Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na kuenda kwa babu! 🤣Mtoa mada umeongea Jambo la mbolea Sana , nilifatilia CV ya Michael Scofield kwenye series ya Prison Break ,aisee jamaa mpak ana master's ya uigizaji , yaani kiufupi Tu Holywood huwez kupewa script kama shule ni zero kichwani.
Bongo movie hawana jipya Kwa sababu ni poor in education , hebu niambie kama kuna kipande cha kuiendesha ndege au meli nani atacheza ?.? Hata masuala ya ku-crack code za Mawasiliano hcho kipengele Nani atacheza ?? Wanabaki Tu na vitu normal kama Mapenzi , kuendesha vigali basi., na kufunguliana mageti huku wakiwaza
Hahaha.Mtu ameshika bastola halafu anasema nitakuchinja
Hawafahamu hayo mambo mkuu. Kuna movies zina very small ratings rotten tomatoes na metacritic lakini zimefanya vizuri kwenye soko na box office.
Hawafahamu haya mambo mkuu
Wewe ndio huna ujuacho kuhusu filamu, huko Zile zinazowekwaga Youtube Netflix ni nini yako?
Nimeshakuambia wekeni mfumo Youtube wa kurusha matangazo ya filamu zenu, mnazubaa zubaa kwa ukilaza wenu
Director ndio kila kitu katika movie industry anaweza kubadilisha hata scriptSidhani kama elimu ya waigizaji ndo tatizo maana kile ni kipaji. Tatizo ni directors na watunga hadithi. Unless mwigizaji ndo awe director.
😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂Mtu ameshika bastola halafu anasema nitakuchinja
Hao ndio walengwa wenu na ndio maana hamsongi mbele, Bollywood, Hollywood na Nollywood wanapotengeneza movie hawaangalii India, Marekani au Nigeria bali wanaangalia soko la dunia nyie mnaotafuta wadada wanaovutia soko lenu litaishia buza kwa mpalange lakini hata wao wakiona movie nzuri wataachana na bongo movieHivi unadhani mkaazi wa Buza au kwa mfuga mbwa ataanza kushuhulikia critics wanasemaje kuhusu filamu? yeye atakua na vivutio vyake yeye mwenyewe tu kama ni mshabiki wa actor Fulani, au wadada waliokuemo wanavutia, kaona filamu ina action au comedy ambazo yeye ndio anapenda.
Haha, Tommy n Jerry ni kali sana wewe! Pale akili na teknolojia kibao imetumika!Mimi siamini mpaka niione walahi,
Wanashindwa hata na Rango au Tommy na Jerry
Ndio raha ya movie ile, sio mtu apigwe ngumi 'tomato paste' itoke mdomoni, huo ni utopolo! 🤣 🤣 🤣Acheni ujinga watanzania wengi mnakawaida ya kutopenda vya kwenu inawezekana kweli kuna mapungufu kwenye bongo movie lakini si kwa ukubwa uo mnaoongela hapa,,,,,
Mtoa mada unaponda bongo movie alfu unakuja kusifia movie ya kihindi wewe ndo Bogaz kabisa wahindi wale mtu anapigwa ngumi anarushwa mita50 had anabomoa ukuta ule ndo uhalisia,,,[emoji15]
Sidhani kama elimu ya waigizaji ndo tatizo maana kile ni kipaji. Tatizo ni directors na watunga hadithi. Unless mwigizaji ndo awe director.
Director ndio kila kitu katika movie industry anaweza kubadilisha hata script
Hao ndio walengwa wenu na ndio maana hamsongi mbele, Bollywood, Hollywood na Nollywood wanapotengeneza movie hawaangalii India, Marekani au Nigeria bali wanaangalia soko la dunia nyie mnaotafuta wadada wanaovutia soko lenu litaishia buza kwa mpalange lakini hata wao wakiona movie nzuri wataachana na bongo movie
SahihiHapo ndipo kwenye point wakuu, matatizo ya filamu za bongo yapo kwenye utengenezaji, Directors na crew wao. kuwashutumu ma actors ni kutafuta kichaka cha kutoa matusi tu ila wao ni sehemu ndogo tu ya tatizo.
Mleta mada alikuja na hoja za kuwatolea povu ma actors kuwa hawana elimu hawajafika chou hapo ndipo nilipoanza kumpinga mimi.
Dah mkuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]BONGO MOVIE WENGI NI VILAZA, SIO AJABU WAMEILAZA SANAA YA UIGIZAJI.
Anaandika, Robert Heriel.
Hapana shaka sanaa ya Uigizaji kwa sasa imelala Usingizi wa Pono, imelala fofofo na waigizaji wake wanakoroma. Wapo kwenye ndoto za majinamizi wabaya wanaowakimbiza kwenye mitaro huko usingizini. Tangu kifo cha Marehemu Kanumba miaka zaidi ya tisa iliyopita Tasnia ya Bongo Movie imelala fofofo.
Hakuna Tasnia inayoongozwa na Vilaza isilale, sijawahi kuona popote pale duniani. Bongo Movie imejaa wasanii vilaza kwa kiwango kikubwa sana, watu waliokimbia shule ndio wamekimbilia huko kwenye tasnia ya filamu. Embu fikiria mtu amekimbia shule kwa kushindwa somo hata la kiswahili unafikiri atatuambia nini kwenye suala la kuelimisha jamii kupitia fani ya uigizaji.
Kilaza ni kilaza tuu, uwezo wake wa kufikiri ni mdogo alafu anakuwa Director wa filamu, unafikiri filamu yake itakuwaje kama sio Utopolo. Kilaza hufikiri mambo chini ya kiwango, ukiwaangalia wasanii wengi wa bongo movie wakiigiza kwanza hawawezi kuuvaa uhusika, wanachojua ni kutoa macho, kukenua, kubinua makalio, kuvaa nguo fupi, wakati kwa upande wa wasanii wa kiume wanachjua ni kupaka piko sijui waves nywele zao, kutoboa masikio au kubandika stiker masikioni, na kulamba lamba midomo kama sio kusuka nywele. Kwa mambo haya wamefuzu kwani mambo haya hufanywa kwa sehemu kubwa na vilaza, kwani hata mtu asiye msanii anaweza kufanya mambo hayo. Vilaza hufanya mambo ambayo mtu yeyote anaweza kufanya.
i/ Muongoza Filamu alifeli shule, akaunga unga wee akapata cheti, huyo akajiingiza kwenye Tasnia ya Filamu, haya embu niambie atatupa kipi cha maana hapo?
ii/ Mtayarishaji alifeli shule, akaunga unga wee, embu niambie ataleta jambo gani katika ulimwengu huu wa elimu, sayansi na teknolojia?
iii/Mchukua Kamera alipata sifuri au four ya mwisho kabisa, hivi unategemea atakuwa na ubunifu gani kwenye masuala ya kurekodi picha na video na kamera?
iv/ Mtia sauti, aliishia kidato cha nne, embu niambie anauelewa gani na mambo ya sauti, muziki na ala? Sio ajabu sauti nyingi zinazoingizwa kwenye movies nyingi ni zile zile haziendani na uhalisia,
v/ Mtu wa Makeup aliishia darasa la pili, hivi anajua nini kuhusu urembo? Kama utabisha angalia filamu zetu kisha angalia za wenzetu kama wanaijeria utaelewa.
vi/ Mtu wa simulizi, aliishia darasa la saba, hivi unafikiri uwezo wake wa kufikiri, na uelewa wa mambo ataandika script ipi yenye kufanya kizazi cha sasa kukubali kisa chake
Shida kubwa ya Wasanii wa Bongo Movie ni elimu ni ndogo sana kwa wengi wao, wengi ni Slow Learner, wachache sana wanauwezo mkubwa wa kiakili, kufikiri na kuchambua mambo. Wengi wao ni bora liende nao wawemo.
Ukitaka kujua kuwa Wasanii wetu wengi wao ni Vilaza basi angalia Role Model wao waliopo ughaibuni kama Marekani, bado ni wale wale waliokimbia shule, watu wenye Skendo, wavaa uchi, watumiaji wa madawa ya kulevya, na wahuni walioshindikana.
Bongo Movie ikataka iinuke iache kuchukua Vilaza, slow Learner watu waliokimbia shule ambao kimsingi lazima wawe na akili finyu na kazi zao lazima ziwe duni.
Waigizaji wengi wa Nigeria, Ghana, South Afrika wana elimu Degree moja kuendelea, yaani ambao hawajasoma ni wachache sana ukilinganisha na wenye shahada. Ndio maana wanajua kile wafanyacho. Embu angalia filamu na tamthilia za Kikorea ambazo kwa sasa zinateka soko hapa nchini, waigizaji karibu wote wa Kikorea ni Wasomi wa elimu ya juu kabisa kuanzia Degree tena nyingine ni zile za moto. Njoo kwa Wahindi, wafilipino, na kule Amerika ya kusini, waigizaji karibu wote ni wasome wa elimu ya juu kabisa.
Mtu mwenye elimu ya uhakika sio ile elimu ya kuunga unga kwenye vyuo visivyoeleweka hawezi kutoa kazi mbovu.
Naipongeza serikali kwa kuanzisha michepuo mipya itakayoendana na mambo ya sanaa na Lugha ili kufufua Tasnia ya Filamu hapa nchini.
Mtu kaishia Darasa la saba au kidato cha nne, atajuaje na kuigizaje mambo ya Ujasusi wa kidola na kiuchumi yaani ataanzia wapi?
Mtu madarasa hayamtoshi, ataweza kuigiza filamu za kisiasa, ugaidi, na masuala ya demokrasia? Atawezaje ikiwa hajui hata historia ya hiyo demokrasia yenyewe zaidi ya maneno ya mtaani na vijiweni.
Mtu kaishia kidato cha nne atawezaje kufikiria kuandaa scripts ya mambo ya Mpango wa dunia wa milleniam, atawezaje kuigiza Umuhimu wa vyama vingi vya siasa ndani ya nchi?
Mtu kaishia kidato cha nne kwa kulazimishwa, atawezaje kuigiza filamu ya masuala ya sheria na haki za binadamu, hajui hata katiba ya nchi yake, mtu kama huyo huoni ni jipu?
Mtu kaishia kidato cha nne, atawezaje kuandaa filamu ya athari ya udikteta na ukosefu wa uhuru wa kujieleza ndani ya jamii,lini atawaza hayo, yeye kama sio kuwaza mapenzi tuu muda wote?
Mtu kaishia darasa la saba au kidato cha nne, atawezaje kufikiri hata kuigiza filamu inayopromoti utalii wa nchi yetu, utashangaa licha ya nchi yetu kuwa na Mbuga na vivutio vingi lakini tangu tupate uhuru hakuna filamu ya wanyama iliyochezwa na wabongo, utashangaa. Ndio shida ya vilaza hiyo. Wenyewe watakuambia uchumi mgumu.
Mtu anaelimu ya kuunga unga, atawezaje kuigiza inayozungumzia masuala ya fani za kitaalamu kama vile Ualimu wenyewe sio ule wa kuigiza kama wanaoigiza watoto kibaba baba na kimama mama. Au udaktari, au sheria, au injinia, utawezaje igiza kitu hukijui na huna akili ya ku-master kwa upesi.
Mimi nawashauri wenye nafasi na wanaotaka Bongo Movie iamke basi wafanye haya;
Wasajili watu wenye vipaji Fresh from the School, waende shule zenye vipaji huko, Vyuo vikuu vinavyotambulika wachukue watu huko.
Wasaniii wawekewe sheria kuwa ili uwe mwigizaji basi yakubidi uwe na elimu isiyochini ya Diploma. Na uwe umefaulu vizuri kidato cha nne
Tasnia inapoongozwa na Kilaza kamwe haiwezi kuzaa matunda chanya kwenye jamii.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Sumbawanga
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Mtoa mada umeongea Jambo la mbolea Sana , nilifatilia CV ya Michael Scofield kwenye series ya Prison Break ,aisee jamaa mpak ana master's ya uigizaji , yaani kiufupi Tu Holywood huwez kupewa script kama shule ni zero kichwani.
Bongo movie hawana jipya Kwa sababu ni poor in education , hebu niambie kama kuna kipande cha kuiendesha ndege au meli nani atacheza ?.? Hata masuala ya ku-crack code za Mawasiliano hcho kipengele Nani atacheza ?? Wanabaki Tu na vitu normal kama Mapenzi , kuendesha vigali basi., na kufunguliana mageti huku wakiwaza
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna siku nliona Daktari wa bongo movie akisema "presha iko sawa, maleria pia iko sawa...." Nikatoka nje make nlikua kwa watu ningekua kwangu ningezima tv.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]..Yule jamaa Idrisa Sultan alianza kujitahidi kuweka mambo sawa.....hakuna kitu inakera na wakati huo huo kuumiza kama kuangalia bongo movie...hakuna uhalisia hata kidogo.....kwa Bongo movie siku zote Gateman lazima awe kama taahira fulani hivi..sijui wamejifunza wapi?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mi nilishangazwa marehemu kafa wakamzika na suti eti mzimu wake unakuja na KIPENSI alafu umepakwa masizi na chaki...mama.eee walahi