule ndo uhalisia,,,[emoji15]

Mkuu zile shangwe za kisanaa ambazo washabiki huzifurahia, kule kwao ukumbi wa sinema hujaa filamu ikiwa na mambo kama yale.
 
Shida wote wanataka kuigiza juu ya mapenzi tu.
Mkuu kiukweli kabisa film za mapenzi zinaelimisha sana na kitu kingine hujui nikwamba tuanaangalia tunaigiza maisha halisi ya waafrika na Tamaduni zao huwezi ukanambia nikaigize nimeshika mitutu ya bunduki wakati nchi yangu ni ya amani, mkuu right kungekuwa na kitufe cha kurekodi sauti hapa ningefunguka vziri
 
Himaya yangu nimehangaika nayo miaka nenda Rudi halafu From no where tu uje kuniaribia, lazima nikuroge ikiwezekana kukuua kabisa, hiyo ndo slogan ya bongo movie
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mweeeeh
 
Mkuu kutengeneza filamu sio jambo rahisi, bongo budget nalo ni tatizo sugu, shooting za open space nalo ni shida sana
Soko lenu mnaangalia wapi, mbona watu wa comedy kama mizengwe wanafanya vizuri, tatizo lenu mkiona mwanamke ana mvuto mnalazimisha aigize hata kama hana uwezo.
Chuo cha sanaa bagamoyo kuna watu waliofundishwa sanaa ya uigizaji vizuri ila mnawaacha mnakimbilia vilaza matokeo yake filamu zinakosa uhalisia
 
mbona nyalile yule aliegiza Gods must be crazy hana elimu yoyote na script alipewa na hollywood,,,,,Acheni ufala na vielimu vyenu uchwaraa hivyo muanze kuzalau walioishia kidato cha nne
Mkuu agiza bia naja kulipa
Unajua mtoa mada kasahau kitu kinaitwa kipaji wazungu wanaita talent kwa mf akina mhogo mchungu, Bambo, senga, dr Cheni, Kanumba kwasasa marehemu na wengineo ambao walikuwa kaole na walifanya vizuri sana kipindi kile na ukiangalia wengi wao vipaji viliwabeba ukiachilia mbali Mafunzo waliyopewa pale kaole

Kwakifupi nikwamba kitu kilichouwa Bongo movie ni Majungu ya watanzania na kutopeana sapoti imesababisha hii tasnia kushuka kwa kasi sana, kwa mf kuna mtu anaitwa Mussa Banzi siyo siri ni mtunzi mzuri sana wa stori na kuandika script, ukiangalia film kama Fungu la kukosa imebeba kila utamaduni wa mtanzania kwa asilimia zote, ukiangalia film kama Sikio la kufa nimoja ya film yenye maudhui ya kitanzania na nyingine nyingi ila huyu jamaa alishindwa kuendelea baada ya kampuni iliyokuwepo mwanzo kuacha kusambaza film kama unavyoona steps walivyoacha kawa kisingizio tasinia imekufa

Wasanii wa zamani walikuwa wanajituma kutokana na sapoti kutoka kwa watanzania.ilifika kipindi msanii akipita mtaani watu wote mnatoka kumuangalia yaani msanii aliheshimika sana, nakumbuka kiwewe alikatiza mtaani watu wote walitoka kumuangalia pia kingwedu alikua akikatiza mtaani ilikua ni taflani ukija kwa akina Kanumba ilikuwa kama rais kapita mtaani nahii yote ni kutokana na kile tuchokuwa tunakiona wanakifanya kupitia Runinga zetu

Kiufupi Bongo movie inahitaji saport hasahasa kutoka kwa watunzi mpaka kwa waigizaji pia tusiangalie sura kwani ilifika kipindi asipokuwepo Hemedi kwenye hiyo mvie eti hatuangalii na ikapelekea kila film awepo yule jamaa yaani akawa anawekwa mbele ya kava kabisa ili kuvutia naomba niishie hapa.
 
Soko lenu mnaangalia wapi, mbona watu wa comedy kama mizengwe wanafanya vizuri, tatizo lenu mkiona mwanamke ana mvuto mnalazimisha aigize hata kama hana uwezo.
Chuo cha sanaa bagamoyo kuna watu waliofundishwa sanaa ya uigizaji vizuri ila mnawaacha mnakimbilia vilaza matokeo yake filamu zinakosa uhalisia

Mkuu suala la acting ni uwanja mpana sana, kupasi vizuri chuoni hakukutoshelezi wewe kuwa ni muigizaji mzuri.
 
Back
Top Bottom