Bongo Plus na Uchaguzi Mkuu 2025: Wanatafuta Historia ya Vijana wa Kale na Vijana wa Leo Katika Siasa
Leo Maktaba ilitembelewa na Mtangazaji Victor Madaha wa Bongo Plus kutafuta historia ya vijana katika siasa kuanzia kudai uhuru wa Tanganyika hadi leo.
Victor anasema kasukumwa kwa kuona wimbi kubwa la vijana kuingia kwenye kinyang'anyiro kuwania nafasi za uongozi katika taifa kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu.
Kwa ajili hii angependa kusikia hali ilikuwaje kwa vijana wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nilimchukua Victor kwenye safari ya vijana waliokuwapo miaka ya mwanzoni 1924 wakati Dr. Kwegyr Aggrey alipofika Tanganyika akakuta Waafrika hawana chama chochote kuwaunganisha.
View: https://youtu.be/bX-WREAAGG8