nyumba kubwa
JF-Expert Member
- Oct 8, 2010
- 10,309
- 8,379
mkuu umeni inspire sana kusoma vitabu ila ebhu niambie ni vitabu gani ulivyovisoma vikakusaidia kupresent vizur
Kwa sasa nina kitabu kinaitwa Perfect presentation cha Peter Levin and Graham Topping (2006) lakini siwezi sema ndio kimenifundhisha nilikuwa nacho muda tu na sikuwa nakisoma kivile...ila sasa miaka kama 3 na nusu ilopita tulipewa kozi bana ya namna ya kupresent...hiyo kozi naweza sema ilikuwa sumu...ilinifanya ni learn from my mistakes...
Alokuwa anatufundisha alikuwa anatusisitizia wote tuwe na talking points always tunapokuwa tuna present...mimi zilinifanya nilipo present proposal yangu hadi supervisor wangu akanambia hakupenda kwani nilikuwa nategemea sana notes...lakini alitupata wengi sababu proposal ni mtihani...kuna kufukuzwa ukichemsha...kwa hiyo suala la muda wa ku pressent ni muhimu kuliko mbwembwe za how you present...tulikuwa na woga... kweli hatukutoka nje ya talking points most of us....matokeao yake inakuwa kama unasoma speech...yani wizi mtupu...afu huyo mama alitufanya tuone bila ile podium mtu huwezi present...sumu tupu...
Nikapata bahati ya kuwa jirani na baba mmoja amestahafu toka UN huyu akanipa trick nyingine...akasema ukitaka uwe good presenter lazima u memorize unachotaka kuongea...that real worked...
Yani trick ni kujua next slide hata kabla haujaifungua...na kujua kwenye hiyo slide utaongelea nini...presentation ni kama acting...you smile ...you tease people with questions that they don't have to answer; or you let them answer if they want to etc...na haina uhusiano wa kujua lugha or not...you don't have to be a native English speaker to be a good presenter ...we have many who are real bad na ni natives....
Sasa wengi unakuta anaanza kushangaa anatafuta cha kuongea na audience nayo inakosa imani na wewe...nikisema memorize haina maana hujui unachoongea ila umepangilia cha kuongea...unakuwa na flow ambayo ni coherent na inayoweka wasikilizaji kwenye suspense of what will be next....wanasema you need to tell your story...hata kama ni Biology you still can tell a story...
Kuna mdada ali present kuhusu topic ambayo ina uhusiano na nutrition (ni medical doctor) ...cha kwanza alichofanya alituonyesha picha mbili...moja ya mtu katoka supermarket kanunu makeki na lots of junk food...nyingine ya mtu alonunua vegetables na other healthy staff.... Akaanza kwa kutuuliza,...if you were the first person how would you feel after stepping out of the supermarket....watu 'Guilty'....unaona aliweza ku involve the audience kiasi kwamba hata miye si mtaalamu wa lishe ninaikumbuka presentation yake..she had a story to tell us...while presenting her technical work...begin with a story and finish with something memorable...yani kila mtu alikuwa anamsikiliza mwanzo mwisho maana we felt like we knew her topic already...
Siri kubwa ya kuwa presenter mwenye mvuto ni ku find a story to tell that people can remember... pili be ana expert to whatever you are presenting and memorize what you are to talk...all these needs rehearsal...ukisha master utakuwa unatamani kila siku upewe chance kuongea badala ya kukimbia kwa woga...
Nina ma supervisor wawili...moja hakuwepo akati na present lakini aliniomba eti nimtumie slides zangu maana amesikia habari zangu...nilimtumia lakini moyoni nikawa nasema it's not about slides ...it is about the presentation...na niliwa suprize mbaya maana supervisor alokuwepo alishazipitia slides zangu lakini hakujua kuwa ntamalizia na video clip ya 5 minutes (hiyo ilikuwa siri yangu maana nilijua kama muda hautaruhusu si lazima)...na hapo nilimuuliza chair if I still had time...akasema una 7 more minutes...ndio nikawaambia haya basi tumalize na hii video...siwezi iweka hapa maana nachofanyia research ni sensitive na kinagusa maslahi ya watu...nkiweka watanijua maana walinisumbua sana wakati niko field...