Boniface Jacob: Rais Samia tunaomba Afande Mafwele anayetuhumiwa kumteka Sativa achunguzwe

Boniface Jacob: Rais Samia tunaomba Afande Mafwele anayetuhumiwa kumteka Sativa achunguzwe

Mnatuchosha sana na haya mahabari yenu yasiyo kuwa na kikomo.

Hao watu ulio waorodhesha hapo wewe unadhani ni mjuaji zaidi kuliko walivyo wao?

Nimeshindwa hata kusoma hilo tangazo zima
Umelazimishwa kusoma? au ni kiherehere chako tu ? maana nyuzi ziko nyingi ni kujichagulia tu wa kusoma
 
Sativa ahakikishe Yuko sehemu salama vinginevyo watamtafuta na kumuua tena....

Na wewe Bw. Boniface Jacob unatafutwa Ili aidha ubandikwe kesi moja mbaya sana au uwawe kabisa....

Kuwa makini katika kila unalofanya, unapoishi, kila uendako na kila unayehusiana naye kwa namna zote....

Don't trust anyone including me. Mwamini Mungu muumba wako pekee yake...!
Huyo mwamba atakuwa kajipanga, hakai kizembe
 
Sativa ahakikishe Yuko sehemu salama vinginevyo watamtafuta na kumuua tena....

Na wewe Bw. Boniface Jacob unatafutwa Ili aidha ubandikwe kesi moja mbaya sana au uwawe kabisa....

Kuwa makini katika kila unalofanya, unapoishi, kila uendako na kila unayehusiana naye kwa namna zote....

Don't trust anyone including me. Mwamini Mungu muumba wako pekee yake...!
Umeeleza kitu sahihi kabisa.
Wahusika wanapaswa kuwa waangalifu muda wote kabisa, wasipende kumuamini mtu yoyote yule kirahisi. Wawe waangalifu zaidi na Watu wao wa karibu zaidi ambao wanahusiana nao kila siku katika mizunguko ya maisha yao binafsi, wakiwamo na ndugu zao wa karibu zaidi
 
MAMBO YAKISHAKUWA WAZI KWA NAMNA HII, PUBLICITY YAKE IKO JUU KIASI HIKI, RAIS NI LAZIMA AFANYE JAMBO, HUWA HAKUNA NAMNA TENA!
Kwa vipi nyie wa mrengo ule huwa mnaweka comments kwa herufi kubwa kubwa?
Faiza, big show, na wale wengine. Huwa mnahisi herufi ndogo hazionekani? Huwa ni culture yenu mrengo huo au ni jazba
 
1. Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
2. Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Hamad Masauni.
3. Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Camillus Mongoso Wambura
4. Jaji Mkuu wa Tanzania, Ibrahim Juma
5. Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob Nkunda
6. Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, DIGS, Suleiman Mombo
7. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Hamza Johari

1. Mheshimiwa Rais, Wakati huu nchi ikiwa katika taharuki kubwa na sintofahamu ya watu kutekwa na kupotea kwa watu kisha mauaji ya kiongozi wa CHADEMA Makao Makuu, Ali Muhammad Kibao.

Niruhusu nimlete kwenu mtumishi wa serikali na afisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ACP Faustine Mafwele katika tuhuma za Mtanzania Mwenzetu Edger Edson Mwakabela (SATIVA).

2. Mheshikiwa Rais, napenda kukukumbusha kwamba, Edger Edson Mwakabela (Sativa) kijana ambaye alitekwa 23 June 2024 na kupatikana 27 June 2024 akiwa amejeruhiwa na risasi ya kichwa katika mapori ya hifadhi ya Taifa ya katavi, Mkoa wa Katavi na baadae RAIS ukamchangia matibabu ya jeraha la risasi kiasi cha Tsh Millioni 30.

3. Mheshimiwa, Rais Edger Edson Mwakabela kwa sasa amepona na hana itilifafu yoyote ya kumbukumbu wala akili pamoja na kupitishwa na katika madhira makubwa ya ukatili mbaya sana dhidi ya binadamu.

4. Mheshimiwa Rais, 27 June 2024 Edger Edson Mwakabela akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Mkoa katavi alihojiwa na gazeti la Nipashe kwa njia ya video



Katika mahojiano hayo SATIVA anasema kwa kumbukumbu kuwa alitekwa Jumapili usiku na kupelekwa katika Karakana ya Kituo cha Polisi Oysterbay na siyo kituoni ndani kabla ya kusafirishwa kupelekwa Mkoani Arusha na baadae Katavi.

5. Mheshimiwa Rais, kwa muda wote huu Edger Edson Mwakabela alishahojiwa na Jeshi la Polisi na baadae walipotaka maelezo ya nyongeza Edger Edson Mwakabela alikuwa katika upasuaji katika hospitali ya Aga Khan.

Mwezi August Edger Edson Mwakabela aliwataarifu Jeshi la Polisi kuwa tayari ameondolewa vyuma vya taya na sasa yupo tayari kwa mahojiano na Jeshi la Polisi, akawauliza, Je, afike kituo gani na muda gani kwa mahojiano?

Soma Pia:

Kwa masikitiko makubwa Jeshi la Polisi kupitia Afande James wa kutoka Ofisi ya DCI - Dodona, alimjibu kuwa watamtafuta kwa mahojiano siku wakipata nafasi na mpaka leo Jeshi la Polisi halijawahi kupata nafasi ya kumuhoji Sativa.

6. Mheshimiwa Rais, 21 August 2024 baada ya kupotea Vijana watatu wanachama na Viongozi wa chadema Godwin Mlay, Deusdedith Soka na Frank Mbise Watanzania walianza kusambaza watu wanaowatuhumu kwa matukio ya kuteka watu kutoka katika vyombo vya dola, mmoja ya watu ambao picha zao zilisambazwa alikuwa ni ACP Faustine Mafwele

7. Mheshimiwa Rais, Kijana wako Edger Edson Mwakabela alipo iona picha ya ACP Faustine Mafwele, 22 August 20224 alitutaarifu watu wake wa karibu ikiwamo mimi, kuwa mtu yule ambaye picha yake ilikuwa ikisambaa mitandaoni ndiye alifika nje ya Kituo cha Polisi Oysterbay usiku wa Jumapili ya 23 June majira ya Saa 2:00 kuelekea majira ya Saa 3:00 usiku.

Na kwamba ACP Faustine Mafwele alimuhoji Edger Edson Mwakabela maswali matatu 1.Unaitwa nani 2. Unafanya shughuli gani 3.Unajua kwanini upo hapa?

Baada ya mahojiano hayo mafupi ACP Faustine Mafwele aliwafuata watu waliomteka Edger Edson Mwakabela na kwenda kuongea nao mazungumzo ambayo Edger Edson Mwakabela hakuyasikia, kilichofuata hapo ni watu wengine kufika muda kidogo wa baadae na kuanza naye safari ya kwenda Arusha na baadae Katavi walipoenda kutekeleza mauaji waliyopanga

8. Mheshimiwa Rais, upo uthibitisho wa Kieletroniki wa Edger Edson Mwakabela kuwepo eneo hilo siku ya Jumapili ya tarehe 23 June 2024 majira ya 2 na Dakika 45 usiku. Kwa bahati mbaya watekaji wa Edger Edson Mwakabela walisahau kuzima simu yake namba 0757637880 wakati wote waliokuwa nayo tangu wamteke eneo la Kimara Korogwe.

CDR (Call detail Records) ya simu ya Sativa namba 0757637880 inaonyesha kuwa simu yake iliendelea kupigigwa na kupokea meseji ikiwa eneo la Kituo cha Polisi Oysterbay kwa uthibitisho wa mnara aliokuwa anapokelea mawasiliano pamoja na simu yake kusomeka kwa Latitude na longitude za CDR

Bila shaka kwa kupitia CDR ya simu namba 0757637880 ya Edger Edson Mwakabela hakuna wasiwasi kuhusu tuhuma kuwa Edger Edson Mwakabela kufikishwa eneo la Oysterbay.

9. Mheshimiwa Rais, Kijana wako Edger Edson Mwakabela ndiye mtu pekee ambaye amewahi kwenda Kuzimu na kurudi (survivor). Ni mtu pekee aliye hai mwenye ushahidi juu ya nani anatoa amri za watu kutekwa, anashirikiana na kina nani kuteka na wanaoteka wanafananaje na mwisho wanaoteka na kwenda kuua wanavyofanya kazi yao kwa uaminifu.

Liwekwe graride la Utambuzi, Kijana Edger Edson Mwakabela amtambue ACP Faustine Mafwele. Huyu ni ZCO kanda Maalum ya Polisi, Dar es Salaam.

10. Mheshimiwa Rais, ndiyo maana unaona kila Mtanzania anakupinga unaposema unasubiri kuletewa report juu ya matukio ya utekaji na mauaji kutoka kwa Jeshi la Polisi au vyombo vya dola wakati viongozi wakubwa wa Jeshi la Polisi ni sehemu ya watuhumiwa wa kazi hii chafu ya utekaji na mauaji. Je watakuletea report gani kama na wao ni watuhumiwa..?

10. Mheshimiwa Rais, kwakuwa tunaye tayari mtuhumiwa mmoja wa kuanza naye ambaye ni ACP Faustine Mafwele ambaye bado yupo ofisi za umma anatoa amri na anaendelea na usimamizi wa vikosi vya serikali;

1.Tunaomba ahojiwe Edger Edson Mwakabela haraka sana
2.Tunaomba ahojiwe ACP Faustine Mafwele haraka sana
3.Tunaomba ubatilishe uamuzi wako wa sisi wasamaria wema wenye taarifa kupeleka raarifa za utekaji na mauaji kwa Jeshi la Polis.

Badala yake tunaomba uunde tume huru ya Kijaji itakayo kusaidia kubaini ukweli na kukuletea taarifa Juu ya tatizo la utekeji na mauaji ya watu.

Ahsante kwa ushirikiano wako.

Boniface Jacob
Ex-Mayor, Kinondoni & Ubungo.
0712 239 595
The voice of the silenced Majority

Mkuu wa nchi ni kama haoni wala hasikii
 
Inasikitisha sana ,yaani hadi ushahidi wa ki-electronic unaonyesha Sativa likuwa Oyserbay na hadi aliye -engineer utekeaji ametajwa lakini hakuna kiilchofanyika mpaka sasa ,Mh Samia atambue si kwamba enzi za nyerere ,mwinyi,mkapa hayo mambo yalikuwa hayafanyiki ,yalikuwa yanafanyika ila waliofanyiwa ni wale watu kweli ambao walikuwa wanahatarisha usalama wa taifa na si hawa wa sasa wanaoikosoa serikali tu pale inapokosea.

Yaani mtu amepiga picha ufa kwenye majengo anatekwa wakati pale ananusuru wanafunzi wasije poromokewa na ghorofa ,mtu anasema maisha magumu anatekwa ,ni upuuzi na ndiyo maana kila wanachofanya wanahaibika ,wamempiga SATIVA lakin kapona na anawataja.
Alafu mjinga Nchimbi anakuja na stori za mazungumzo.
Anaenda zjngumza nini ni vitu vipo wazi?
 
Tume ya kijaji inaweza kuaminika kweli? Si itaurudisha mpira kwa Serikali kama lile sakata la Bunge kubariki HGA na IGA za DPW 🤔
Hili sakata linahitaji uchunguzi ufanywe na vyombo huru bobezi tena vya kimataifa.... Historia hupenda kujirudia!! Tuliishawahi kumwomba mkoloni atusaidie kubaini moto uliozuka stong room ya BOT wakati fulani, Tuwaombe Scotland yard waje wafanye uchunguzi.:KasugaYeah:
Majaji hawawa kina biswalo na feleshi?
 
Tume ya kijaji inaweza kuaminika kweli? Si itaurudisha mpira kwa Serikali kama lile sakata la Bunge kubariki HGA na IGA za DPW 🤔
Hili sakata linahitaji uchunguzi ufanywe na vyombo huru bobezi tena vya kimataifa.... Historia hupenda kujirudia!! Tuliishawahi kumwomba mkoloni atusaidie kubaini moto uliozuka stong room ya BOT wakati fulani, Tuwaombe Scotland yard waje wafanye uchunguzi.:KasugaYeah:
Nakazia ✍️ ✍️
Majaji wa Tanzania ni makada, machawa, hawaaminiki
 
Back
Top Bottom