Bongo Zozo ni nani na amefuata nini Tanzania?

Bongo Zozo ni nani na amefuata nini Tanzania?

Kuna mwingine nae ni muingereza kama bongo zozo na yupo hivyo hivyo, Ana kichapa kiswahili ipasavyo kuliko ata bongo zozo

Kwa Sasa namuona mitandaoni akiwa mapumzikoni zenji

Anajiita Jesse.
Anakitwanga kiswahili vizuri sana.
Anadai ana muda mrefu TZ, aliishi sana mkoa wa Mara akifanya research juu ya ukeketaji.
 
Nisicho kipenda toka kwake ni maudhui yake tu!
View attachment 2795079
Ubaya wa hii Video ni nini?

"Any doctor will tell you the great mental & physical damage that results when a person has bitterness or hatred in his heart. It is a poison of the worst sort. Only a fool will allow himself to be a victim of bitterness or hate"

- Archie Moore
 
Hakunaga mzungu anaeweza kulipenda taifa jingine lazima alifedheheshe taifa tu
"Any doctor will tell you the great mental & physical damage that results when a person has bitterness or hatred in his heart. It is a poison of the worst sort. Only a fool will allow himself to be a victim of bitterness or hate."

That's true chief
 
Ni muingereza ambaye alizaliwa Zimbabwe, na wazazi wake ambao walikuwa waloezi huko Zimbabwe lakini walirudi kuishi Uingereza wakati Bongozozo akiwa baado mdogo...

Uhusiano wake na Tanzania ulianza pale Bongozozo alipoamua kutaka kuja kuishi Afrika pindi alipomaliza elimu ya chuo, bara alilozaliwa na "asili ya pili ya wazazi wake".

Akaishia kuja Tanzania hatimaye mkoani Iringa sababu ya hali ya hewa yenye ubaridi mwanana, na mwanzo alipanga aishi kwa muda mfupi lakini akajipata anaishi miaka 18 na kuoa mwanamke wa Kitanzania mwenye asili ya Kichaga huko huko Iringa na baadaye akahamia Moshi...

Kwa mtu aliyeishi Tanzania kwa miaka 18, mahali ambapo ni ukweni kwake na nchi ya mke wake hivyo it's a no brainer kutokuwa na mapenzi na Tanzania...

Hata watoto wake haswa mtoto wake wa kiume, huwa anawatambulisha kama Watanzania na mwanaye huyo ambaye hushiriki shughuli mbalimbali za kimichezo huwa anaiwakilisha Tanzania kwenye events ambazo sio official haswa riadha...

Kitaaluma jamaa ni kocha wa mpira wa miguu kwa kusomea. Lakini pia huwa anasema yeye ni youtuber...

Nimeandika kwa mujibu wa mahojiano ambayo nimewahi kumsikiliza na kusoma akielezea historia yake...

Wenye kujua zaidi wataandika zaidi...
Mwamba anatumia jina lenye kufikirisha sana, kuna kitu cha hatari sana kimejificha nyuma ya pazia kwa huyu jamaa
Ameoa na Kuzaana Mwanamke wa Kitanzania, Mkewe ni Mchaga.

Yeye ni Raia wa Uingereza

Ni mapenzi tu aliyonayo kwa Tanzania kama nchi ambayo amewahi kuishi na kubahatika kupata Mke.

Bongo Zozo ni trader, ni mmoja wa "Early Adopter" wa Bitcoin na Cryptocurrency lakini pia ni Collector wa Coins haswa zile za Zamani. Kwa wenzetu watu aina ya Bongo Zozo wanaitwa "Digital Nomad" hajaajiriwa na mtu yeyote yule, mtaji wake mkubwa ni Laptop yake na uwepo wa mtandao wa internet sehemu yoyote atakayokuwepo kwani shughuli zake za kumuingizia kipato zinahitaji vitu hivyo kama vitendea kazi.

Asante.
Mpaka hapo nshapata kitu, something like "Money laundering" inakuja na kupotea kichwani kwangu.
REJEA: GOLD MAFIA by AL JAZEERA
 
Mwamba anatumia jina lenye kufikirisha sana, kuna kitu cha hatari sana kimejificha nyuma ya pazia kwa huyu jamaa

Kwa mujibu wake, neno "zozo" kalitoa toka lugha ya kishona, likiwa na maana ya chaos au fujo...ndio mwanzo mwa slogan yake ya fujo zisizoumiza
 
Watanzania wanapenda sana kufuatilia maisha ya watu wa kawaida wanasahau kufuatilia viongozi wao wenye nyendo za kutilia shaka.

Hili taifa linalaana.
 
Mpaka Huwa nahisi utumwa Bado upo. Isije ikawa huyu mwamba ni missionary kama wale waliikujaga enzi za utumwa [emoji134][emoji134][emoji134]​
Vasco da gama [emoji38][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Kwanza natanguliza hoja kwamba sina chuki yoyote na huyo jamaa kwa sababu hata silijui lolote linalomhusu bali pia nampongeza kwa kuhamasisha morali ya wachezaji wa Taifa Stars kwa kuhudhuria kwake mechi zao hata zile zinazopigwa nje ya nchi.

Leo ameshinda tuzo ya mhamasishaji bora wa msimu wa Tuzo za ligi iliyopita ya Vodacom (Maajabu), maana huyu yeye alikuwa Mhamasishaji wa Timu ya Taifa tu sijui huku kafikaje ila siyo kesi maana aliwahi hata kuitwa kwenye bunge la Tanzania na kupongezwa.

Swali langu ni hili, huyu jamaa ni nani katika soka la nchi hii na kwa vile nchi hii haina Uraia pacha amefuata nini?
Bongo zozo ni Mwingereza aliyezaliwa Zimbabwe, akakulia Mkoa wa Iringa, akaenda kuishi kama raia Uingereza. ameoa mchaga na wana watoto wawili.
 
Anajiita Jesse.
Anakitwanga kiswahili vizuri sana.
Anadai ana muda mrefu TZ, aliishi sana mkoa wa Mara akifanya research juu ya ukeketaji.
huyo amekulia Iringa, anaongea hadi Kihehe
 
Mwamba anatumia jina lenye kufikirisha sana, kuna kitu cha hatari sana kimejificha nyuma ya pazia kwa huyu jamaa

Mpaka hapo nshapata kitu, something like "Money laundering" inakuja na kupotea kichwani kwangu.
REJEA: GOLD aMAFIA by AL JAZEERA
Badilika Mkuu,
aMwamba anatumia jina lenye kufikirisha sana, kuna kitu cha hatari sana kimejificha nyuma ya pazia kwa huyu jamaa

Mpaka hapo nshapata kitu, something like "Money laundering" inakuja na kupotea kichwani kwangu.
REJEA: GOLD MAFIA by AL JAZEERA
Punguza ujuaji na kuchanganya Mambo. Bongo zozo ni mjasiriamali wa kidigitali ambae anaishi maisha huru, hajaajiriwa na mtu wala taasisi yoyote ile. Na watu wa aina yake siku hizi wapo wengi tu. Dunia imebadilika sana saivi. Ni vizuri ukijifunza vitu usivyovijua kuliko kuwa mjuaji na mitazamo hasi katika mitindo ya maisha ya watu wengine usiyoijua.
 
Ni fikra zako.
Vile unavyowaza na kufikiria usinifundishe nami niwaze na kufikiria kama wewe. Nimewaza vile nilivyowaza na kuunganisha dots kwa haraka zaidi na pia kwa ufupi zaidi unyasikia maisha yake ya nje kupitia mitandao, maisha yake ya ndani huyajui.
REJEA; DEEP STATE.
 
Mtazamo wangu wa maisha hautegemei Documentaries, Movies na Videos za youtube, Nayazungumzia maisha kwa vile ninavyoyajua kwa uhalisia wake. Wewe umemfahamu Bongo zozo leo hii sie wengine tunamfahamu tangu enzi hizo hajaanza kuuza sura mitandaoni. Hana jambo lolote la kutisha zaidi ya yeye kuwa raia tu wa kawaida na mjasiriamali wa mtandaoni. Tatizo lenu wabongo mtu kuwa mjasiriamali basi lazima awe na frame kariakoo au alime na kufuga kuku.
 
Back
Top Bottom