Book reading: Unasoma au Umesoma kitabu gani ungependa wengine wakisome?

Book reading: Unasoma au Umesoma kitabu gani ungependa wengine wakisome?

mkuu umeni inspire sana kusoma vitabu ila ebhu niambie ni vitabu gani ulivyovisoma vikakusaidia kupresent vizur

Kwa sasa nina kitabu kinaitwa Perfect presentation cha Peter Levin and Graham Topping (2006) lakini siwezi sema ndio kimenifundhisha nilikuwa nacho muda tu na sikuwa nakisoma kivile...ila sasa miaka kama 3 na nusu ilopita tulipewa kozi bana ya namna ya kupresent...hiyo kozi naweza sema ilikuwa sumu...ilinifanya ni learn from my mistakes...

Alokuwa anatufundisha alikuwa anatusisitizia wote tuwe na talking points always tunapokuwa tuna present...mimi zilinifanya nilipo present proposal yangu hadi supervisor wangu akanambia hakupenda kwani nilikuwa nategemea sana notes...lakini alitupata wengi sababu proposal ni mtihani...kuna kufukuzwa ukichemsha...kwa hiyo suala la muda wa ku pressent ni muhimu kuliko mbwembwe za how you present...tulikuwa na woga... kweli hatukutoka nje ya talking points most of us....matokeao yake inakuwa kama unasoma speech...yani wizi mtupu...afu huyo mama alitufanya tuone bila ile podium mtu huwezi present...sumu tupu...

Nikapata bahati ya kuwa jirani na baba mmoja amestahafu toka UN huyu akanipa trick nyingine...akasema ukitaka uwe good presenter lazima u memorize unachotaka kuongea...that real worked...

Yani trick ni kujua next slide hata kabla haujaifungua...na kujua kwenye hiyo slide utaongelea nini...presentation ni kama acting...you smile ...you tease people with questions that they don't have to answer; or you let them answer if they want to etc...na haina uhusiano wa kujua lugha or not...you don't have to be a native English speaker to be a good presenter ...we have many who are real bad na ni natives....

Sasa wengi unakuta anaanza kushangaa anatafuta cha kuongea na audience nayo inakosa imani na wewe...nikisema memorize haina maana hujui unachoongea ila umepangilia cha kuongea...unakuwa na flow ambayo ni coherent na inayoweka wasikilizaji kwenye suspense of what will be next....wanasema you need to tell your story...hata kama ni Biology you still can tell a story...

Kuna mdada ali present kuhusu topic ambayo ina uhusiano na nutrition (ni medical doctor) ...cha kwanza alichofanya alituonyesha picha mbili...moja ya mtu katoka supermarket kanunu makeki na lots of junk food...nyingine ya mtu alonunua vegetables na other healthy staff.... Akaanza kwa kutuuliza,...if you were the first person how would you feel after stepping out of the supermarket....watu 'Guilty'....unaona aliweza ku involve the audience kiasi kwamba hata miye si mtaalamu wa lishe ninaikumbuka presentation yake..she had a story to tell us...while presenting her technical work...begin with a story and finish with something memorable...yani kila mtu alikuwa anamsikiliza mwanzo mwisho maana we felt like we knew her topic already...

Siri kubwa ya kuwa presenter mwenye mvuto ni ku find a story to tell that people can remember... pili be ana expert to whatever you are presenting and memorize what you are to talk...all these needs rehearsal...ukisha master utakuwa unatamani kila siku upewe chance kuongea badala ya kukimbia kwa woga...

Nina ma supervisor wawili...moja hakuwepo akati na present lakini aliniomba eti nimtumie slides zangu maana amesikia habari zangu...nilimtumia lakini moyoni nikawa nasema it's not about slides ...it is about the presentation...na niliwa suprize mbaya maana supervisor alokuwepo alishazipitia slides zangu lakini hakujua kuwa ntamalizia na video clip ya 5 minutes (hiyo ilikuwa siri yangu maana nilijua kama muda hautaruhusu si lazima)...na hapo nilimuuliza chair if I still had time...akasema una 7 more minutes...ndio nikawaambia haya basi tumalize na hii video...siwezi iweka hapa maana nachofanyia research ni sensitive na kinagusa maslahi ya watu...nkiweka watanijua maana walinisumbua sana wakati niko field...
 
By best 3 books kati ya nilivyosoma mwaka huu 2014 ni hivi vifuatavyo;

3. Seven Habit of highly effective people by Stphene Covey

2. The Secret by Rhonda Bryrne

1. Kwaheri Ukoloni, kwaheri uhuru by Dr. Haith Ghasamy
 
Red Giant, mwaka huu niliutoa kwa ajili ya kusoma biblia, nimesoma (sio kwa roho kama wanavyoambiwa waamini) na kugundua mapungufu, uongo, kukosekana kwa ukubalifu wa dhana zake na upotoshwaji wa historia, imani na utamaduni.

Nimekuwa na mtazamo mpya juu ya 'maandiko matakatifu'!

Aione: MR. CONFIDENT

ukusoma kwa roho that's why ukagundua huh ushetani ulioandika
 
Last edited by a moderator:
inawezekana haujapata vinavyo kukonga roho. mi kuna vitabu vingi nimeishia njiani ila vingine nasoma hadi usiku mrefu. kuna mdau aliwahisema kusoma isiwe adhabu bali tukufurahie. i hope utapata vinavyokupendeza.

sasa mkuu fanya kunipa list ya vile vitakavyokonga roho nivitafute nisome kwanzia mwakani lakini
 
I've always been an omnivorous reader.

So I read a whole bunch of different things - blogs, newspapers (I even read The Gleaner...now how many in here even know what that is?), The Encyclopedia Americana, the Encyclopaedia Britannica.....

You name it I read it.

But right now I've been busy reading my dad's work - from the time he was a student in the US all the way to his college/ university teaching career.

Hahaha,

The Gleaner as in from Jamdown?

Kingston society ukikosa "Sunday Gleaner" wana ku disown.

Bounty Killer anakwambia atakufanyia halafu kesho watu wasome kwenye Gleaner.
 
Hahaha,

The Gleaner as in from Jamdown?

Yup...you got it.

Kingston society ukikosa "Sunday Gleaner" wana ku disown.

Bounty Killer anakwambia atakufanyia halafu kesho watu wasome kwenye Gleaner.

Nakumbuka wakati niko mdogo sana (early 80s) kuna siku nilienda na mshua Nkrumah hall kusikiliza hotuba ya Edward Seaga, waziri mkuu wa zamani wa Jamaica.

Si kwamba hata nilikuwa najua huyo Edward Seaga ni nani, la hasha. Ni kwamba tu mshua hakupata babysitter baada ya kunichukua kutoka kwenye daycare ya chuo (enzi hizo kulikuwa na daycare ya faculty and staff wa UDSM).

Sikuelewa kabisa huyo jamaa alichokuwa anakiongea lakini kila mara watu walikuwa wanapiga makofi. Wakati tunarudi nyumbani ndo nikaanza kumdadisi mshua.

Baadaye nilipoanza kujifunza kusoma na kuandika nikawa na mazoea ya kusoma soma chochote kilichokuwa kwenye meza ya kahawa.

Kila baada ya muda fulani nikawa naliona hilo gazeti. Ikabidi nimwulize mshua hilo gazeti linaitwaje naye akaniuliza kama nakumbuka nilipoenda naye pale Nkrumah kumsikiliza yule mgeni aliyekuja kutoa hotuba na akanambia hilo gazeti ni la nchi anayotoka huyo mgeni.

Kuna kipindi kwenye miaka ya 70 na 80 UDSM ilikuwa na faculty members kutoka nchi za Caribbean, Jamaica ikiwa mojawapo. Colleague mmoja wa mshua alikuwa na subscription (kupitia snail mail) na ndo huyo alikuwa akimpa kopi mshua.

Hii experience yangu ni ushahidi tosha kwamba wazazi wana influence kubwa sana kwa watoto wao hususan during formative years.

Mimi isingekuwa mshua sina hakika kama hata ningejua kuna gazeti linaitwa The Gleaner.
 
Duh, mchizi umemuona Edward Seaga Nkrumah Hall?

Mimi hata sijajua kwamba Seaga alishafika bongo.

Gleaner ukiwa msikilizaji wa reggae/dancehall halafu unasikikiza lyrics kama mimi huwezi hukosi kulijua.

Wanalitaja sana.
 
mimi nimesoma vitabu vufuatavyo,

1. 168HRS You have more time than youth - ni kitabu kinachofundisha kuwa muda upo mwingi. Kuna mifano hai ya watu waliofanikiwa katika suala hili, ukikisoma kwa utulivu hautabaki kama ulivo. Misisitizo ni kuinvest katika key competency yk.
2. The Monk who sold his Ferrari - inspirational book safi sana.

3. Managing Difficult projects - techniques za kuendesha miradi sumbufu kikiwa na case study za kutosha.

4. Prophets and Kings - kitabu kinaelezeamanabii na wafalme wote wa bibilia na jinsi Mwenyezi Mungu alivyokuwa akifanya nao kazi. Utajifunza kulikuwa na watu wakorofi, vigeugeu, wenyemisimamo, waovu, jasiri, Pia Mungu ukifanya uovu wowote ule siku ukiamua kumrudia yeye hana shida kabisa.

5. Mwanzo na Kutoka - Vitabu vya bibilia vinavyofundisha dunia hii imetoka wapi na kwa nini tuko katika taabu, vita mashaka. pia vitu tunavyoviona leo sio vipya vimewahi tokea zamani. Uhusiano wa Mungu na ISRAEL (familia ya jamaa mmoja anaitwa yakobo)

6. Take Charge of your life -inspirational audio za Jimm Lohn

7. Inspirational Speeches of Dr Otabil Mensah.

8. miday's touch by robert kiyosaki

Mwakani ni mpango wa kumaliza Bibilia Nzima, Ni rahisi maana natumia KJV Dramatized audio huku nafuatilia kwa hard copy ya bibilia. unakuwa unasoma kama vile upo kwenye tukio. zaidi ya hilo nahitaji kusoma vitabu zaidi ya kumi nikianza na why nations fail. Lakini mwisho wa siku niwe na uwezo wa kuandaa articles za kuelimisha jamii kutokana na elimu nitakayoipata.

Ni kazi lakini naamini tatizo huwa sio muda tatizo ni nia.
sure mkuu, tatizo siyo muda ni nia. inaonekana why nations fail kimetushika wengi.
 
Wakuu mwaka unaelekea ukingoni na ni wakati wa kujitathmini. Mi napenda tujitatmnini juu ya vitabu tulivyosoma mwaka huu kama ilivyo desturiyetu ya kila mwaka. Mimi nimesoma vifuatavyo.

MOSSAD: kimeandikwa na Nissim Mishal na Michael Bar-Zohar. Hiki kitabu kinazungumzia missions kubwa kuwahi kufanywa na shirika la kiijasusi la Israel (Mossad). Toka kukamatwa kwa wanazi walioua wayahudi, kupambana na waarabu, kupambana na “magaidi” , na hadi leo wanavyopambana na jitihada za Iran kuwa nuclear power. Ni kama novel ya kijasusi tofauti ni kwamba haya yalitukia kweli.

THE DARK SIDE OF NYERERE: kimeandikwa na Ludovick Kaijage. Anaelezea jinsi alivyoshikwa na kuwekwa kizuizini na usalama wa taifakipindi cha cha Nyerere kwa kuhisiwa uhaini. Ni kitabu rahisi chenye kurasa 87 na kinavutia kusoma. Shida ni kuwa mhandishi hajasema kama kweli alipanga uhaini au la. Ila kinasaidia kutoa mwanga jinsi usalama wa taifa wanafanya kazi na incompetence yao.

AFRICA IS IN A MESS, what went wrong and what should be done: kimeandikwa na Godfrey Mwakikagile. Kakitabu simple kenye kurasa 60 . kakitabu hakachoshi kusoma. Ila naona jamaa kaelezea tu jinsi Africa iko kweny mess ila hajasema what went wrong and what should be done.

THE FATE OF AFRICA: kimeandikwa na Martin Meredith. Kinaelezea historia ya Africa kiuchumi na kisiasa toka uhuru mpaka miaka ya 2000’s. hakuna nchi imeachwa humo. Ni kitabu kizuri mno na sehemu zingine kinachekesha sana.

CURRENCY WARS; kimeandikwa na James Rickards. Kinazungumzia jinsi sarafu zinatumika kama silaha. Leo kuporomoka kwa ruble ni sehemu ya currency war. Ni kitabu kizuri.

THE ART OF WAR: ili kikuingie usome kikiwa na maelezo ya ziada. Mi nilikisupplement na documentary ya history channel inaitwa the art of war.

AMERICA THE BEAUTIFUL: kimeandikwa na Ben Carson. Kinazungumsia principles zilizoifanya marekani ifike ilipo, jinsi inavyochepuka na jinsi ya kuzirudia.

THE BRIEF HISTORY OF TIME: kimeandikwa na prof Stephen Hawking. Kinaelezea historia ya universe toka big bang. Kuna mambo yanachangamsha sana akili japo kuna concepts sikuweza kuzielewa. Nilikusupplement na documentaries kama through the wormhole na Hawking.

WHY NATION FAIL: kimeandikwa na Daron Acemoglu na James Robinson. Hiki kitabu bado nakisoma ila naona ndiyo best kati ya nilivyosoma mwaka huu. Hiki kinajibu ishu ya Mwakikagile ya what went wrong and what should be done.

THE KNIGHT IN AFRICA: kimeandikwa na mtanzania ambaye ni freemason, sir Chande. Kkinazungumzia maisha ya huyu jamaa aambaya kafanya ishu mbalimbali ndani yah ii nchi. Bibliographies na memoirs huwa zinavutia kusoma ila uhonest wake unakuwaga questionable.

NO LONGER AT EASE: ni kitabu kizuri cha Chinua Achebe.

We mwaka huu umesoma nini?

Katika nyuzi za miaka iliyopita naona hawa walikuwa wachangiaji, karibuni nyote.

Mkuu kwanza hongera kwa kweli, nadhan kuanzia mwakani ni lazima kubadili mtazamo haiwezekani mwaka uishe mtu hata vitabu vitatu hujasoma ni hatare sana hii,mwaka ujao kwa kweli lazima uwe mwaka wa mabadiliko kwa kila jambo.
 
great thread indeed,congrats y'all for good readings n insight..
well for me naonaga I read everything I lay my hands on hadi smtym sikumbuki headings,I.simply seek knowledge..
this December nakumbuka two readings I just finished,1.Rules of work na 2.Business Writing...authors ntaweka badae ,they are good ones kwa wanaofanya kazi maofisini
 
mimi wakati huu nilikuwa na wakati mgumu, nimesoma vitabu viwili, THE AUTOBIOGRAPHY OF BEN RANKLIN, POWER OF POSITIVE THINKING na sasa naendelea na THE LIFE OF MAHATMA GANDHI. najitahidi nimalize kabla mwaka haujaisha. kama kuna mwenyeji wa mwanza anielekeze mahala pa kupata novels nzuri maana tokea nihamie hapa napata shida sana
 
ukusoma kwa roho that's why ukagundua huh ushetani ulioandika

Kusoma kwa roho ni turufu inayotumiwa na watawala wanaotumia jina la Mungu ili kuficha mapungufu yao. Biblia ina mikanganyiko mingi ambayo inaitoa thamani ya kuwa kitabu cha rejea kiimani. Kuna mauwaji makubwa, zinaa zilizohalalishwa, sadaka za binadamu, kuhalalishwa kwa utumwa na mambo mengi ambayo si ya Kimumgu.

Kwa kusoma kwa roho na kusubiri mwongozo kutoka kwa kiongozi wa kiimani hakuwezi kukufunulia haya.
 
Wakuu mwaka unaelekea ukingoni na ni wakati wa kujitathmini. Mi napenda tujitatmnini juu ya vitabu tulivyosoma mwaka huu kama ilivyo desturiyetu ya kila mwaka. Mimi nimesoma vifuatavyo.

MOSSAD: kimeandikwa na Nissim Mishal na Michael Bar-Zohar. Hiki kitabu kinazungumzia missions kubwa kuwahi kufanywa na shirika la kiijasusi la Israel (Mossad). Toka kukamatwa kwa wanazi walioua wayahudi, kupambana na waarabu, kupambana na “magaidi” , na hadi leo wanavyopambana na jitihada za Iran kuwa nuclear power. Ni kama novel ya kijasusi tofauti ni kwamba haya yalitukia kweli.

THE DARK SIDE OF NYERERE: kimeandikwa na Ludovick Kaijage. Anaelezea jinsi alivyoshikwa na kuwekwa kizuizini na usalama wa taifakipindi cha cha Nyerere kwa kuhisiwa uhaini. Ni kitabu rahisi chenye kurasa 87 na kinavutia kusoma. Shida ni kuwa mhandishi hajasema kama kweli alipanga uhaini au la. Ila kinasaidia kutoa mwanga jinsi usalama wa taifa wanafanya kazi na incompetence yao.

AFRICA IS IN A MESS, what went wrong and what should be done: kimeandikwa na Godfrey Mwakikagile. Kakitabu simple kenye kurasa 60 . kakitabu hakachoshi kusoma. Ila naona jamaa kaelezea tu jinsi Africa iko kweny mess ila hajasema what went wrong and what should be done.

THE FATE OF AFRICA: kimeandikwa na Martin Meredith. Kinaelezea historia ya Africa kiuchumi na kisiasa toka uhuru mpaka miaka ya 2000’s. hakuna nchi imeachwa humo. Ni kitabu kizuri mno na sehemu zingine kinachekesha sana.

CURRENCY WARS; kimeandikwa na James Rickards. Kinazungumzia jinsi sarafu zinatumika kama silaha. Leo kuporomoka kwa ruble ni sehemu ya currency war. Ni kitabu kizuri.

THE ART OF WAR: ili kikuingie usome kikiwa na maelezo ya ziada. Mi nilikisupplement na documentary ya history channel inaitwa the art of war.

AMERICA THE BEAUTIFUL: kimeandikwa na Ben Carson. Kinazungumsia principles zilizoifanya marekani ifike ilipo, jinsi inavyochepuka na jinsi ya kuzirudia.

THE BRIEF HISTORY OF TIME: kimeandikwa na prof Stephen Hawking. Kinaelezea historia ya universe toka big bang. Kuna mambo yanachangamsha sana akili japo kuna concepts sikuweza kuzielewa. Nilikusupplement na documentaries kama through the wormhole na Hawking.

WHY NATION FAIL: kimeandikwa na Daron Acemoglu na James Robinson. Hiki kitabu bado nakisoma ila naona ndiyo best kati ya nilivyosoma mwaka huu. Hiki kinajibu ishu ya Mwakikagile ya what went wrong and what should be done.

THE KNIGHT IN AFRICA: kimeandikwa na mtanzania ambaye ni freemason, sir Chande. Kkinazungumzia maisha ya huyu jamaa aambaya kafanya ishu mbalimbali ndani yah ii nchi. Bibliographies na memoirs huwa zinavutia kusoma ila uhonest wake unakuwaga questionable.

NO LONGER AT EASE: ni kitabu kizuri cha Chinua Achebe.

We mwaka huu umesoma nini?

Katika nyuzi za miaka iliyopita naona hawa walikuwa wachangiaji, karibuni nyote.

Kiranga, Roulette, EMT, The Boss, Nyani Ngabu, nyumba kubwa Mzee Mwanakijiji, Horseshoe Arch, LORDVILLE, jeba, Mwelewa, Laleyo, Habdavi, AL SHARPTON, leo.leo, Mjuni Lwambo, MSEZA MKULU, Makirita Amani, Kanigini,
hongera msomi mwenzangu. nimesoma vitabu kiasi japo ratiba inabana. kati ya vingi nimesoma acres of diamond, the richest man in babylon, (very interesting educative books on how to make money and keep it), nimerudia the merchants of Venice, na the struggle from within, the walk to fredom cha mandela, na the davinch code. na vingine vingi. ( hiyo list yako nitaipata duka gani?)
 
Last edited by a moderator:
1 the summons john grisham
2 the chambers john grisham
3 33 concise strategy of war jina limenitoka kidogo,
4 Re-membering Africa by WATHIONG'O
5 Why nations fail.
6. Dead Aid by Dambisa moyo
7. just a matter of time by james hadley chase
8. The things men do by james hadley chase
9 The guilty are Afraid by james hadley chase
10. How to win friends and influence people by Carnege
11. The world in my pocket James hadley chase
12. nimerudia How Europe underdeveloped Africa by Dr Walter Rodney
13. blood harvest by Richard kunzman
kwa sasa nasoma romantic novel inaitwa The lost wife by Maggie Cox.

welcome to the fans of john Gresham. tafuta the firm-the best of john gresham, hautalala mpaka uimalize.
 
COMPLETE GUIDE IN PUBLIC SPEAKING - by Nick Jackson

WORLD GRAND SPEECHES - by Payal Kalia D.litt

GAY TRAVEL IN THE MUSLIM WORLD - by Michael T. luongo.

SUCCESSS THROUGH POSITIVE THINKING - by S.P Sharma

HOMOSEXUALITY IN ISLAM - Scott Siraj al-Haqq Kugle.
 
snipa ilikuwaje ukawa innterested na homosexuality?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom