Bongo Nyoso mtu ana Certificate ya Clinical Officer anajiita Daktari (MD)

Nje ya miji au vijijini hao wanaitwa daktari tena Kwa mbwembwe zote.
 
Usipojua tofauti zao utafanyiwa malpractice uanze kulialia madaktari wabaya, kumbe nesi au mtu wa maabara kaharibu. Mnaishi kama sokwe nyani tu.
Nipo Hospital kwa miaka 14 sasa.Nimeandika kirahisi rahisi mno ili ieleweke.
 
Mfano ukiulizwa, clinical officer, assistant clinical officer, assistant medical officer utawaitaje kwa kiswahili? ( Nadhani kiswahili hakina maneno mengi hivyo tunawaita wote ni madokta tu)

Pia watu wa maabara na wafamasia sijui kwa nini ili imekaa kushoto kuwaita ( mfamasia, mtaalamu wa maabara) mwisho tunawaita madaktari tu

Kimsingi mazoea ndio yanatufanya tuwaite hivyo
 
Wanaitwa sio wanajiita ndugu, Rabies ni pale ule ufafanuzi kuwa huyu ni Tabibu na huyu Daktari wakati wote wanafanya kazi ile ile ya consultation and treatment,, wagonjwa na walimwengu hawana huo muda wao wanawaita wote madaktari na dawa zinazoandikwa ni zile zile na watu wanapona tu.
 
Sio nchi zilizoendelea au zenye mipango endelevu. Huo ujinga wa kucheza kamari sio kila mtu anaweza. Mtabaki kila siku kusema kazi yake Mungu pale mochwari. Yani operation ya jicho, lazima nijiridhishe na qualifications za huyo mtu. Madaktari wanakuwa smart , wana business cards, ata ukigoogle tu unampata. Ndio nije nijikabidhi kwa mtu ata form 4* tu misukosuko. Nyie ndio maana mnapiga ramli bado. Kamari hiyo siwezi milele.
 
Nimechekaa, πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hata madaktari wanajiita waganga wafawidhi au waganga wa mikoa

Kila anayetibu ni dokta
 
Daktari ni Daktari tuu awe na cheti(astashahada), Diploma(stashahada) au Degree(shahada)

Ni sawa na Mwalimu, awe wa chekechea, msingi, secondary, au chuo. Mwalimu ni Mwalimu. Hizo za kusema sijui mhadhiri, sijui mkufunzi ni Mbwembwe.

Halikadhalika na fani zingine
 
Wewe ndio zwaziwa,cheo cha udoctor Kipo mpaka kwenye dini na Business,wapo Doctor of Business Administration.Zwazwa kubwa lao wewe.Wapo PHD(Doctor of Phylosophy.
Imekugusa kinyeoni sio🀣
 
Kwani mganga mwenye diploma yeye anatakiwa aitweje? Ni kosa kumuita Daktari? Je, Kwa kawaida anapaswa aitweje?
Kwa mfano, kwenye ualimu, mwalimu wa shahada na mwalimu wa diploma wote huitwa Walimu. Tofauti ipo kwenye vyeo. Utakuta mwingine ni mwalimu mwandamizi daraja la pili. Mwingine mwalimu daraja la pili n.k japo wote wanatambulika kama Walimu. Sasa huko kwenye udaktari pakoje???
 
Sahihi mkuu ni issue ya mazoea ya kimatamshi..lakini Haina haja kuwa attack sababu kwenye issue ya majukumu wanatekeleza yanayowahusu kwa professional zao tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…