Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Bongo Movies wengi ni vilaza, si ajabu wameilaza sanaa ya uigizaji. Wasomi ingieni huko

Bwana Heriel umeongelea sababu moja tu kati ya nyingi inayosababisha kuwepo kwa hii hali. Sababu kubwa ya hali kuendelea kuwa hivi ni serikali yako kupuuzia hii tasnia na kutouwa serious. Bajeti za filamu kali ni mabilioni ya pesa huko Hollywood. Huyo kijana wa darasa la saba au hata aliyetoka chuo mwenye degree anapataje mamilioni ya kutengeneza filamu kali? Wakijitokeza wenye hela zao na kutaka ku-finance hawatawekewa zengwe la kodi kama zote na wengine kuanza kuambiwa ni watakatisha pesa? Hakuna fani yoyote duniani iliyoweza kukua bila mkono wa serikali. Pale DRC muziki wao ni mkubwa kwasababu serikali zao ziliwapa sapoti kuanzia ukoloni hadi leo. Hata ukiangalia Simba leo inafanya vizuri ni kutokana na hela kuwekezwa za kutosha. Acheni kuwalaumu tu wasanii bila kufikiria. Au basi waache hata hiyo fani wawe vibaka ndo mtaelewa.
Umetolea mfano wa simba kwani simba inapewa pesa na serikali.
Mtu anataka kuweka pesa akiangalia wasanii ndio hawa, story ndio hizi mapenzi, mapenzi hebu angalia hizi series za uko datv(maisha magic), na azam tv nyingi ni visa ni mapenzi na vinafanana lakini kiuhalisia mkuu mtaani story ni nying hususani hapa Tz kuna visa vingi tu mtu anaejielewa anaweza kutungia story. Achana na za mapigano hizo uwezo wetu bado hizi hizi za kijamii kwani marehemu kanumba ye story alikua anatoa wapi.

Kwasababu filamu zake zilikua na mapenzi kama part tu ya kukuza migogoro(lazma iwepo kwenye filamu) lakini sio hizi wadada series yote wamevaa nusu utupu wakati kibongo bongo sio uhalisia huo achana tu na utamaduni.
 
Mitaji sio shida mkuu.

Hizo hizo filamu wanazoigiza mbona wanaigiza utumbo mtupu?

Shida ni shule Mkuu,
Mtunzi hana shule
Muongozaji hana shule
Mtayarishaji hana shule
Mchukua kamera hana shule
Waigizaji hawana shule unategemea nini hapo?

Hizo filamu zingine kama Siri ya Mtungi, Chumo zimeongozwa na watu wenye shule,
Siri ya mtungi daah unaona kabisa hawa jamaa wana kitu aisee .

Na kuna short film niliangalia youtube zinaendana na siri ya mtungi kiuigizaji nadhani kuna shirika lilifadhili.

Em niielezee kidogo sababu ni story tu ya kawaida lakini wameigiza vizuri kama kweli vile. Ni story inayogusia masuala ya mwanamke kuachiwa afanye kilimo na kazi zote za nyumbani ilhali baba yeye ni kucheza bao tu ila wakati wa mavuno yeye ndo anaenda kuvuna kwa kutegea pia na kuuza kwa bei ya kutupa kwa uyo mnunuzi wa kijiji ambae ni mnyonyaji haswa.

Ni kisa icho tu lakini filamu inavutia haswa, waigizaji baadhi ni wale waliokua kwenye siri ya mtungi ebana jamaa wanajua nini wanafanya. Lakini ajabu ni kua wengi hawapo kwenye hizi series za sasa hata waliopo daah perfomance yao ni mbovu nadhani tatizo lipo kwa waongozaji wa hizi filamu huenda msanii anafata alichoambiwa na muongozaji.
 
Ni kwel tasnia ina mapungufu ,Ila habari ya make up artist kuishia darasa la pili ni ndo unaona jambo la kushangaza kwako mtoa thread? Je unataka mtu awe masters ndo akapake make up wasanii wakat ^makeup ni local knowledge inatolewa na collage za mtaani eg maznat collage.
Nawasilisha
Ndio maana mwaitwa vilaza, ukisikia make up unadhani ni kupaka poda tu, make up artist ni kipengele kikubwa sana, hizo movies za wenzetu uzionazo mfano za kutisha sio wote wanavaa masks au zamani tuliaminishwa ni computer, kuna wengine ni make up tu, mfano kaangalie movies za Guardians of the Galaxy, yule Drax mwili wake kua na michoro michoro vile ni make up ilipakwa 3 hrs, yule Gamora ile rangi ni make up pia, kuna Joker, na wasanii wengine wengi tu,

Usimchukulie poa make up artist katika kiwanda cha movie.
 
Mtoa mada umeongea Jambo la mbolea Sana , nilifatilia CV ya Michael Scofield kwenye series ya Prison Break ,aisee jamaa mpak ana master's ya uigizaji , yaani kiufupi Tu Holywood huwez kupewa script kama shule ni zero kichwani.

Bongo movie hawana jipya Kwa sababu ni poor in education , hebu niambie kama kuna kipande cha kuiendesha ndege au meli nani atacheza ?.? Hata masuala ya ku-crack code za Mawasiliano hcho kipengele Nani atacheza ?? Wanabaki Tu na vitu normal kama Mapenzi , kuendesha vigali basi., na kufunguliana mageti huku wakiwaza
Na siku hizi sijui wamegundua nini, cheating mwanzo mwisho, huyu kam cheat yule, yule kamcheat huyu wake na waume za watu.
 
Mazingira gani hayo Boss?

Unajua Movies wanazoigiza hizi hizi kama zingeigizwa na watu wenye uwezo mkubwa zingekuwa tofauti kabisa?
Mbona nilishaelezea ni masuala ya financial issues, ndy yanayopelekea hizo movie wanazofanya zisiwe na ubora...
 
Bongo movie nawapendea mahips na makalio makubwa..kaangalie Siri za familia..utafikiri Ni dangulo..yaani series nzima Ni kutuonyesha matako..miguu..mapaja na matiti yalivyobanwa ..yaani Ni upuuzi mtupu
 
NAAAM Kwa kiasi kikubwa nakubaliana na mleta mada kwamba bongo movie wamefeli sana...movie zao nyingi zimekaaa kimaudhui ya ngono ngono muda wote na pia hata cinematographic technique ni bure kabisa..editing bado .. kwa mfano unaangalia movie ghafla unaona hadi ile boom mic ya kurekodi sauti sio poa kabisa yaani.
 
Nakubaliana na wewe na pia napishana wewe mleta mada...

Ninapokubaliana nawe.
Utengenezaji wa filamu unahitaji watu wasomi kuanzia waigizaji, wapigaji picha na hata watengenezaji. Kama ilivyo tu kwa kada nyingine, kiwanda cha filamu kinakimbizana na teknolojia....

Ninapopishana nawe.
Kiwanda cha filamu kinahitaji uwekezaji mkubwa wa miundombinu na vitendea kazi ambapo sidhani kwa sasa kama watu binafsi wanaweza kutoa fedha nyingi kuwekeza...

Jaribu kutazama uwekezaji kama wa Hollywood ambapo kuna studios kama Disney, Paramount Pictures, Warner Bros, Universal Pictures au jaribu kutazama uwekezaji kama ule wa Tyler Perry na studios zake...

Mwisho wa siku unapata hawa ndugu zetu wanafyatua tu kazi zao kibongo bongo kama tu ambavyo mambo yetu mengine tunavyoyaendesha kibongo bongo...
 
Mkuu hizo hizo wanazoigiza zenye bajeti ndogo mbona hakuna wanachofanya.
Hivi unafuatilia filamu za kikorea au kifilipino?
Yaani kuna filamu ukiiangalia tuu ukiikadiria bajeti yake sio kubwa haina mambo mengi, lakini filamu inakuwa nzuri,

Haya niambie Kanumba aliwezaje?
Mkuu au atafute tu ile short film ya dk 1 "maybe another time " aone ni dk 1 tu lakini unakua thrilled.
 
Yaan wanatutisha, na hili Monalisa aliwahi lizungumzia kwenye kipindi cha Salama na Monalisa, wenyeji wanabana chances za wageni wenye uelewa wa darasani kwa maslahi yao,
Si dhambi kujifunza vitu vipya atii.

But kila kitu kina mwisho wake, Zama zinabadilika tunataka wasomi kwenye industry ya bongo movie , we have been entertaining non sense for so long , we want changes kwa kweli

Nikiangalia tamthilia zao Sijui jua Kali , Mimi Naona bado safar ni ndefu , uigizaji wa kishamba sana
 
Embu angalia Series nyingi za Kikorea au Kifilipino Bajeti ni yakawaida, mazingira ni ya dailojia tuu lakini filamu zao zinakuwa nzuri, embu angalia Wanaijeria halikadhalika
Mi nilijua watasingizi labda tecnology ukicheck series na vi movies za kifilipino hakuna TECNOLOGY sena mtiririko mzuri wa story unavutia mtazamaji.
 
Mkuu hizo hizo wanazoigiza zenye bajeti ndogo mbona hakuna wanachofanya.
Hivi unafuatilia filamu za kikorea au kifilipino?
Yaani kuna filamu ukiiangalia tuu ukiikadiria bajeti yake sio kubwa haina mambo mengi, lakini filamu inakuwa nzuri,

Haya niambie Kanumba aliwezaje?

Sasa mkuu ushasema bajeti ni ndogo watafanyaje kitu kizuri? Ushawahi kufanya production? Unajua Episode Moja ya SALAMANA ilikuwa inacost how much? Na ile show tu sembuse Movie?

Alafu unahisi leo wakaungana wolper, JB, Aunty Ezekiel, Rammy gallis, Ray na Gabo wakachukua bank loan wakachukua DIRECTOR WA KICHINA kuongoza na wakatengeneza bonge la BLOCK BUSTER ACTION film kama ile ya james Bond wanashindwa?

Ishu ni kuwa WATAUZIA WAPI? NA WATARUDISHAJE COST? Hayo masuala sijui ya madirector kukosa elimu ni propaganda tu . Huwezi kuniambia bongo hamna director mzuri na hata kama hayupo wameshindwa kukodi kutokea nje?

Ishu imekaa kimfumo mkuu. Yaaani nchi hata local theatres hamna na CCM ipo tu alafu mnataka muwalaumu wasanii?
 
Bongo movie kweli ni vilaza sana. Maisha yao yote hawanaga kabisa ubunifu wa aina yoyote kila siku theme yao ni mapenzi tu kila movie ni mapenzi tu yani mapenzi tu kila kona kumbaf zao.

Mara yako ya mwisho kuangalia bongo movie ilikuwa lini?
 
Back
Top Bottom