Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo akirushiwa kwa Wananchi wenye hasira kali sekunde 10 nyingi kashatakata haraka sanani kweli inatakiwa kupata maumivu lakini inabidi kwanza tujue nani anamtuma unajua mara nyingi
pale wengi hushoshea kidole kuwa ni pale pengine sio pale kumbe ni hapa
Imeandikwa usimshuhudie jirani yako uongo. Usemayo ni kweli na unaweza thibitishaaa?View attachment 3094522View attachment 3094523
Mamlaka hazimwezi , wakuu wa usalama wote wana mwogopa ! Mikono yake inaoga damu kila baada ya mda mfupi !!
Sativa ahakikishe Yuko sehemu salama vinginevyo watamtafuta na kumuua tena....Mheshimiwa Rais ZCO ACP FAUSTINE MAFWELE AHOJIWE KWA TUHUMA ZA KUTEKWA NA KUPIGWA RISASI YA KICHWA SATIVA.
1. Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
2. Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Hamad Masauni.
3. Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Mongoso Wambura
4. Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma
5. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob Nkunda
6. Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, DIGS, Suleiman Mombo
7. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Hamza Johari1.
Mheshimiwa Rais, Wakati huu nchi ikiwa katika taharuki kubwa na sintofahamu ya watu kutekwa na kupotea kwa watu kisha mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Makao Makuu, Ali Muhammad Kibao Niruhusu nimlete kwenu mtumishi wa serikali na afisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ACP Faustine Mafwele katika tuhuma za Mtanzania Mwenzetu Edger Edson Mwakabela (SATIVA).
Mheshikiwa Rais, napenda kukukumbusha kwamba, Edger Edson Mwakabela (Sativa) kijana ambaye alitekwa 23 June 2024 na kupatikana 27 June 2024 akiwa amejeruhiwa na risasi ya kichwa katika mapori ya hifadhi ya Taifa ya katavi, Mkoa wa Katavi na baadae RAIS ukamchangia matibabu ya jeraha la risasi kiasi cha Tsh Millioni 30.
Mheshimiwa, Rais Edger Edson Mwakabela kwa sasa amepona na hana itilifafu yoyote ya kumbukumbu wala akili pamoja na kupitishwa na katika madhira makubwa ya ukatili mbaya sana dhidi ya binadamu.4. Mheshimiwa Rais, 27 June 2024 Edger Edson Mwakabela akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Mkoa katavi alihojiwa na gazeti la Nipashe kwa njia ya video https://facebook.com/share/v/BJFfk7G2iBrXYbCP/?mibextid=oFDknk
Katika mahojiano hayo SATIVA anasema kwa kumbukumbu kuwa alitekwa Jumapili usiku na kupelekwa katika Karakana ya Kituo cha Polisi Oysterbay na siyo kituoni ndani kabla ya kusafirishwa kupelekwa Mkoani Arusha na baadae Katavi.
Mheshimiwa Rais, kwa muda wote huu Edger Edson Mwakabela alishahojiwa na Jeshi la Polisi na baadae walipotaka maelezo ya nyongeza Edger Edson Mwakabela alikuwa katika upasuaji katika hospitali ya Aga Khan. Mwezi August Edger Edson Mwakabela aliwataarifu Jeshi la Polisi kuwa tayari ameondolewa vyuma vya taya na sasa yupo tayari kwa mahojiano na Jeshi la Polisi, akawauliza, Je, afike kituo gani na muda gani kwa mahojiano? Kwa masikitiko makubwa Jeshi la Polisi kupitia Afande James wa kutoka Ofisi ya DCI - Dodona, alimjibu kuwa watamtafuta kwa mahojiano siku wakipata nafasi na mpaka leo Jeshi la Polisi halijawahi kupata nafasi ya kumuhoji Sativa.
Mheshimiwa Rais, 21 August 2024 baada ya kupotea Vijana watatu wanachama na Viongozi wa chadema Godwin Mlay, Deusdedith Soka na Frank Mbise Watanzania walianza kusambaza watu wanaowatuhumu kwa matukio ya kuteka watu kutoka katika vyombo vya dola, mmoja ya watu ambao picha zao zilisambazwa alikuwa ni ACP Faustine Mafwele.
Mheshimiwa Rais, Kijana wako Edger Edson Mwakabela alipo iona picha ya ACP Faustine Mafwele, 22 August 20224 alitutaarifu watu wake wa karibu ikiwamo mimi, kuwa mtu yule ambaye picha yake ilikuwa ikisambaa mitandaoni ndiye alifika nje ya Kituo cha Polisi Oysterbay usiku wa Jumapili ya 23 June majira ya Saa 2:00 kuelekea majira ya Saa 3:00 usiku. Na kwamba ACP Faustine Mafwele alimuhoji Edger Edson Mwakabela maswali matatu 1. Unaitwa nani 2. Unafanya shughuli gani 3. Unajua kwanini upo hapa..?Baada ya mahojiano hayo mafupi ACP Faustine Mafwele aliwafuata watu waliomteka Edger Edson Mwakabela na kwenda kuongea nao mazungumzo ambayo Edger Edson Mwakabela hakuyasikia, kilichofuata hapo ni watu wengine kufika muda kidogo wa baadae na kuanza naye safari ya kwenda Arusha na baadae Katavi walipoenda kutekeleza mauaji waliyopanga.
Mheshimiwa Rais, upo uthibitisho wa Kieletroniki wa Edger Edson Mwakabela kuwepo eneo hilo siku ya Jumapili ya tarehe 23 June 2024 majira ya 2 na Dakika 45 usiku. Kwa bahati mbaya watekaji wa Edger Edson Mwakabela walisahau kuzima simu yake namba 0757637880 wakati wote waliokuwa nayo tangu wamteke eneo la Kimara Korogwe.CDR (Call detail Records) ya simu ya Sativa namba 0757637880 inaonyesha kuwa simu yake iliendelea kupigigwa na kupokea meseji ikiwa eneo la Kituo cha Polisi Oysterbay kwa uthibitisho wa mnara aliokuwa anapokelea mawasiliano pamoja na simu yake kusomeka kwa Latitude na longitude za CDRBila shaka kwa kupitia CDR ya simu namba 0757637880 ya Edger Edson Mwakabela hakuna wasiwasi kuhusu tuhuma kuwa Edger Edson Mwakabela kufikishwa eneo la Oysterbay.
Mheshimiwa Rais, Kijana wako Edger Edson Mwakabela ndiye mtu pekee ambaye amewahi kwenda Kuzimu na kurudi (survivor). Ni mtu pekee aliye hai mwenye ushahidi juu ya nani anatoa amri za watu kutekwa, anashirikiana na kina nani kuteka na wanaoteka wanafananaje na mwisho wanaoteka na kwenda kuua wanavyofanya kazi yao kwa uaminifu. Liwekwe graride la Utambuzi, Kijana Edger Edson Mwakabela amtambue ACP Faustine Mafwele. Huyu ni ZCO kanda Maalum ya Polisi, Dar es Salaam.
Mheshimiwa Rais, ndiyo maana unaona kila Mtanzania anakupinga unaposema unasubiri kuletewa report juu ya matukio ya utekaji na mauaji kutoka kwa Jeshi la Polisi au vyombo vya dola wakati viongozi wakubwa wa Jeshi la Polisi ni sehemu ya watuhumiwa wa kazi hii chafu ya utekaji na mauaji. Je watakuletea report gani kama na wao ni watuhumiwa..?
Mheshimiwa Rais, kwakuwa tunaye tayari mtuhumiwa mmoja wa kuanza naye ambaye ni ACP Faustine Mafwele ambaye bado yupo ofisi za umma anatoa amri na anaendelea na usimamizi wa vikosi vya serikali;
1.Tunaomba ahojiwe Edger Edson Mwakabela haraka sana
2.Tunaomba ahojiwe ACP Faustine Mafwele haraka sana
3.Tunaomba ubatilishe uamuzi wako wa sisi wasamaria wema wenye taarifa kupeleka raarifa za utekaji na mauaji kwa Jeshi la Polis.
Badala yake tunaomba uunde tume huru ya Kijaji itakayo kusaidia kubaini ukweli na kukuletea taarifa Juu ya tatizo la utekeji na mauaji ya watu. Ahsante kwa ushirikiano wako.
Boniface Jacob
Ex-Mayor, Kinondoni & Ubungo.
0712 239 595
The voice of the silenced Majority
Pia soma: Alichosimulia Edgar Mwakabela "Sativa" kuhusu waliomteka na kumpiga Risasi ya Kichwa
Hakuna cha siri ni kwamba Sativa kamwaga ugalihapa zinaongea codes tu kama sio usalama wa taifa hutaelewa ata kidogo
Hawanusi hata harufu ya petrol hawa nyenyere asee, naona wanajisogeza kwenye tanuru kupitia uzi uliounganishwa hadi kule bondeni!.Uoga wa sisimizi tunaujua wakiona wenzao kadhaa wamemwagiwa majivu ya moto hutawanyika na kurudi kwenye mashimo yao, sahivi anaangaliwa aliembele ya wenzake ni nani majivu yaanze kumwagiwa kwake
Askari anapokea amri. Akiambiwa acha anaacha, akiambiwa mshughulikie anakushughulikiamzee inaonesha ni mtu wa kuogopwa sana
lakini natamani kujua upande wake wa pili kwanini alifanya hivi au kwanini hufanya hivi
kamwaga ugali kivipi ....mi naona ni kama kuna mpunga dogo kachezea hili jamaa ajulikane maboss waendelee kukaushaHakuna cha siri ni kwamba Sativa kamwaga ugali
kiufupi sisi ni wanaumeAskari anapokea amri. Akiambiwa acha anaacha, akiambiwa mshughulikie anakushughulikia
Umefikiri vyema japo hakuna uhakika wala ushahidikamwaga ugali kivipi ....mi naona ni kama kuna mpunga dogo kachezea hili jamaa ajulikane maboss waendelee kukausha
Anajiamini sanaaa..... Hapo pengine ngoja kwanza 😹Mie namtaman anavyojiamini...yaan nawazaga mbaalii😉..raha sana mwanaume anayejiamini ujue...
Hii sura imekaa kinyarwanda kabisa.View attachment 3094522View attachment 3094523
Mamlaka hazimwezi , wakuu wa usalama wote wana mwogopa ! Mikono yake inaoga damu kila baada ya mda mfupi !!
Sativa alishakufa, huo ni mzimu wakeSativa anafanya makosa mengi yasiyo ya lazima ambayo yanaweza kumgharimu.
Sura yake tu inasadifu kwamba huyu ni mtu hatari Sana. Muuaji Katili having a devilish face.View attachment 3094669
Jina: Faustine Jackson Mafwele
Umri: miaka 47
Kabila : Mkerewe
Dini: Mkristo
Makazi : Mikocheni
Kazi: Afisa mwandamizi wa polisi
Cheo: Kamishina Msaidizi wa Polisi
Madaraka: Zonal Crime Officer
Tuhuma: Kuendesha genge la uhalifu dhidi ya binadamu.
Mawasiliano: +255 755 855 743
+255 787 922 913
1. ACP Faustine Mafwele kwa mara ya kwanza amethibitishwa hadharani na kutambuliwa na Edger Edson Mwakabela (Sativa) kama afisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania ambaye alitoa amri ya kubebwa kwake kisha kusafirishwa kwenda Arusha na katavi kupigwa risasi ya kichwa kabla ya kunusurika kuuawa.
2. ACP Faustine Mafwele amewahi kuwa OC-CID mwaka 2011-2015 wa kituo cha Polisi Arusha na baadae akawa RCO wa Mkoa wa Arusha
Wakati wa mauaji ya wanachama wa CHADEMA maandamano ya Arusha ya 04 January 2011 alikuwa OC-CID.
Wakati huo Faustine Mafwele akiwa na cheo cha ni Mrakibu Msaidizi wa Polisi
Tarehe 05 January 2012 akiwa Mrakibu Msaidizi wa Polisi Faustine Mafwele alipigwa risa